Somo La 6 | Kipaumbele Cha Ahadi

Somo limetafsiriwa na Mgune Masatu


(Wagalatia 3:15-20)

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2011, Bruce N. Cameron, J.D. Marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya New International Version (NIV), copr. 1973, 1978, 1984 International Bible Society, isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo. Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya NIV inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji wa Biblia wa Zondervan. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sehemu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na hukulipata kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

Utangulizi: Mwanzo 15:6 inasema kuwa “Ibrahamu akamwamini Bwana, naye akamhesabia jambo hili kuwa haki.” Paulo anatuambia kwamba hii ndio kanuni aiwazayo Mungu kwa ajili yetu. Tunatakiwa kumwamini na kumtumaini Mungu. Tukifanya hivyo, hiyo inatosha kwa sisi kuwa na uhusiano sahihi na Mungu. Hiyo ndio tiketi yetu ya kuingilia mbinguni. Lakini je, hii ni sahihi? Vipi kuhusu ukweli kwamba Mungu aliwapa watu wake Ahadi Kumi kupitia kwa Musa? Vipi kuhusu ukweli kwamba Yesu aliufanya utiifu uwe mgumu zaidi kwa kusema kuwa kitendo cha kuangalia kwa “kutamani” kilikuwa ni sawa na kuzini “moyoni” na mtu kuwa na hasira kunamwingiza kwenye hukumu sawa na mtu aliyeua anavyohukumiwa (Mathayo 5)? Zungumzia juu ya kuweka viwango kuwa vya juu na vyenye ukali! Paulo anajadili athari za sheria katika somo letu la juma hili. Hebu tuzame kwenye Biblia yetu ili tujifunze zaidi!

I.                   Ahadi

A.                Soma Wagalatia 3:15. Unadhani “agano la mwanadamu” ni kitu gani? (Agano ni mkataba, makubaliano kati ya watu wawili (au zaidi).)

1.                  Fikiria mara ya mwisho uliposaini mkataba. Je, uliahidi kufanya jambo lolote? Je, upande wa pili uliahidi kufanya jambo fulani? (Wanasheria wanaziita ahadi hizi “consideration.” Kila upande katika mkataba unaahidi kutimiza jambo fulani.)

B.                 Angalia tena Wagalatia 3:15. Paulo anasema kuwa jambo gani haliwezi kutendwa kwenye mkataba uliosainiwa? (Unakubaliana na kuenenda na vigezo na masharti yaliyokubalika. Huwezi kuomba mambo ya ziada, na huwezi kutenda kwa uchache pungufu ya ulivyoahidi.)

1.                  Je, huo ndio uzoefu wako? (Paulo anazungumzia jambo linaloweza kutekelezwa. Anazungumzia jambo linalofikirika. Ukitoa ahadi yako kwenye mkataba, unapaswa kuitimiza. Ukikubali kwamba mtu mwingine anapaswa kutenda jambo mahsusi, usimtarajie atende zaidi ya makubaliano.)

C.                 Soma Wagalatia 3:16-17. Unawezaje kuhusianisha Ahadi Kumi na mjadala tuliokuwa nao hivi punde kuhusu ahadi za mkataba? Ikiwa mkataba unasema kwamba Mungu anakuchukulia kuwa u mwenye haki ikiwa unamtumaini, utakuwa na mjibizo (reaction) gani katika kuongezea Ahadi Kumi? (Nitalalamika juu ya uvunjaji wa mkataba. Hata nitalalamika kwa nguvu na sauti kubwa zaidi ikiwa Mungu ataniambia kuwa kanuni hizo zitatafsiriwa kwa namna ya ukali kadri iwezekanavyo! Nitajenga hoja kwamba Mungu ananitaka kutenda mambo mengi zaidi ya yale yaliyomo kwenye mkataba wa awali (halisi).)

1.                  Paulo anamaanisha nini hapa? (Mungu hatafanya hivyo. Sheria haikutolewa kama sehemu ya mkataba wa awali kati ya Mungu na wanadamu. Ilitolewa kwa malengo mengine. Mkataba wa awali unabaki kama ulivyo.)

II.                Mzao

A.                Soma tena Wagalatia 3:16 na ujikite kwenye mjadala wa “mzao” na “wazao.” Je, Paulo anasema kwamba mkataba huu haukuwa kati ya Mungu na Ibrahimu (na uzao wake), badala yake ulikuwa kati ya Mungu, Ibrahimu na Yesu?

1.                  Mungu anawezaje kuingia mkataba baina yake? Mungu Baba aliingia mkataba na Mungu Mwana?

2.                  Kuna mashaka yoyote kwamba “mzao” ni Yesu? (Paulo anasema kwa umahsusi kabisa kwamba mzao ni Kristo.)

B.                 Angalia tena mwanzoni mwa Wagalatia 3:17. Je, Paulo anatarajia kwamba tunaweza tusielewe jambo hili? (Anasema, “Nisemalo ni hili….” Sielewi hiki kinachoonekana kuwa ni mkataba na Yesu, hivyo tunatakiwa kuangalia kama Paulo ataliweka bayana hapo baadaye.)

C.                 Soma Wagalatia 3:18. Sasa Paulo anaingiza msamiati mwingine wa kisheria, “urithi.” Urithi unahusianaje na kile tunachokijadili? (Mtu anaweza kurithi haki za kimkataba. Tuchukulie kwamba baba yako amekubali kumkodisha mtu ardhi kwa miaka kumi kwa $ 10,000 kwa mwaka. Baba yako akifariki, na ukairithi ardhi, utaichukua ardhi hiyo kwa mujibu wa mkataba – ikimaanisha kwamba utaiendeleza ahadi na utaendelea kunufaika kutokana na ahadi iliyowekwa na mtu mwingine. Nadhani Paulo anatuambia kuwa tulirithi matamanio ya Ibrahimu kwenye mkataba kati ya Mungu na Ibrahimu.)

D.                Soma Wagalatia 3:19. Hii inabainishaje mkanganyiko wa awali juu ya Mzao? (Badala ya kusema kwamba “Mzao” ni mnufaika wa mkataba, inasema “Mzao” ni kiini cha mkataba. Hiyo inaleta mantiki kamilifu kwangu!)

III.             Torati

A.                Hebu tuangalie sehemu ya Wagalatia 3:19 inayozungumzia “lengo” la torati. Inaeleza kuwa lengo la torati ni lipi? (Iliingizwa “kwa sababu ya makosa,” na ina ukomo wa matumizi.)

1.                  Ikiwa Yesu alitii torati kwa niaba yetu, na sisi hatuko chini ya adhabu ya torati, kwa nini pawepo na hitaji la torati kujazilizia ombwe hadi Yesu alipokuja? Kwa nini wahitaji jambo jingine lolote lile? (Fikiria taswira pana. Je, Mungu anataka tutende dhambi? Kwa dhahiri, hapana. Yesu alikuja na kuishika torati kwa sehemu fulani ili kuonesha kuwa Adamu angeweza kuishika torati. Kuishika sheria ni jambo jema. Yesu alipokuja, hakutuonesha tu jinsi ya kuishi (kutuonesha “zaidi ya torati” ilikuwa jambo la kufikirika, kuishika torati pekee ilikuwa ni kuwa na malengo ya chini sana), bali pia alimpeleka Roho Mtakatifu ili atusaidie kuishi maisha yanayoendana na mapenzi ya Mungu. Tulihitaji kiongozi.)

B.                 Soma Wagalatia 3:19-20. Nimejumuisha kifungu cha 19 kwa sababu nataka kujikita kwenye rejea ya “mjumbe.” Unadhani huyu mjumbe ni nani? Musa? (Soma 1 Timotheo 2:5-6 na Waebrania 9:15. Kwa dhahiri vifungu hivi vinamwita Yesu Mpatanishi wetu – hususani kwa sababu ya kifo chake kwa ajili (niaba) yetu.)


1.                  Angalia tena Wagalatia 3:19. Je, Yesu aliiweka sheria “katika utekelezaji kwa njia ya malaika?” Ni kwa jinsi gani torati ilikuwa sehemu ya upatanisho? (Soma Warumi 5:10 na 2 Wakorintho 5:17-19. Mungu ni mtakatifu na sisi sio watakatifu. Watu wa Mungu, wakati wakiwa utumwani Misri, kwa hakika walipoteza na kuachana na lengo la Mungu maishani mwao. Katika kuwasaidia waweze kuendana vizuri zaidi na mapenzi ya Mungu, aliwapatia torati. Hivyo, nadhani kwamba Musa ndiye “mpatanishi” wa awali. Hata hivyo, Yesu ndiye Mpatanishi wa kweli alipoishi na kufa na kulipa adhabu kwa ajili ya dhambi zetu.)

2.                  Paulo anamaanisha nini kwa kuadika kwamba “Mungu ni mmoja?” Hii inahusianaje na Yesu kuwa “Mpatanishi?” (Mpatanishi hawakilishi upande wowote. Katika sheria ya sasa ya Marekani, mpatanishi anajaribu kuzileta pande mbili zinazopingana ili zifikie makubaliano. Yesu ni Mungu kamili na mwanadamu kamili. Yeye ni Mmoja pamoja na Mungu. Hivyo, Yesu, katika namna isiyo ya kawaida kupita zote, ametuleta na kutukutanisha pamoja na Mungu.)

C.                 Soma tena sentesi ya kwanza ya Wagalatia 3:19 na kisha usome sentesi ya kwanza ya Wagalatia 3:21. Tutajifunza Wagalatia 21 juma lijalo, lakini kwa sasa ninataka uangalie maswali mawili yaliyoulizwa kwenye hivi vifungu viwili. Je, maswali yote mawili yanatuuliza jambo moja? (Ndiyo. Ikiwa tunaweza kuelewa lengo la torati, basi tunaweza kuelezea ikiwa inapingana na mkataba wa awali (asili) kati ya Mungu na Ibrahimu.)

1.                  Kwa kuangalia lengo la jumla la Mungu kwa ajili yetu, je, torati inakinzana na mkataba?

2.                  Mungu alimtaka Ibrahimu afanye nini? (Amtumaini yeye!)

3.                  Kwa nini Mungu awatake wanadamu wamtumaini? (Wataishi (watakaa) kwa amani na Mungu. Tutakuwa na tumaini kwamba njia ya Mungu na mapenzi ya Mungu vilikuwa vitu bora kabisa kwa ajili ya maisha yetu.)

4.                  Torati inatutendea nini? (Soma Warumi 7:7. Torati inayafunua mapenzi ya Mungu kwa ajili yetu. Je, unataka kufahamu jinsi ya kuishi kwa amani na mapenzi ya Mungu? Soma Amri Kumi.)

5.                  Vipi kuhusu maoni ya Yesu juu ya tamaa na hasira kuwa matatizo yanayolingana na uzinzi na mauaji? Je, mwelekeo huo ni jambo linalotusaidia kuwa na amani na Mungu? (Soma Yakobo 1:13-15. Wanadamu hawatumbukii kwenye uzinzi na mauaji bila kutarajia. Kitendo huanza na tamaa, mpango unapangiliwa akilini, ili kutenda matendo haya. Nadhani anachokimaanisha Yesu ni kwamba ikiwa hufanyi uzinzi au mauaji kwa sababu tu huna fursa ya kufanya hivyo, maisha yako hayaendani na mapenzi ya Mungu. Ikiwa unapanga kufanya uzinzi au mauaji, basi maisha yako hayaendani na mapenzi ya Mungu.)

D.                Tunapaswa kuishije basi? (Tukiyakiri maisha, kifo na ufufuo wa Yesu kwa ajili yetu, tunao uhakika kwamba adhabu ya dhambi haihusiki kwetu. Tumeokolewa. Wakati huo huo, tunapoishi maisha yanayoongozwa na Roho Mtakatifu, tunatambua kwamba yale yote aliyoyafanya Yesu yalilenga kutupatanisha na Mungu. Kwa msaada wa Roho Mtakatifu, tunachagua kuyaelekeza mawazo yetu na maisha yetu kwa namna inayoendana na amri zilizofunuliwa na Mungu. Tunafanya hivi kwa kuwa tunamtumaini Mungu. Tunajua kwamba hii itayaboresha maisha yetu, na tunafahamu kwamba hii itampa Mungu utukufu!)

E.                 Rafiki, je, unakubali na kukiri kile alichokitenda Yesu kwa ajili yako? Je, utakubali kumtumaini katika yote uyatendayo?


IV.             Juma lijalo: Njia ya Kuiendea Imani.

Somo La 5 | Imani Katika Agano La Kale

Somo limetafsiriwa na Mgune Masatu

(Wagalatia 3:1-14)
Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2011, Bruce N. Cameron, J.D. Marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya New International Version (NIV), copr. 1973, 1978, 1984 International Bible Society, isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo. Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya NIV inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji wa Biblia wa Zondervan. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sehemu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na hukulipata kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.
Utangulizi: Nilipokuwa mdogo, kulikuwa na programu kwenye televisheni iliyokuwa inaitwa “Kurogwa.” Katika somo letu juma hili, Paulo anawaambia Wagalatia kwamba “wamerogwa.” Tunafahamu kwamba Wagalatia wasingekuwa wanatazama televisheni kupita kiasi! Je, Paulo anazungumzia juu ya kupagawa pepo? Nimeangalia tafsiri ya “Strong” juu ya neno la Kiyunani na linamaanisha “kupumbaza (kwa kutumia mbinu za uongo).” Tusingependa kupotoshwa juu ya injili, hivyo hebu tuzame kwenye somo letu la barua kwa Wagalatia ili tuubaini ukweli!
I.                   Kurogwa
A.                Soma Wagalatia 3:1. Kwa nini ufahamu wa mateso ya Yesu ni muhimu ili “kutokurogwa?” (Soma Wagalatia 2:21. Tulimalizia somo la juma lililopita kwa ujumbe huu – ikiwa tunadhani kuwa tunaweza kuokolewa kwa matendo yetu, tunakidhihaki kifo cha Yesu kwa ajili yetu. Kudhihaki kile ambacho Yesu ametutendea ni kosa kubwa sana.)
B.                 Soma Wagalatia 3:2. Ni muhimu kiasi gani “kumpokea Roho?” (Kwa namna Paulo anavyoandika jambo hili, ni uthibitisho wa muhimu sana kwamba maisha yako ya Kikristo yapo kwenye msitari sahihi. Paulo anawakumbusha kwamba Roho Mtakatifu hakuwaendea kutokana na wao kutii matendo ya sheria.)
1.                  Je, umegundua jambo ambalo Paulo analizungumzia? Makanisa yanayoonekana kujikita kwenye sheria yamekauka kama mifupa. Hawana (wanapungukiwa) Roho Mtakatifu. Kwa upande mwingine, makanisa yaliyojaa watu wanaofurahia kukubaliwa kwao kwa imani wanaonekana kujawa Roho. Je, haya ndio maoni yako?
C.                 Soma Wagalatia 3:3-4. Wagalatia wametesekea nini bure? Mateso hayo ni yapi na jambo gani ni bure? (Kubadili imani yako ya dini kutakufarakanisha na marafiki na wanafamilia. Kwa kuwa kila dini, isipokuwa Ukristo, imejengwa juu ya matendo kwa namna fulani, Paulo anasema kwamba baada ya kuteseka kutokana na uamuzi wako wa kubadilika, sasa unarejea kwenye matendo yako. Hivyo, kubadilika kwako kulikuwa bure.)
D.                Soma Wagalatia 3:5. Paulo anahusianisha nini na kuwa na Roho Mtakatifu kanisani? (Miujiza.)
1.                  Ikiwa hatuna miujiza, na katika eneo la dunia hii ninakoishi ninadhani kwamba tunapungukiwa/hatuna miujiza ya “hakuna anayeweza kuwaamulia,” je, hiyo inamaanisha kuwa hatuna Roho Mtakatifu? (Ninaamini kuwa mjukuu wangu wa kike aliponywa kimiujiza baada ya kuzaliwa. Lakini, naweza kufikiria jinsi baadhi ya watu wanavyoweza kusema juu ya jambo hili. Ubashiri wangu ni kwamba wewe pia unao uzoefu wa kufanyiwa/kuona miujiza, lakini miujiza hiyo si sawa na ile miujiza mbalimbali ya Mathayo 12:22-23 – kila mtu anashangazwa nayo. Kutokuwepo kwa miujiza ya namna hii katika eneo langu leo hunitaabisha.)

2.                  Je, miujiza inaweza kutokana na kuishika sheria? (Hapana! Ninachokiona kuwa ni sababu ya kutokuwepo miujiza ni kwamba tunajikita zaidi kwenye sheria kuliko neema na Roho Mtakatifu. Panaweza kuwepo sababu nyingine, kwa mfano, kwamba hatuna udhibiti juu ya kazi ya Mungu, lakini hili ni jambo la kulichukulia kwa umakini.)
II.                Ibrahimu
A.                Soma Wagalatia 3:6. Je, kuhesabiwa haki kwa njia ya imani ni fundisho la Agano la Kale? (Ndiyo! Fikiria mfumo wa patakatifu. Ulimchinja mnyama na damu yake ilifanya upatanisho wa dhambi zako. Huo si wokovu kwa njia ya matendo, huo ni wokovu kwa njia ya kifo cha mnyama. Naam, tunajua kwamba jambo hilo lilikuwa linazungumzia kifo cha Yesu katika siku zijazo.)
B.                 Hebu tusome utangulizi wa kauli ya Paulo juu ya Ibrahimu. Soma Mwanzo 15:4-6. Ibrahimu anaamini nini? (Kwamba atampata mwana na uzao mkubwa.)
1.                  Kwa nini imani huleta haki? Kwa nini tusisema kuwa imani huleta “watoto?” (Hii inaonesha kwamba jambo halisi na la msingi ni kumtumaini Mungu. Je, tunaamini anachokisema Mungu na kile alichokitenda na atakachotutendea?)
C.                 Soma Wagalatia 3:7-9. Kwa nini kusema kwamba injili ilitangazwa “mapema kabla” kwa Ibrahimu? Je, injili (kuhesabiwa haki kwa njia ya imani) haikutolewa tangu kipindi hicho? (Hii ilikuwa ni kabla ya kutolewa kwa Amri Kumi pamoja na sheria nyingine zilizotangazwa na Musa. Dhana iliyopo ni kwamba kila kilichofuatia, fundisho la msingi lilikuwa ni kuhesabiwa haki kwa njia ya imani.)
III.             Laana
A.                Soma Wagalatia 3:10. Hivi karibuni, nilikuwa ninatafakari jinsi ninavyoweza kushiriki injili na mtu aliyekuwa anakaribia kufariki, na alikuwa anaichukia dini kwa kiasi fulani. Nina uhakika mtu huyu anadhani kwamba “mimi ni mtu mwema sana, sina hitaji la kitu kingine chochote kile.” Je, huu ni mtazamo unaoleta laana? (Ndiyo. Mtu anaposema, “mimi ni mwema na ni mtu bora zaidi kuliko watu wengine wengi tu ninaowafahamu,” mtu huyo anadhani kuwa wokovu wake unatokana na matendo yake. Tatizo la njia hiyo ni kwamba haitoshi kuwa bora zaidi ya watu wengine. Unatakiwa kuwa mkamilifu, unatakiwa “kuendelea kutenda kila jambo lililoandikwa kwenye Kitabu cha Sheria.”)
B.                 Soma Wagalatia 3:11-12. Je, unapata wakati mgumu kutafakari wazo la kwamba mtu anayejtahidi sana kuishika sheria anaweza kulaaniwa? Huyu ni “mtu mwema.” (Kuyatii mapenzi ya Mungu ni jambo jema. Tatizo ni kuutegemea utiifu huo kwa ajili ya wokovu wako.)
1.                  Watu wangapi wanayategemea matendo yao kwa ajili ya wokovu na hawajui kuwa wanayategemea? (Utaona kwamba Paulo anawazungumzia wale wanaoishika sheria: “Mtu atendaye mambo haya ataishi kwa imani.” Hii inatoa taswira ya mtu mtiifu, na anayeamini kuwa jambo hili huleta stahili ya kukubaliwa na Mungu.)
C.                 Soma Wagalatia 3:13. Je, adhabu, laana ya sheria ilitundikwa juu ya nani? (Yesu. Alilipa adhabu kwa ajili ya dhambi zetu. Alilaaniwa ili kutukomboa kutoka kwenye laana.)

1.                  Ikiwa tunayategemea matendo yetu kwa ajili ya wokovu, je, tunaichukua laana? (Ndiyo!)
D.                Siku za hivi karibuni, nimekuwa nikipambana na dhambi mahsusi. Sina chembe ya shaka mawazoni mwangu kwamba Mungu anatamani tuwe watiifu, kwa ajili ya manufaa yetu na kwa ajili ya utukufu wake. Tatizo ni kwamba ninaposhindwa, ninadhani kuwa kitendo hiki kinaathiri kwa kiasi kikubwa sana uhusiano wangu na Mungu. Wakati huo huo naamini kuwa kitendo hiki kinakiuka maelekezo ya Paulo kwamba hatupaswi “kutegemea” ushikaji wa sheria. Una maoni gani?
1.                  Je, itakuwa sahihi kuamini kwamba kila (wewe na mimi) tunapoielekea haki, anguko lolote linaathiri maisha yetu ya hapa duniani, haliathiri uhusiano wetu na Mungu?
2.                  Soma Warumi 7:4-6. Hapa Paulo anatuambia kuwa tunapaswa kuishi kwa mujibu wa maelekezo ya Roho Mtakatifu. Hii inaashiria kwamba ikiwa “tunadhibitiwa” na asili ya dhambi, kimsingi tunakuwa na tatizo la kiuhusiano na Roho Mtakatifu. Unawezaje kuelezea kwa ufupi ukweli juu ya mapambano dhidi ya dhambi? (Hiki ndicho ninachokifikiria: Roho Mtakatifu akaaye ndani yetu anasimama mahali pa sheria katika kuyaelekeza matendo yetu. Tunapopambana na dhambi, ni Roho Mtakatifu ndiye anayetenda kazi pamoja nasi. Tusichoweza kukifanya ni kumpuuzia Roho Mtakatifu. Katika mapambano haya, bado tunaokolewa kwa neema. Kazi ya Roho Mtakatifu ni kuyapatanisha zaidi maisha yetu na mapenzi ya Mungu.)
E.                 Soma Wagalatia 3:14. “Ahadi aliyopewa Ibrahimu” ni ipi? Watoto wengi? (Soma tena Wagalatia 3:6. Mbaraka unaozungumziwa hapa ni kuhesabiwa haki. Fursa hii sasa imeongezwa kwetu sisi tusio Wayahudi.)
1.                  Ni jambo gani tunalolipokea kwa imani? (Ahadi ya Roho Mtakatifu.)
a.                   Hii inaongezea msisitizo wa Roho Mtakatifu. Nilidhani lengo lilikuwa ni kuhesabiwa haki kwa njia ya imani, badala ya karama ya Roho Mtakatifu. Kwa nini Paulo anabainisha karama ya Roho Mtakatifu kama matokeo ya imani yetu? Hii inaturejesha kwenye Warumi 7:6. Mbadala wa kuzishika Amri Kumi sio kuishi kwa namna yoyote ile unayoichagua. Mbadala ni kwamba “tupate kutumika katika hali mpya ya Roho.”)
F.                  Rafiki, ikiwa unaamini (kama nilivyokuwa ninaamini wakati fulani), kwamba kuzishika Amri Kumi ni muhimu sana kwa ajili ya wokovu, unaweza kuona jinsi kitendo hicho kinavyoweza kukutumbukiza kwenye kulaaniwa? Kwa kuwa ni hakika kwamba utashindwa katika juhudi zako za kuishika sheria yote, utapungukiwa (utaukosa) ukamilifu, na hivyo utaukosa wokovu. Yesu anatupatia kitu kingine. Anatupatia fursa, kwa njia ya ubatizo, kushiriki kifo chake kwa ajili ya dhambi zetu, na ufufuo wake kwa ajili ya uzima wa milele. Anatupatia uchaguzi wa kuishi maisha yanayoongozwa na Roho Mtakatifu. Je, utakubali, sasa hivi, “ofa” ya Yesu?

IV.             Juma lijalo: Kipaumbele cha Ahadi.

USHINDI HATIMAYE | ALL SERMONS DAVID MMBAGA & PAUL SEMBA

Katika maisha haya,kuna tabia za ajabu ambazo wengi zimewazuia wasisonge mbele kiroho na kimaisha. Wakati mwingine unazifanya kwa kujua au kutokujua. Sikiliza na Tazama somo hili.
Usisahau kupakua Maombi App na ku subscribe haps Youtube.
               
               
               
               
                 
                  
                 
                 

        Ushindi Hatimaye 2017 EPISODE 18-     Wachungaji 3 wabatizwa, maswali  &majibu - Mchungaji Mmbaga   

       

Ni toleo jipya toka kwa THE CHEN wakitokea Arusha, barikiwa na Audio Acapella hii…..

Waimbaji wa The Chen walianza wakiwa wanne yaani Elifuraha Msese, Joseph Senguo, Esther Meda na Rebeca Mtinga na huku muhasisi wa kikundi alikuwa Elifuraha Msese.

Elifuraha Msese alipata wazo hili la kuanzisha kikundi mara baada ya kufikiria kufanya kitu cha tofauti katika mziki wa injili kwa mtindo wa akapella yaani uimbaji usiotumia ala na ndipo alikutana na wenzake hawa ambao alisoma nao.
Barikiwa na wimbo wao wa NJOONI KWANGU

Somo La 4 | Kuhesabiwa Haki kwa Imani Pekee

Somo limetafsiriwa na Mgune Masatu


(Wagalatia 2:15-21, Warumi 7)

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2011, Bruce N. Cameron, J.D. Marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya New International Version (NIV), copr. 1973, 1978, 1984 International Bible Society, isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo. Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya NIV inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji wa Biblia wa Zondervan. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sehemu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na hukulipata kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

Utangulizi: Juma hili tunaanza mjadala juu ya kiini cha injili – ni kwa jinsi gani Mkristo anaokolewa kutoka kwenye dhambi zake. Ni muhimu sana kuelewa jambo hili kwa usahihi. Unakumbuka kwamba katika Wagalatia 1:8 Paulo anasema kuwa wale wanaofundisha injili ya uongo wanapaswa “kulaaniwa milele.” Nitajaribu kuelezea jambo hili kwa usahihi! Jambo la muhimu zaidi ya kile ninachokiandika, angalia kwa makini kile anachokiandika Paulo ili uweze kuyaelewa mapenzi ya Mungu kwa usahihi kabisa. Hebu tuzame kwenye somo hili la muhimu kabisa!

I.                   Wayahudi Dhidi ya Mataifa

A.                Soma Wagalatia 2:15-16. Utakumbuka kwamba tulipohitimisha mjadala wetu wa somo lililopita, Paulo alihoji kuwa Petro alikuwa anaenenda kama mnafiki katika kujitenga na Mataifa. Nilibainisha kwamba Paulo anapaswa (na anatakiwa) kujenga hoja inayojengwa juu ya Biblia. Je, hiyo ndio hoja uliyoahidiwa? Hoja iliyojengwa juu ya Biblia? (Hapana, sio kwa kiasi hicho. Badala yake, Paulo anawaambia Wayahudi kutafakari uelewa wao juu ya tofauti zilizopo kati ya Wayahudi na Mataifa.)

1.                  Tofauti hiyo ni ipi? (Soma Warumi 2:17-18. Wayahudi walikuwa na uhusiano wa pekee na Mungu. Aliwapa sheria nyingi ili kuyafanya maisha yao kuwa bora zaidi kuliko watu wa Mataifa waliokuwa wakiwazunguka. Wahayudi walikuwa “nuru” miongoni mwa giza la Mataifa.)

2.                  Licha ya huu uelewa kwamba Wayahudi walipendelewa na sheria na kuwa na uhusiano wa pekee na Mungu, je, Wayahudi walioongoka na kuingia kwenye Ukristo pia wanaonesha nini? (Kwamba hawahesabiwi haki kwa sheria. Badala yake, wanahesabiwa haki kwa njia ya imani katika Yesu.)

a.                   Je, tunapaswa kuamini jambo hili kwa kuwa tu waongofu wa mwanzo wa Kiyahudi waliamini hivyo?

B.                 Soma Warumi 2:21-24. Hivi punde tumesoma sehemu ya kwanza ya hoja ya Paulo hapa – kwamba Wayahudi wanapendelewa kwa kupewa sheria na kuwa na uhusiano wa pekee na Mungu. Matokeo ya kuwa na huu uhusiano wa pekee ni yapi? Je, waliishika sheria iliyokuwa mbaraka wa pekee kwao? (Hapana. Badala ya kuwa nuru, hawakumtii Mungu na walimkufuru kwa matendo yao ya dhambi.)

1.                  Ni jambo gani hilo basi ambalo waongofu wa Kiyahudi walilijua linalopaswa kutufanya tukiri kwamba sheria haituokoi? (Walifahamu kwamba wasingeweza kuishika sheria.)

2.                  Hebu tusiache jambo hili katika mawazo ya watu tusiowafahamu. Je, unafahamu kwamba mara kwa mara huwa unaivunja sheria? (Kama utajibu kwa uaminifu, basi utasema kuwa (kama ilivyokuwa kwa waongofu wa Kiyahudi wa mwanzo) “ndiyo, ninaivunja sheria mara kwa mara.”)

3.                  Hebu tupitie tena Wagalatia 2:16. Ukitenda dhambi, je, unaweza “kuhesabiwa haki kwa kuishika sheria?” (Kwa dhahiri, hapana. Paulo haanzi kwa hoja ya kiteolojia, anaanza na uzoefu wa kila mwana na binti wa Adamu na Hawa. “Kwa kuishika sheria hakuna atakayehesabiwa haki.”)

II.                Kuhesabiwa Haki Kwa Njia ya Imani

A.                Wagalatia 2:15-16 inatumia neno “kuhesabiwa haki” mara kadhaa. Unadhani hiyo inamaanisha nini? (Katika mtazamo wa sheria ya Marekani, inamaanisha kuwa unavunja sheria lakini hauchukuliwi kwamba una hatia. Kwa mfano, mtu anavunja mlango na kuingia nyumbani kwako usiku, na unahofia kwamba mtu huyo atakudhuru. Ukimpiga risasi na kumwua mtu huyo anapokuwa anakukaribia, hicho ndicho sheria inachokiita, “mauaji ya haki.” Kumwua mtu kwa makusudi ni kosa la jinai la kutisha. Lakini, katika mazingira haya mauaji ni ya “haki.”)

1.                  Umewahi kuusikia msemo “Umeokolewa kutoka dhambini na si katika dhambi zako?” Ikiwa tunahesabiwa haki hata pale tunapotenda dhambi, je, huu msemo ni wa kweli?

B.                 Soma Wagalatia 2:17. Fikiria muktadha wa sheria ya Marekani niliouelezea hivi punde. Je, sheria hii inakuza na kuhamasisha mauaji? Je, inahafifisha sheria dhidi ya mauaji? (Inayaacha mamlaka ya sheria mahali pake. Inasema tu kwamba katika mazingira fulani, utawala wa sheria unakuzwa kwa kumruhusu mtu kujitetea.)

C.                 Soma Wagalatia 2:18. Kitu gani “kilibomolewa?” (Tukitumia jambo hili katika mazingira ya Petro, alipogeukia njia zake za kale kwa kujitenga na Mataifa, alifufua sheria (ushikiliaji mno wa sheria) na, matokeo yake, alijihukumu mwenyewe. Ingawa baadhi ya watu wanadhani kuwa sheria imeangamizwa, nadhani ni sahihi zaidi kuhitimisha kwamba adhabu ya sheria “imeangamizwa” tunapookolewa kwa imani.)

D.                Soma Wagalatia 2:19. Hii inasema kuwa “naliifia sheria.” Haisemi kuwa sheria “iliangamizwa.” Mkristo “anaifiaje sheria?” (Soma Warumi 6:3-7. Tunapobatizwa, tunakufa pamoja na Yesu, na kufufuka pamoja na Yesu. Tunafahamu kwamba Yesu alikufa kwa sababu ya dhambi zetu. Kwa hiyo, sisi (kwa njia ya Yesu) tumelipa adhabu kwa ajili ya dhambi zetu. Tayari tumeshalipa gharama ambayo sheria inatutaka kufanya hivyo kwa ajili ya dhambi. Sheria “haiangamizwi,” bali si tishio tena kwetu kwa sababu tumeshalipa adhabu kamili ya dhambi kupitia kwa Yesu.)

E.                 Soma Warumi 7:1-4. Paulo anasema kuwa sisi ni sawa na mke aliyefiwa mume, na hivyo mwanamke huyo yuko huru dhidi ya sheria ya uzinzi. (Soma Warumi 6:1-2 na Warumi 6:5-7. Vifungu hivi vinatuambia kuwa hatutakiwi kuendelea kutenda dhambi. Vinatuambia kuwa “utu wetu wa kale” ulikufa. Namna bora ya kuelewa jambo hili ni kusema kuwa tuliifia adhabu kwa ajili ya uzinzi – pamoja na adhabu kwa ajili ya kutenda dhambi nyingine yoyote ile. Lakini, hatukufa kutokana na uelewa wa kwamba sheria ipo ili kuyafanya maisha yetu kuwa bora. Hatukufa kutokana na uelewa wa kwamba kuishi kwa mujibu wa mapenzi ya Mungu humpa yeye utukufu.)

F.                  Soma Wagalatia 2:19-20. Je, mtu anayezini “anaishi kwa ajili ya Mungu?” (Kwa dhahiri kabisa, hapana.)

1.                  Kristo anaishije ndani yetu? (Hii inarejea suala la Roho Mtakatifu kukaa ndani yetu.)

2.                  Hebu tutumie mfano. Chukulia kwamba nimesema kuwa ulizifia sheria zote za usalama barabarani. Je, hiyo itakufanya kuwa dereva bora? (Ikiwa ulikuwa umekufa, usingezijua sheria za usalama barabarani. Hivyo, tukichukulia kwamba ungeweza kuendesha ilhali umekufa, basi utakuwa dereva mbaya sana.)

a.                   Sasa chukulia kwamba mtunzi wa sheria zote za usalama barabarani “anakaa ndani yako.” Je, utakuwa dereva wa namna gani? (Endapo ningekuwa nimejawa na mtu aliyetunga sheria zote za usalama barabarani, basi ningekuwa ninazifahamu kwa ukamilifu. Nisingezitii kwa sababu ninaweza kuandikiwa makosa na kupewa adhabu na polisi. Ningezitii kwa sababu nilifahamu kwamba ziliweka mazingira salama ya uendeshaji. Nadhani hicho ndicho anachokimaanisha Paulo.)

G.                Soma Wagalatia 2:21. Mtu anawezaje “kuitenga” neema? (Kwa kudhani kuwa anatakiwa kuishika sheria ili aweze kuokolewa. Kamwe sheria haitatuokoa. Hivyo, ni makosa kuishika sheria kwa kuwa tunadhani ina athari kwenye wokovu wetu. Sio tu kwamba hatuwezi kuishika sheria kikamilifu kutokana na asili yetu ya dhambi, bali kuishika sheria ili tuweze kuokolewa ni kumkashifu Yesu kwa sababu inamaanisha kuwa alikufa bure.)

III.             Sheria

A.                Tumekuwa tukizungumzia sheria. Nilipokuwa mdogo, nilifundishwa na baadhi ya watu kwamba Paulo anarejea “sheria ya mapokeo,” ikimaanisha sheria zilizoandikwa na Musa zikihusiana na huduma za patakatifu. Ninaposoma “commentaries” za zamani za Biblia, inaonekana kuwa baadhi ya watu walioandika maoni hayo wanaamini kwamba Paulo anamaanisha sheria ya mapokeo. Hivyo, nadhani huu ndio uliokuwa (nadhani hata sasa) uelewa miongoni mwa baadhi ya Wakristo. Utakumbuka jambo mahsusi linaloleta mtafaruku (mkanganyikio) ni tohara. Je, hiyo ni sehemu ya sheria ya mapokeo? (Hapana. Muda mrefu kabla ya huduma ya patakatifu, Mungu alimpa Ibrahamu hii sheria. Mwanzo 17:9-11.)

B.                 Ikiwa Paulo hazungumzii sheria ya mapokeo peke yake, je, anajumuisha Amri Kumi? (Soma Warumi 7:7-8. Paulo anazungumzia “amri,” na tunaitambua kama Amri ya Kumi. Kutoka 20:17. Paulo anapoandika kuhusu uzinzi na tamaa kwenye mjadala wake wa “sheria,” tunajifunza kwamba anaamini tulizifia Amri Kumi.)

C.                 Soma Warumi 7:4-5. Tunaweza kudhani kwamba kuiwekea ukomo tafsiri ya Paulo ya “sheria” katika sheria ya mapokeo hutusaidia kuwa na tabia njema. Paulo anazungumzia nini juu ya athari ya sheria kwa tabia njema? (Sheria inaamsha tamaa zetu za dhambi. Unalielewa jambo hili. Mwambie mtu kwamba hatakiwi kutenda jambo fulani, na atataka kulitenda. Hivyo, kuitafsiri sheria kwa mapana (na kisha kusema kwamba tunaifia sheria yote) hutusaidia kuishi maisha bora. Kupitia kwa Yesu, tulilipa adhabu ya kukiuka kila aina ya sheria ya kiroho.)

D.                Soma Warumi 7:6. Sasa tunamtumikiaje Mungu? (Kwa kuishi maisha yanayoongozwa na Roho Mtakatifu!)


E.                 Rafiki, je, umezipata habari njema hapa? Ulipobatizwa, ulishiriki katika maisha makamilifu ya Yesu na kifo chake kwa ajili ya dhambi zako. Adhabu ya dhambi zako imekwishalipwa. Je, sasa utaishi maisha yanayoongozwa na Roho Mtakatifu? Kwa nini usiombe, sasa hivi, kwa ajili ya msamaha wa dhambi na ujazwe Roho Mtakatifu? Kwa nini usichague kuishi maisha yanayoongozwa na Roho?


IV.             Juma lijalo: Imani Katika Agano la Kale.

TAUS YACHANGIA MILIONI 27 KWA AJILI YA MIRADI YA UTUME TANZANIA


 Image may contain: 21 people, people smiling, crowd, tree, child, sky, grass, shoes, outdoor and nature

Mkutano wa Umoja wa  Watanzania Waadventista waishio Marekani  (TAUS)umemalizika hivi karibuni ambapo watanzania hao wakichangia Dola za Kimarekani 12,000 sawa na Shilingii 27 Milioni za Tanzania kwa ajili ya miradi ya utume wa Injili nchini Tanzania.

Mkutano huo uliohudhuriwa na Makamu wa Mwenyekiti wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato Duniani Mchungaji Geofrey Gabriel Mbwana ,Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Vijana ya Kanisa hilo duniani Mchungaji Pako Edson Mokgwane,Mchungaji David Mmbaga toka  Dodoma,Tanzania ulifanyika Columbus,Wisconsin  ambapo hotuba za neno la MUNGU na mada mbalimbali za ujasiriamali,usimamizi wa Biashara  na uendelezaji wa miradi mbalimbali nchini Tanzania 

Wajumbe wa mkutano huo toka katika majimbo mbalimbali nchini Marekani wengine wakiwa na familia zao waliungana kwa pamoja katika kuchangia fedha hizo ambazo zitakwenda kusaidia kwa awamu kuendeleza  miradi ya kuwasomesha wachungaji,ujenzi wa makanisa na vyombo vya habari.

TAUS ilianzishwa mwaka 1999 huko Massachusetts na wanachama 25 kwa lengo la kuwatanisha Waadventista Watanzania walioko nchini humo ambapo kwa sasa inawachama wapatao 300.Waweza kutembelea katika tovuti yao ambayo ni www.tausinc.org