TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI


Shule ya Agape Adventist Pre & Primary School, inawatangazia nafasi za kazi kama ifuatavyo;

WALIMU NAFASI 4
i. MWALIMU WA SOMO LA KISWAHILI – NAFASI 1
SIFA: Awe na uwezo mkubwa/amebobea kufundisha somo la Kiswahili kwa ufasaha
• Awe na diploma (stashahada) au shahada katika somo la Kiswahili na somo jingine la ziada.
• Awe na uwezo wa kuwasiliana kwa lugha ya kiingereza na Kiswahili kwa ufasaha. 


ii. MWALIMU WA DARASA LA KWANZA NA DARASA LA PILI – NAFASI 3
SIFA : Awe na stashahada au shahada ya ualimu na uzoefu wa muda mrefu.
• Awe na uwezo wa kuwasiliana kwa lugha ya kiingereza na Kiswahili kwa ufasaha.
• Awe na uwezo mkubwa wa kufundisha “kusoma” kwa njia ya vitamkwa –Foni (phonics)
• Awe na uwezo mkubwa wa kufundisha “kuandika” kwa ufasaha.
• Awe na uwezo mkubwa wa kufundisha matendo ya hisabati kwa ufasaha


MATRON – NAFASI 1
SIFA: Awe na umri wa miaka 40 au zaidi
• Awe amehitimu angalau elimu ya sekondari
• Awe amesomea taaluma ya lishe au uuguzi
• Awe na uzoefu wa muda mrefu katika taaluma yake
• Awe na uwezo wa kufundisha neno la Mungu na mwenye msimamo mzuri katika mambo ya kiroho
• Awe na uwezo wa kuongoza
• Mwenye uwezo wa kuwasiliana kwa lugha ya kiingereza atapewa kipaumbele. 


NESI (MUUGUZI) – NAFASI 1
SIFA : Awe na umri wa miaka 25 au zaidi na mwenye mapenzi na watoto.
• Awe na cheti katika mafunzo ya uuguzi.
• Awe na uzoefu usiopungua miaka 2
• Awe mtu anayeweza kujisimamia katika kazi yake. 


MLEZI WA WATOTO –NAFASI 2
SIFA : Awe na elimu ya sekondari
• Awe na mapenzi kwa watoto
• Awe mchapa kazi, msafi na mwenye uwezo wa kujisimamia katika kazi
• Mwenye uzoefu wa malezi ya watoto atapewa kipaumbele.
Barua zifikishwe kwa: i) Mkono ofisini Agape pre and Primary School ii) Anuani ya posta.
Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 7 /11/2016 saa 8:00 mchana.
Kumbuka kuandika namba ya simu kwenye barua yako.
Maombi yatumwe kwa: MKUU WA SHULE
AGAPE ADVENTIST PRE & PRIMARY SCHOOL
P.O.BOX 751
MOROGORO
Au tuma kwa E-mail: agapeadventist@gmail.com

No comments:

Post a Comment