KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO MBALIZI LANUSURIKA KULIPUKA MOTO, CHANZO NI KIMBUNGA KILICHOEZUA PAA YA NYUMBA JIRANI NA KANISA HILO.

 Mbeya: Kanisa la Waadventisa wa sabato Mbalizi la Nusurika Kulipuka Moto Tarehe 12/10/2016.
Kanisa la Waadventista wa Sabato Mbalizi Mbeya limenusurika kuwaka moto hii leo Majira ya Saa Tisa Jioni Baada ya Kimbunga kilicho pita eneo hilo Kuezua Paa la Nyumba ya Jirani na Kanisa na kulitupa juu ya Paa la Kanisa na Kufunika Waya za Umeme zilizo pita juu ya paa hilo na kusababisha Cheche kali kutokea Hatahivyo Tanesco kupitia Idara ya dharula Waligundua jambo hili mapema na kuzima umeme katika Eneo hilo.
Mara Baada ya Kutoa Mabati hayo tumegundua kua Hasara chache zilizo jitokeza kwani Dish la King'amuzi cha Ting limeharibika pia Bati 4 za Kanisa zilichimbwa na kuharibiwa kwa mkito wa Hilo paa.
Tunamshukuru Mungu kwani hakuna mtu aliye dhurika katika kimbunga hiki.
Pia Tunapenda kukishukuru kitengo cha Dharula cha Tanesco kwa umakini na Umahili katika kazi yao kwani walichukua hatua mapema na ndani ya Mda mfupi walikuwa wamesha fika katika Tukio hili na kushirikana nasi katika Utoaji wa Paa hilo na hatimaye kurudisha Umeme.
By. Mwanahabari wako Mchungaji Haruni Kikiwa Mchungaji wa Mtaa Mbalizi.

No comments:

Post a Comment