JE UNAJUA KWA NINI HUFANIKIWI?



Una mizigo mingi isiyo ya lazima wala faida ambayo umeibeba:-

1.Umejipa jukumu la kuwa "mpelelezi" wa maisha ya wengine na umesahau maisha yako.

2.Umebeba vinyongo na visasi moyoni vinavyokufanya uwafikirie waliokuumiza zaidi kuliko kufikiria furaha na maendeleo yako.

3. Una marafiki wengi ambao ni kama kupe, wapo kukutumia tu na hawachangii lolote katika maendeleo zaidi ya  kujifanya ndio watu wako karibu lakini kumbe wapo kwa maslahi yao!

4.Umeweka mbele zaidi "watu watanichukuliaje" kuliko kuangalia maisha yako.Watu ndio wanakuchagulia aina ya maisha unayoishi na unajilazimisha kuishi kama wao hata kama huna uwezo huo.

5.Unaongea zaidi ya kasuku lakini vitendo hakuna.Unatamani mafanikio tu moyoni lakini huna mipango ya kuyafikia.

6.Maisha yako yote umeyaweka kwenye mitandao ya kijamii.Huna siri hata moja!Hivyo unalazimika kuishi aina ya maisha ambayo yataendelea kufanana na yale uliyoyaweka kwenye mitandao ya jamii kwa sababu ukibadilika tu watasema "umefulia"

7.Kila aliefanikiwa ni rafiki yako au utasema ni mtu wako wa karibu na unaishia kuwasifia tu na kupiga nao picha lakini hujifunzi kutokana na mafanikio yao na wala hutumii fursa hiyo ya kujuana nao.

8.Upo sahihi kila siku(you are always right). Huambiliki, hushauriki na kila wazo atakalotoa mwenzako basi si zuri ila la kwako ndio sahihi na utataka litekelezwe hilo hilo. Mwisho wa siku kila mtu anakukimbia hakuna wa kukuambia "hapa umekosea" kwa sababu ya ujuaji wako.

9.Hujifunzi maarifa mapya.Mara ya mwisho kusoma kitabu ilikuwa ni "Ngoswe, penzi kitovu cha uzembe" Tena ni kwa sababu ilikuwa ni kwa ajili ya kujibia mtihani. Hujifunzi "life skills" wala ujuzi mwingine.

10.Unazurura mno mitandaoni bila faida. Kwako wewe intaneti ni kwa ajili ya kuchati tu na kufuatilia habari za mjini ambazo tangu umeanza kuzifuatilia hujawahi kuingiza hata shilingi moja, zaidi unateketeza tu hela yako ya vocha.

ISHUSHE hiyo mizigo kama kweli inahitaji kusonga mbele!
 

No comments:

Post a Comment