ADRA YAFIKIA WAHANGA WA TETEMEKO MKOANI KAGERA, YASAIDIA FEDHA TASLIMU NA VITU BAADHI

Na.ABG-ONLINETV

Shirika la Maendeleo na Misaada la kanisa la waadventista wasabato Tanzania (ADRA) limetoa kiasi cha Fedha Taslimu za kitanzania Milioni kumi na Sita(16,000,000/=)  kwaajili ya kusaidia wahanga wa tetemeko la Ardhi lililotokea mkoani KAGERA.Fedha hizo zilikabidhiwa kwa Mkuu wa mkoa wa Kagera Meja Jenerali mstaafu  SALIM MSTAFA KIJUU kutoka kwa Kaimu mkurugenzi wa shirika hilo ELAM BUNDE hapo jana 19/10/2016.


Mbali na Fedha taslimu pia shirika hilo limetoa vitu Taslimu VYANDARUA na BLANKET vyenye thamani ya fedha za kitanzania  ,  Milioni Thelasini(30,000,000).Hivyo kupelekea jumla ya Msaada wa Milioni 46.

No comments:

Post a Comment