KWAYA YA KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO ILALA WATEMBELEA HIFADHI YA SAADAN

Wakazi wa kijiji cha Saadan na majirani zao hasa wanaozunguka Hifadhi ya taifa ya wanyama ya Saadan iliyoko wilaya ya Bagamoyo na Pangani mkoani Tanga, Juma hili wamepokea ugeni mkubwa wa kwaya ya kanisa la Waadventista Wasabato Ilala ya jijini Dar es Salaam, waliotembelea hapo kwa malengo ya kujifunza maajabu ya Mungu katika uumbaji lakini pia kwa lengo la uinjilisti yaani kupanda mbegu kwa njia ya ugawaji wa vitabu na Vijizuu vya neno la Mungu.

Safari kutoka Ilala ilianza saa 9 usiku wa kuamkia Jumapili, na kufika kule majira ya saa 2 asubuhi na kuanza kuzunguka katika hifadhi kutazama wanyama.

Baada ya hapo walipata chakula cha mchana na kisha kujifunza neno la Mungu na baadae kuzunguka katika kila nyumba ya jirani kugawa zawadi ya kitabu cha TUMAINI KUU na baadhi ya machapisho mengine kwa kuanza na wale wote walioshiriki kwenye ile safari kama Dereva na Msaidizi wake, Waongozaji na wafanyakazi wa Hifadhi, wahudumu wa chakula na wageni wengine waliokuwa wametembelea hifadhi kwa siku hiyo na kisha nyumba zote zinazozunguka.

Hapa kuna picha ya tukio zima.


No comments:

Post a Comment