FILADELFIA: - ZAMA ZA UAMSHO (1798 BK ? 1844 BK)

Hiki ni kipindi cha kanisa la Kristo katika zama za uamsho wa kiroho,

Maeneo mengi duniani kote kulikuwa na uamsho mkuu wa kiroho, kuamka kwa injili nchini Uingereza na Uamsho mkuu katika Amerika yalifufua makanisa yaliyokuwepo na kuzidi kuwa imara hadi kuelekea uanzishwaji wa harakati za makanisa ya Baptisti na Methodisti.

Misheni na vituo vya kujifunza biblia, vingi vilianzishwa na wamisionari wa kuzunguka maeneo mapya kama vile David Livingstone walijitokeza.

Kweli muhimu za biblia kama vile Sabato ya siku ya saba na kazi ya Yesu Kristo kama kuhani Mkuu kule patakatifu pa patakatifu zilivumbuliwa tena.�
Katika wakati huu

Uamsho mkuu wa kiroho ulijulisha ulimwengu kwa kiwango kikubwa juu ya kurudi upesi kwa Yesu Kristo.

TABIA ZA KUIGA KUTOKA KWA WATU WA KANISA LA FILADEFIA(Ufunuo 3:8-12)

1:Nguvu ya kiroho.

2:Kushika na kulitunza Neno la Mungu.

3:Kutolikana jina la Mungu

4:Kuwa wavumilivu, Pamoja na kudharauliwa kutokana na kuamini juu ya unabii wa Biblia kuhusu Ujio wa pili wa Yesu Kristo bado walibaki na uvumilivu wakisubiri kurudi kwa Yesu Kristo.

Tukiziishi hizo Tabia hakika Yesu Kristo atatulinda dhidi ya majaribu yote na kutufanya kuwa Nguzo katika hekalu la Mungu kama fahari pekee kutokana na msaada kwa kanisa la Kristo na wokovu wetu ni wa hakika.
 

No comments:

Post a Comment