DR MWAKYEMBE AWAPONGEZA WAADVENTISTA WA SABATO KWA UIMBAJI MZURI WENYE KUMTUKUZA MUNGU.

 Waziri wa katiba na sheria, Mh. Harisson Mwakyembe amewaomba WaadventistaWasabato Tanzania kuendeleza ukarimu na umoja walionao. Lakini pia amewapongeza kwa uimbaji mzuri wenye kumtukuza MUNGU, Wakati huo huo pia amewaomba Viongozi wa kanisa hilo kugonga hadi ofisini kwake endapo kutatokea mtu yoyote atakaemnyanyasa muumini wa kanisa hilo katika swala la UHURU WA KUABUDU.
Waziri huyo ameyasema hayo katika tafrija fupi ya kufunga mikutano ya Injili ya UHURU HATIMAYE iliyokua ikirushwa moja kwa moja LIVE na Runinga ya MORNING STAR pamoja na Radio katika Kanisa la Waadventista Wasabato Ushindi jijini Dar es salaam.


 PICHA/HABARI NA Jackson Mwarangi Sekiete


No comments:

Post a Comment