(Yeremia 1)
Somo hili limetafsiriwa
kutoka katika Copr. 2011, Bruce N. Cameron, J.D. Marejeo yote ya maandiko
yametoka kwenye tafsiri ya New International Version (NIV), copr. 1973, 1978,
1984 International Bible Society, isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo. Nukuu kutoka
kwenye tafsiri ya Biblia ya NIV inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji wa Biblia
wa Zondervan. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye
mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sehemu nyingine
yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Kama huwa una kawaida ya kupokea
somo hili kwa njia ya barua pepe na hukulipata kwa juma moja, unaweza kulipata
kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org
kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa,
Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.
Utangulizi:
Je, Mungu ana mpango kwa ajili ya maisha yako? Je, matendo ya viongozi na watu
wa taifa lako yanaleta tofauti kwa jinsi ambavyo Mungu analitendea taifa lako? Juma
hili tunaanza mfululizo mpya wa masomo kuhusu mtu ambaye Mungu alimwita ili
kulionya taifa lililomgeuzia Mungu mgongo. Hebu tuchinbue somo letu ili tuone
kile tunachoweza kujifunza kuhusu kazi ngumu!
I.
Wito
A.
Soma
Yeremia 1:1-3. Chukulia kwamba unasikiliza kisa fulani, na una mashaka kama
kinaelezea ukweli. Je, utafanya nini hapo hapo, ili kuwa na uhakika zaidi na
kisa hicho? (Unaweza kuulizia kwa undani zaidi. Mtu anayeeleza ukweli atakuwa
na habari za kina zaidi.)
1.
Kuna
habari gani kuu katika mafungu haya ya mwanzo ya kitabu cha Yeremia? (Habari za
kina!)
1.
Mambo
gani yanahitimisha unabii wa Yeremia, ule ulioandikwa kwenye hiki kitabu? (Watu
wake wanakwenda uhamishoni.)
A.
Soma
Yeremia 1:4-5. Mafungu haya yanatoa ushauri gani kuhusu suala la utoaji mimba?
(Mungu anatufahamu tangu mwanzo kabisa. Mungu anatupangia majukumu ambayo
angependa tuyatekeleze kabla hatujazaliwa. Utoaji mimba unaingilia kati mipango
ya Mungu.)
1.
Je,
Yeremia ndiye alikuwa chaguo la kwanza la Mungu kwa ajili ya kutekeleza kazi
yake? (Naam!)
1.
Jiweke
kwenye nafasi ya Yeremia, ingekuwa vigumu kiasi gani kukataa kuitikia wito wa
Mungu? (Mungu aliniambia kwamba ana huu mpango mahsusi kwa ajili ya maisha
yangu – na nilizaliwa mpango huo ukiwepo akilini. Nawezaje kumkatalia Mungu?)
A.
Soma
Yeremia 1:6. Yeremia ana wasiwasi gani? (Kwamba bado ni mdogo sana.)
1.
Ni
jambo gani hasa mahsusi kuhusu ujana wake, linaleta tatizo kubwa? (Uwezo wake
wa kuzungumza.)
1.
Je,
Yeremia anajaribu kumkatalia Mungu? Je, Yeremia anajaribu kusogeza muda mbele? Je,
anaamua tu kuwa mnenyekevu?
A.
Soma
Yeremia 1:7-8. Suluhisho la Mungu kwa wasiwasi wa Yeremia ni lipi? (Mungu
anasema kuwa atamwambia Yeremia mambo ya kusema.)
1.
Tuchukulie
kwamba Mungu anakuita ili uwe mtume/nabii na wewe una wasiwasi kwamba si
mzungumzaji mzuri. Je, woga wako halisi ni upi? (Kwamba utafadhaishwa. Watu hawatakuchukulia
kwamba u mtu mwema.)
a.
Jibu
la Mungu kwa wasiwasi huo ni lipi? (Usiogope. Mungu atakuokoa, Yeremia.)
a.
Una
wasiwasi kiasi gani katika ushuhudiaji unaotokana na uwezekano wa wewe
kufikiria kudhalilishwa?
A.
Soma
Yeremia 1:9. Je, jambo hili linatendaje kazi? Endapo tutafungua kinywa cha
Yeremia, je, tutaona fungu la maneno limeshindiliwa kinywani mwake? Ikiwa sivyo
(na sidhani kama kuna mtu yeyote anatarajia kuyaona maneno), je, Mungu anafanya
nini? (Itakumbukwa kwamba Yesu alipotenda miujiza wakati mwingine alizungumza
na mara nyingine alimgusa mtu. Nadhani mguso ni kwa manufaa ya mtu anayepokea
muujiza. Yeremia anatiwa hamasa kwa mguso na kwamba ana karama ya pekee kutoka
kwa Mungu.)
A.
Soma
Yeremia 1:10. Ikiwa Mungu angekupatia majukumu haya, je, ungeyaelewaje?
1.
Angalia
mpangilio wa majukumu yake. Je, hiyo inaashiria nini? (Atakuwa anabomoa, kuharibu
na kuangamiza kabla ya kujenga.
1.
Chukulia
mpangilio huu kwa kuulinganisha na kazi yetu ya injili. Kwa ujumla mtazamo
wangu huwa ni kujenga juu ya chochote kilichopo. Je, wakati mwingine tunapaswa
kubomoa kabla hatujaanza kujenga?
a.
Ikiwa
hivyo ndivyo, ni wakati gani tutafahamu kwamba kubomoa ndilo jambo sahihi?
(Nitahitaji maelekezo mahsusi kutoka kwa Mungu.)
I.
Kujaribisha
Kifaa
A.
Soma
Yeremia 1:11. Angalia jambo nililolibainisha hapo awali. Hii ni mara ya pili
tunasoma “Neno la Bwana likanijia.” Hiyo inamaanisha nini? Kumbuka mara ya
mwisho Mungu “aligusa” kinywa cha Yeremia. Je, Yeremia yupo katika maono? Je,
kweli Mungu anamtembelea? Jambo gani limekuwa likiendelea? (Kwa jinsi Yeremia
anavyoandika jambo hili anaonekana kuwa kwenye maono.)
1.
Mungu
aliposema “nimetia maneno yangu kinywani mwako,” je, alimaanisha kwamba alimpa
Yeremia uwezo wa kupokea ndoto? (Nadhani. Pia anamaanisha kuwa atamsaidia
Yeremia kuzungumza.)
A.
Soma
tena Yeremia 1:11 na uongezee Yeremia 1:12. Unalielewaje jibu la Mungu? Je,
Mungu ana wasiwasi kwamba maono yanaweza yasifanye kazi?
1.
Kila
ninapotaka kuongea kwa kutumia mikrofoni, mara zote huwa ninaijaribisha. Huwa sipendi
kuijaribisha mara baada ya kuanza kuzungumza. Je, Mungu anaujaribu uwezo wa
Yeremia kuona maono kama ninavyojaribisha mikrofoni? (Nadhani. Suala lililopo
ni kwamba, “Yeremia, angalia jambo hili linawezekana!”)
A.
Angalia
tena Yeremia 1:11-12. Pamoja na “kujaribisha kifaa,” je, Mungu anapeleka ujumbe
halisi? (Maoni mengi ya waandishi huwa yanabainisha kwamba mti wa mlozi ndio
huwa unakuwa wa kwanza kuchanua. Kimsingi huwa unachanua katika majira ya
baridi kali (winter). Endapo unaangalia ishara ya kukaribia kwa kipindi cha majira
ya kuchipua (spring), basi utauangalia mti wa mlozi.)
1.
Unapata
maana gani katika jambo hili? (Mungu anasema kuwa anaanza mchakato wa hukumu
kwa watu wake. Mungu anaangalia jambo hili kwa ukaribu sana ili kuangalia
maendeleo yake, kama ambavyo mtu anavyouchunguza mti wa mlozi ili kuona jinsi
majira yanavyoendelea.)
A.
Soma
Yeremia 1:13-14. Mungu anaongezea nini katika mwendelezo wa jaribio la maono ya
Yeremia? (Mungu anaongezea mtazamo mwingine pamoja na ufafanuzi. Unaweza kuona
mwendelezo wenye mantiki? Kwanza, Mungu anachunguza ili kuona kama Yeremia
anaweza kuona picha (maono) ambayo Mungu anayatuma. Pili, Mungu anaelezea maana
ya picha hizo.)
1.
Hii
inatufundisha nini kuhusu kufanya ushuhudiaji kwa ajili ya Mungu? (Mungu
atatusaidia katika kila hatua.)
I.
Onyo
A.
Soma
Yeremia 1:15. Hapo awali tulisoma kwamba sufuria lenye maji yatokotayo na mdomo
wake “unaelekea” toka upande wa kaskazini, hii ikifanya ionekane kwamba vitu
vilivyomo vichemkavyo vinautishia upande wa kusini. Hii inamaanisha nini?
(Maafa yatatokea upande wa kaskazini na yatautesa upande wa kusini. Katika Agano
la Kale, rejea ya “kaskazini” mara kwa mara huwa inawazungumzia watu wabaya. Hapa
inaonekana kuizungumzia Babeli.)
1.
Neno
picha linamaanisha kwamba “viti vya enzi” vya wafalme wa falme za kaskazini
vitawekwa malangoni mwa Yerusalemu. Unalinganisha mawazo gani na “malango” ya
mji wa nyakati hizo? (Hapo ndipo biashara (Mwanzo 23:10-11) na shughuli za serikali
zinapofanyikia.)
1.
Ipi
basi, ndio iliyo maana ya maono haya? (Wafalme wa Babeli watatawala biashara na
serikali ya Yuda.)
A.
Soma
Yeremia 1:16. Kwa nini ufalme mwovu (Babeli) utekeleze hukumu ya Mungu kwa watu
wa Mungu? (Watu wa Mungu wamemwacha Mungu. Wanafukiza uvumba na kuabudu kazi za
mikono yao wenyewe.)
1.
Hebu
tuchimbue suala hili zaidi. Hakuna jirani yangu hata mmoja anayeabudu sanamu
aliyoitengeneza. Kiini cha dhambi hii ni kipi? (Mungu aliwaumba wanadamu. Wanadamu
wanaweza kutengeneza vitu vingi. Kwa nini wanadamu wanaabudu kitu
walichokitengeneza tofauti na kumwabudu Mungu aliyewaumba? Unaweza kuona jinsi
jambo hili linavyomtukana na kumfedhehesha Mungu? Unaweza kuona jinsi kitendo
hiki kilivyo cha kipumbavu na kisicho na mantiki?
a.
Je,
Mungu anauadhibu upumbavu? (Kwa kweli huku ni kumkataa Mungu kwa kiburi cha
hali ya juu.)
1.
Lengo
la kutengeneza sanamu ni lipi? (Yumkini, itayaboresha maisha yako kwa namna fulani.
Itakulinda au kukuletea vitu.)
a.
Je,
unaziamini fedha ulizozipata kuweza kukulinda na kukuletea vitu?
a.
Je,
unawaamini watu wengine kuweza kukulinda au kukupatia vitu?
a.
Je,
unaweza kuona jinsi tatizo la msingi lilivyo katika kuabudu sanamu leo, hata
kama hatumwoni mtu yeyote akiabudu sanamu halisi?
1.
Je,
inaleta mantiki kwako kuwatumia watu waovu kuwaadhibu watu wa Mungu? Je, tatizo
halipo kwa watu wa Mungu kwamba wameingia uovuni? Kwa nini kuwazawadia watu
ambao tayari ni waovu? (Wakati majengo yenye minara pacha yaliposhambuliwa
mjini New York, watu nchini Marekani waliungana kusema, “Mungu ibariki
Marekani.” Wazo lililokuwepo ni kwamba Mungu anapaswa kuwa upande wa Wakristo
na si Waislam ambao waliangamiza minara hiyo. Lakini, ujumbe kwa Yeremia
unatuambia kwamba Mungu hachunguzi tabia za watu ambao anawatumia kuwaangamiza
watu wake. Hatuwezi kusema kwamba hatutapata adhabu kwa sababu tu tunadhani
kwamba sisi tu wenye haki zaidi kuliko watu wengine.)
A.
Soma
Yeremia 1:17-19. Je, ungependa kuwa Yeremia? Je, utabadilishana naye kazi?
A.
Rafiki,
mara nyingine Mungu anatuchagua kwa ajili ya kutekeleza kazi ngumu. Je,
utamtumaini katika nyakati ngumu?
I. Juma Lijalo: Mgogoro (Kutoka Ndani na Nje)
No comments:
Post a Comment