Somo limetafsiriwa na Mgune Masatu
(Matendo 4, Warumi 1,
Waefeso 2, Ufunuo 20)
Somo hili limetafsiriwa
kutoka katika Copr. 2011, Bruce N. Cameron, J.D. Marejeo yote ya maandiko
yametoka kwenye tafsiri ya New International Version (NIV), copr. 1973, 1978,
1984 International Bible Society, isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo. Nukuu
kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya NIV inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji wa
Biblia wa Zondervan. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi
(kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sehemu
nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Kama huwa una kawaida ya
kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na hukulipata kwa juma moja, unaweza
kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com
kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org
kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa,
Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.
Utangulizi: Viongozin wa dini
wananiambia kuwa lazima injili ihubiriwe kwa kila mtu ili Yesu aweze kurudi
tena. Hawatekelezi jambo hili, kwa kuwa kauli hii inapatikana kwenye Mathayo
24:14. Je, hiki ndicho hasa alichokimaanisha Yesu? Pasipo kulitafakari jambo
hilo, nimelichukulia kiuhalisia. Watu wananichokonoa katika mwelekeo huo kwa
kunionesha sehemu za dunia ambazo bado hazijaisikia injili. Wanasema kuwa
tunatakiwa kuyalenga maeneo hayo, na kisha Yesu anaweza kurudi. Tatizo la
kimantiki linaibuka kwa watu wote ambao tayari wameshafariki kutoka kwenye
maeneo ambayo bado injili haijafika. Vipi kuhusu watu hao? Je, wanaathirije
lengo letu? Hebu tuzame kwenye somo letu la mwisho linalohusu mtu kuwa mmisionari
ili tuone kile Biblia inachokisema!
I.
Jina Pekee
A.
Soma Matendo 4:1-3. Kuna tatizo gani kwenye
mahubiri ya Petro na Yohana? (Walikuwa wanahubiri juu ya ufufuo, na Masadukayo
hawakuwa wakiamini katika ufufuo.)
A.
Soma Matendo 4:5-7. Unadhani kwa nini viongozi
wa Kiyahudi walianza kwa kuuliza swali hili? (Soma Matendo4:8-9. Viongozi wa
Kiyahudi hawaulizi juu ya ufufuo, wanauliza kuhusu uponyaji wa yule mtu dhaifu
(mlemavu). Endapo wanafunzi wangedai kwamba uponyaji ulifanyika kwa njia za
uchawi, basi viongozi wa Kiyahudi wangekuwa na uamuzi mwepesi.)
1.
Unalichukuliaje jibu la Petro? (Kwanza, ni jibu
la busara sana – “je, mlitukamata na kutusweka rumande kwa kumsaidia mtu?” Pili,
inaonyesha mfano wa ahadi iliyopo katika Luka 12:11-12 kwamba Roho Mtakatifu
atatufundisha kitu cha kujibu tutakapopelekwa mbele ya wenye mamlaka.)
A.
Soma Matendo 4:9-12. Unaichukuliaje diplomasia
ya Roho Mtakatifu? (Tuligusia jambo hili katika masomo yaliyopita. Kanuni inayosema
kwamba kamwe tusiwaudhi watu wengine ni ya kijinga. Wakati huo huo, Yesu anatufundisha
kwamba ni vyema kuepuka kutenda makosa katika baadhi ya mistakabali (Mathayo
17:27).)
1.
Wakati Roho Mtakatifu anapoeleza kupitia kwa
Petro kwamba Yesu pekee ndiye anayeweza kutuokoa, je, anaeleza ukweli
unaotamalaki ulimwenguni kote, au anazungumzia tu huu uponyaji mahsusi?
(Tulijifunza kutoka kwa Paulo juma lililopita kwamba hatuwezi kuishi maisha
makamilifu. Hivyo, kuyategemea maisha makamilifu ya Yesu, na kifo chake na
ufufuo wake, ndio njia pekee ambayo wanadamu wanaweza kuokolewa. Huu ndio
ukweli unaotamalaki ulimwenguni kote.)
A.
Soma Yohana 14:6 na Mathayo 28:19-20. Ikiwa watu
wanaweza kuokolewa bila kuisikia injili, kwa nini Yesu anasema kauli hii na
kutoa amri hii?
1.
Hii ina athari gani kwenye suala la endapo ni
lazima watu wote kuisikia injili kabla Yesu hajarudi? (Hii inafanya ionekane
kwamba ujumbe mahsusi kumhusu Yesu lazima uhubiriwe.)
A.
Soma Mathayo 8:11. Tunaambiwa kwamba watu gani
watakuwa mbinguni? (Ibrahimu, Isaka na Yakobo.)
1.
Unadhani walifahamu kwa kiasi gani juu ya
maisha, kifo na ufufuo wa Yesu?
A.
Soma Zaburi 19:1-4 na Warumi 1:18-20. Je, hii
inaashiria nini kuhusu jinsi ambavyo kila mtu anaweza kumjua Mungu? (Utukufu wa
uumbaji unatuelekeza kwa Mungu. Paulo anasema kuwa wanadamu “hawana kisingizio”
katika kumjua Mungu.)
A.
Soma Yohana 14:7. Je, kinyume chake ni kweli,
kwamba tunaweza kujifunza habari za Yesu vya kutosha kwa kumjua Baba?
A.
Hebu tuangalie kama tunaweza kuyaunganisha
mafungu yote haya pamoja na kupata jibu la swali lililouliza kama kweli lazima
watu wote waisikie injili kabla Yesu hajarudi. Je, ni kwa dhahiri kiasi gani
mtu anatakiwa kuelewa na kuyakiri maisha na kazi ya Yesu ili aweze kuokolewa?
(Anachokitamani Mungu ni uelewa mzuri na wa dhahiri kabisa, ndio maana
alitupatia kazi ya kupeleka injili. Lakini, hatimaye, watu wanaokolewa kutokana
na maisha na kafara ya Yesu hata kama hawaielewi vizuri zaidi. Badala yake,
Mungu anatoa aina fulani hivi ya hukumu kutokana na kile kilichofunuliwa kuhusu
yeye (Mungu) kwa njia ya uumbaji na Roho Mtakatifu.)
A.
Soma Kumbukumbu la Torati 29:29. Je, uelewa wetu
wa jinsi Mungu anavyotenda kazi katika suala la wokovu na mambo mengine
umekamilika kwa kiasi gani? (Nadhani hili ni onyo kuhusu kuwa na uhakika sana
katika suala la kubashiri jinsi Mungu atakavyotuokoa. Hata uelewa wetu wa jinsi
Utatu Mtakatifu unavyotenda kazi haujakamilika hata kidogo.)
I.
Nadharia ya Injili
A.
Soma Mathayo 22:37-40. Dini ngapi zinashiriki huu
mtazamo wa “kanuni ya pekee” wa kuonesha upendo na heshima kwa watu wengine na
kumpenda na kumtii Mungu? (Watu wengi.)
1.
Je, hii inamaanisha kwamba watu wema
wataokolewa? Ninamkumbuka baba yangu akisema kwamba alidhani kuwa Winston
Churchil anapaswa kwenda mbinguni kutokana na matendo yake katika Vita vya Pili
vya Dunia. (Baba yangu alipelekwa Uingereza kwenye hatua fulani ya vita.)
A.
Soma Waefeso 2:8-10. Kitu gani kinatuokoa?
(Neema! Tunapata wokovu kwa njia ya imani katika karama ya Mungu. Mungu alituumba
ili tutende matendo mema, lakini hatuokolewi kwa matendo yetu.)
1.
Soma Mathayo 7:13-14. Je, wokovu kwa njia ya
neema pekee inaongeza au kupunguza idadi ya watu wanaookolewa? (Watu wengi
wanadhani kuwa wao ni wema sana, lakini si wengi walio dhati kuhusu kuwa na
uhusiano na Mungu.)
A.
Soma Ufunuo 20:11-15. Je, watu wanahukumiwa kwa
matendo yao? (Wengine wanahukumiwa kwa matendo yao – wale waliopotea.)
1.
Nani ambaye hahukumiwi kwa matendo yake? (Wale
ambao majina yao yameandikwa kwenye Kitabu cha Uzima.)
1.
Hebu subiri kidogo! Je, mafungu haya hayasemi
kwamba “kila mtu alihukumiwa kwa mujibu wa kile alichokitenda?” (Soma Ufunuo
20:4-6. Ili kuelewa jambo hili ni lazima kuelewa kwamba kuna ufufuo wa aina
mbili. Wale ambao majina yao yameandikwa kwenye Kitabu cha Uzima wanafufuliwa
katika “ufufuo wa kwanza.” Miaka elfu baadaye ufufuo wa waovu utafanyika, na
waovu wanahukumiwa kutokana na matendo yao.)
A.
Hebu tuchimbue kwa kina zaidi suala la kupotea
kutokana na matendo yetu, kuokolewa kwa neema, na kile ambacho Biblia
inakifunua kuhusu jinsi Mungu anavyofanya maamuzi. Rejea kwenye Warumi 1:20-23.
Je, ni njia gani ya msingi kabisa ambayo wanadamu wanamkataa Mungu? (Mbingu
zinatuonesha kwamba Mungu yupo, lakini wanadamu waovu wanamkataa kwa kuabudi
kile kilichoumbwa na Mungu, badala ya kumwabudu Mungu.)
A.
Soma Warumi 1:24-25. Inamaanisha nini kusema
kwamba “Mungu aliwaacha katika tamaa za mioyo yao, waufuate uchafu?” (Huu ni
mwendelezo wa kumkataa Mungu. Ikiwa utamkataa Mungu kwa kiwango cha kawaida
kabisa (unamwabudu reptilia – kiumbe mwenye kutambaa, badala ya kumwabudu
Muumba wa wanyama wote), basi Mungu anakuacha utumbukie kwenye dhambi zaidi.)
A.
Soma Warumi 1:26-27. Jambo gani linafuatia “kisicho
cha asili” katika kujikita zaidi kwenye dhambi? (Maelekezo ya kitabu cha Mwanzo
ya mwanaume na mwanamke kuwa mwili mmoja kwa njia ya ndoa, yanabadilishwa na
jambo lililo la asili la muungano wa ndoa ya jinsia moja.)
1.
Hebu tutafakari kidogo mantiki ya Paulo hapa. Huku
sio kuikataa injili, huenda watu hawa hawaifahamu injili. Msingi wa
kuwatenganisha watu wa Mungu na wale wasio watu wa Mungu ni upi? (Warumi
inatuambia kuna mambo ya dhahiri kiasili. Jambo moja ni kumwabudu Muumba badala
ya kiumbe. Jambo jingine ni kufuata ubunifu wa Muumba kwa ajili ya uzao.)
A.
Soma Warumi 1:28-32. Hatua inayofuata katika huu
mwendelezo wa kwenda mbali na Mungu ni upi? (Kwa kuwa hawajifunzi kile ambacho
Mungu anawafundisha kiasili, wanajipenyeza ndani zaidi kuuelekea uovu.)
1.
Hatua ya mwisho katika utelezi huu ni ipi?
(Wanaiidhinisha dhambi.)
1.
Siwezi kuliacha swali hili kwa sababu ya mjadala
unaoendelea sasa kuhusu mapenzi ya jinsia moja (ubasha/usenge). Ikiwa niko
sahihi kwamba Paulo anaelezea kuteleza zaidi na kuingia kwenye dhambi kwa watu
wasioijua injili, je, ni dhambi gani ziko ndani zaidi kuliko usenge? (Ulafi, husuda,
mauaji, ugomvi, ulaghai, uovu wa kudhamiria, usengenyaji/umbeya, kashfa,
kumchukia Mungu, ufidhuli, majigambo na majisifu, pamoja na mengineyo mengi.)
1.
Je, hilo linatufundisha nini kuhusu asili ya
ubasha/usenge? (Kwanza, dhambi iliyoelezewa hapa sio kuvutiwa na jinsia ya aina
moja, badala yake ni kutenda “matendo machafu” ikiwa ni matokeo ya kuvutiwa
huko. Pili, usenge unabainishwa kama kuporomoka kwa uelewa wa dhahiri wa masuala
ya asili. Hakuna mtu hata mmoja anayefikiria kwa usahihi anaweza kuabudu mnyama
badala ya kumwabudu Muumbaji wa wanyama. Hakuna mtu hata mmoja mwenye fikra
sahihi atashindwa kuutambua ubunifu wa mwili wa mwanadamu na mifumo ya uzazi. Kuyakataa
mafundisho ya dhahiri ya Mungu hutuelekeza kwenye matokeo ya dhambi zaidi.)
1.
Mfululizo huu wa dhambi unaendanaje na neema?
(Neema ni kumkiri Mungu. Bila kujali kama unamkiri Mungu kwa uelewa wa kisasa wa
injili, au kumkiri tu kutokana na kile kinachofunuliwa kwenye mambo ya asili,
unakuwa umemkiri Mungu.)
A.
Rafiki, je, unaweza kuona jinsi Mungu
anvyofungua fursa kwa kila mwanadamu ili kumfuata? Unao wajibu na fursa ya
kushiriki ujumbe wa wazi kabisa wa injili, injili ya neema. Je, utajitoa
kufanya hivyo?
I.
Juma lijalo: Tutaanza mfululizo mpya wa masomo
kuhusu nabii Yeremia.
No comments:
Post a Comment