Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis ameripotiwa kukutana na
Kim Daviz karani wa Kentucky ambaye alifungwa jela kwa kukataa kutoa
leseni za ndoa za wapenzi wa jinsia moja,wakati wa ziara yake huko
Marekani.
Wakili wa bi, Davis amesema alikuwa na mkutano wa faragha uliochukua dakika 15 na papa Francis huko Vatican mjini Washington.
Hatahivyo msemaji wa Vatican Frederico Lombardi amesema kuwa hakatai
kwamba mkutano ulifanyika.Bi Davis anapinga ndoa za wapenzi wa jinsia
moja na anahoji kwamba dini yake haimruhusu kutoa vibali kama hivyo.
Alihudumia kifungo cha siku sita mahakamani mapema mwezi huu baada ya
kukiuka agizo la mahakama ya kijimbo kutoa leseni hizo kwa wanandoa wa
jinsia moja huko Rowan mjini Kentucky.
Kim Davis |
Mat Stavers,ambaye ndio wakili wa Davis amekiambia chombo cha habari cha
CBS kwamba bi Davis na mumewe walikuwa wamealikwa kukutana na papa
Francis kufuatia msimamo wake uliotangazwa na vyombo vya habari.
''Papa Francis alimshukuru kwa ujasiri wake na kumwambia aendelee na mwenendo huo'', alisema Bwana Stavers.
N BBCSWAHILI.COM
No comments:
Post a Comment