Makadinali na maasikofu wa kanisa Katoliki mjini Vatican.
Mkutano huo ambao unatarajiwa kumalizika Oktoba 25 mwaka huu na
unaojulikana kama Synodi ulioanza jumamosi kwa misa katika kanisa la
mtakatifu Peter haulengi kubadilisha kanuni au mafundisho ama kanuni za
kanisa hilo bali kuangalia jinsi gani mafundisho yanayotolewa yanaweza
yakaendana na mazingira ya sasa ya kimaisha duniani.
Suala kubwa katika mjadala huo ni juu ya msimamo wa muda mrefu
unaozuia watu waliowahi kuachika katika ndoa na kufunga ndoa tena
kushiriki katika huduma ya sakramenti unavyoweza kubadilishwa na
kuwaruhusu watu wa aina hiyo kushiriki tena huduma hiyo.
Makadinali ndani ya kanisa hilo tayari wameonya ya kuwa kanisa
katoliki linaweza likatumbukia katika mfarakano mkubwa kuhusiana na
utata uliopo katika suala hilo.
Mahusiano ya jinsia moja yaibua mjadala
Suala linalohusiana na mapenzi ya jinsia moja pia ni jambo lingine
linaloibua mjadala ndani ya kanisa hilo. Kauli iliyotolewa hapo juzi na
mmoja wa wanathiolojia wa kanisa hilo kupitia gazeti moja la nchini
Italia ya kuwa ni shoga na amekuwa akiishi na mwanaume mwingine iliibua
pia maswali mengi miongoni mwa waumini na viongozi wa kanisa hilo.
Mwanathiolojia huyo Monsignor Krystof Charasma ambaye ni raia wa
Poland alivuliwa nyadhifa zake zote ndani ya kanisa hilo mara tu baada
ya kukiri hadharani kuhusiana na tabia yake hiyo ya kimaisha.
Msemaji wa kanisa hilo mjini Vatican Padri Federico Lombard alisema
kitendo hicho kinatia doa kanisa hilo na kusababisha kanisa hilo kuwa
katika mijadala isiyotarajiwa ya vyombo katika vyombo vya habari.
Akifungua mkutano huo utakafanyika kwa muda wa wiki tatu kiongozi
mkuu wa kanisa hilo duniani Papa Francis alitetea juu ya umuhimu wa
kulindwa kwa ndoa kati ya mume na mke na kulitaka kanisa hilo kuwa
makini na kutoongozwa na ushabiki wa hoja ambazo zinaweza zikavuruga
misingi ya kanisa hilo.
Aidha Papa Francis alilitaka kanisa hilo kuwatendea haki watu walio
na majeraha ya kisaikolojia miyoni mwao na kuonya kuwa hali ya kuwatenga
watu hao badala ya kuwasikiliza matatizo yao inaonekana kwenda kinyume
cha misingi ya kanisa hilo.
Masuala mengine yanayohusiana na jamii ambayo pia inaundwa na waumini
wa kanisa hilo ambayo Papa Francis amependekeza yapewe nafasi katika
mjadala huo ni pamoja na masuala ya ukosefu wa ajira, mazingira pamoja
na vita.
Mwandishi: Isaac Gamba/ AFPE/DPAE
|
MJADALA VATICAN JUU YA MAGEUZI NDANI YA KANISA KATOLIKI
Takribani
makadinali na viongozi wengine wa kanisa Katoliki duniani wanaokutana
mjini Vatican wamekuwa na mjadala jinsi gani kanisa linavyoweza kuregeza
msimamo juu ya huduma ya sakramenti kwa baadhi ya waumini .
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment