MABALOZI KANISA LA ILALA SDA, WATEMBELEA KUNDI LA MANELUMANGO KISARAWE PWANI.

Jumamosi hii ya Oktoba 3, kundi la vijana katika chama cha Mabalozi katoka kanisa la Waadventista Wasabato Ilala jijini Dar es Salaam, walilitembelea pamoja na kufanya nao ibada kundi lao la Manelumango liliopo Kisarawe Pwani.

Pamoja na kufanya nao Ibada, kwaya ya mabalozi ilipata nafasi ya kushiriki katika uimbaji ulioonekana kuwa kivutio kikubwa kwa majirani waliojitokeza kushuhudia tukio hilo hivyo kupelekea watu 3 kujitoa kubatizwa kufuatia wito uliotolewa na aliyekuwa muhubiri wa siku hiyo muinjilisti Musafiri John.

Pia kundi hlo lilipata nafasi ya kutembelea na kufanya maombi eneo la kiwanja cha kanisa chenye ukubwa wa takribani ekari moja, ambapo kuna njozi kubwa ya kujenga kanisa la kuabudia, Kituo cha Afya na Shule ambavyo vyote ni changamoto kwa wakazi wa eneo hilo.

Kikundi cha uimbaji cha Male voice kutoka kanisa la Ilala SDA wakiimba katika vipindi vya mchana
Vijana walipopelekwa kutembelea kiwanja ambacho kanisa limenunua
Ombi maalum lililofanyika katika eneo la kanisa, likiongozwa na kiongozi wa Mabalozi Abishua Mganga
Wimbo maalum wa kuagana
Muinjililsti Msafiri John akihubiri katika ibada ya asubuhi
Picha wakati wa Mapumzika ya mchana kwa ajili ya chakula
Picha wakati wa Mapumzika ya mchana kwa ajili ya chakula
Picha wakati wa Mapumzika ya mchana kwa ajili ya chakula
Kwaya ya Mabalozi ikiimba

No comments:

Post a Comment