Waumini
wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato nchini Tanzania wametakiwa
kujitokeza kwa wingi siku ya sabato ya leo Oktoba 24,2015 kuchangia
vyombo vya habari vya kanisa hilo Morning Star Radio na Morning Star
Television. Mhazini wa Union ya Kusini Mashariki mwa Tanzania Jack
Manongi ameiambia Morning Star Radio kuhusu muhimu wa vyombo vya habari
katika kueneza utume wa kanisa hilo. Manongi amewashukuru watu
mbalimbali wanaojitokeza kuchangia vyombo hivi vya habari kwa kutoa
fedha zao,kutangaza na kudhamini vipindi mbalimbali katika vituo hivyo
vilivyoko jijini Dar es salaam .
Picha/habari na Mtangazaji Maduhu
No comments:
Post a Comment