(Yohana 4, Mathayo 8 & 15, Luka 17)
Somo hili limetafsiriwa
kutoka katika Copr. 2011, Bruce N. Cameron, J.D. Marejeo yote ya maandiko
yametoka kwenye tafsiri ya New International Version (NIV), copr. 1973, 1978,
1984 International Bible Society, isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo. Nukuu
kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya NIV inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji wa
Biblia wa Zondervan. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi
(kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sehemu
nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Kama huwa una kawaida ya
kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na hukulipata kwa juma moja, unaweza
kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na
http://www.GoBible.org
kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa,
Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.
Utangulizi: Je, uko vizuri kiasi gani unaposhughulika na
masuala ya tamaduni mbalimbali? Mimi siko vizuri sana kwa sababu sijafanyia
sana mazoezi suala hilo. Nilipoanza kusoma shule ya sheria, takribani theluthi
moja ya wanafunzi wenzangu walikuwa Wayahudi. Nilidhani kwamba Wayahudi ndio
wahusika wakuu kwenye Biblia. Ilinishangaza kuwa nao katika darasa moja huku
tukishindania kupata alama nzuri! Wakati nilipokuwa ninasafiri kwenda Canada.
Mcanada anayezungumza Kifaransa alitaka kufahamu kwa nini sizungumzi Kifaransa.
Kifaransa? Nilimjibu kwamba ninaishi Marekani na kwamba lugha mbadala
ninayoweza kuifahamu ni Kihispania. Nina mashaka kama nilifanya urafiki na mtu yule.
Je, tunashughulikaje na tofauti za tamaduni mbalimbali katika kupeleka injili? Hebu
tuzame kwenye somo letu la Biblia ili tuone kile tunachoweza kujifunza!
I.
Msamaria
A.
Soma Yohana 4:3-4. Endapo una GPS, kwa ujumla huwa
inakupatia uchaguzi kati ya njia fupi kabisa na njia nyinginezo unazoweza
kuzipendelea. Hii inaonekana kama Yesu alilazimika kupitia Samaria. Kuna tatizo
gani na kitendo hicho? (Wayahudi na Wasamaria hawakuwa wakipendana. Tatizo kubwa
lilikuwa ni, kama asemavyo Mathhew Henry katika maoni yake, kwamba “Wasamaria
walikuwa ni Wayahudi chotara kidini na kinasaba.” Kwa dhahiri mtazamo wa aina
hiyo sio msingi wa urafiki thabiti.)
B.
Soma Yohana 4:5-8. Jiweke kwenye nafasi ya Yesu. Unajisikiaje?
(Alikuwa amechoka, ana njaa na kiu.)
C.
Soma Yohana 4:9. Nchini Marekani tuna neno la “usahihi
wa kisiasa.” Inamaanisha kwamba unatakiwa kutambua mazingira yanayokuzunguka
ili usiseme neno lolote litakalomuudhi mtu. Je, huyu mwanamke anamwambia Yesu
kwamba hayuko sahihi kisiasa? (Ndiyo. Kimsingi anasema, “Unafahamu tatizo
lililopo kati ya Wayahudi na watu wa Mataifa, hutakiwi kuniomba nikusaidie
endapo ungekuwa unafuata mpangilio wa tabia inayokubalika.)
D.
Soma Yohana 4:10. Je, jibu hili liko sahihi kiasiasa? Unadhani mwanamke
huyu alifikiri Yesu anazungumzia jambo gani? (Utakumbuka kwamba Wasamaria
walikuwa wanachukuliwa kwamba ni watu wa hadhi ya chini kidini na
kimbari/kijamii. Sasa Yesu anasema kuwa mwanamke huyu hamfahamu Mungu na
hafahamu umuhimu wa Yesu. Mambo haya mawili yanaweza kuongeza msuguano kwa
sababu yanaendana na dhana iliyopo ambayo Wayahudi walikuwa nayo dhidi ya
Wasamaria.)
E.
Soma Yohana 4:11-12. Mwanamke Msamaria anajibuje? Je,
naye anavurumisha kwa kujibu matusi, je, anatia changamoto mantiki ya Yesu, au
anakubaliana kwamba Wasamaria ni watu wa hadhi ya chini? (Jibu lake kwa kiwango
kikubwa limelenga mantiki ya Yesu. Anabainisha kwamba Yesu hayupo kwenye nafasi
ya kutoa maji kwa sababu hawezi kuyafikia maji ya kisima. Anamwita Yakobo “baba
yetu” hivyo anabainisha kuwa mbari/jamii yake ni ya muhimu kama ya Yesu.)
F.
Soma Yohana 4:13-14. Jiweke kwenye nafasi ya mwanamke
Msamaria. Jambo gani linaendelea akilini mwako? Majibu yako ni yapi katika
kumjibu Yesu? (Jambo la kwanza ni kuhitimisha kwamba yeye (Yesu) ni kichaa. Jambo
la pili ni kuamini kwamba Yesu ni mtu wa pekee.)
G.
Soma Yohana 4:15. Mwanamke amechagua nini? (Kwa hakika
kabisa hakufanya uchaguzi wa kwamba Yesu ni kichaa. Lakini, jibu lake linaweza
kuwa ni jaribu kwa kile anachokitoa Yesu, au linaashiria kwamba anamwamini
Yesu. Inawezekana hamwelewi Yesu, lakini amevuka msitari na kuamini kwamba Yesu
ni mtu wa pekee.)
H.
Soma Yohana 4:16-19. Jambo gani limetokea hapa? (Sasa
ameelewa kikamilifu. Yesu alipomwambia hali ya familia yake, kitendo hicho
kilimthibitishia kwamba Yesu alikuwa mtu wa pekee, nabii.)
I.
Soma Yohana 4:20. Je, anaomba ushauri wa kiroho?
(Nadhani. Yumkini hii ndio mara ya kwanza anakutana na nabii. Anauliza kuwa
nani yuko sahihi – watu wake au Wayahudi kuhusu mahali sahihi pa kuabudia?)
J.
Soma Yohana 4:21-24. Je, jibu hili ni sahihi kisiasa? Je,
Yesu anamtukana? (Mwanamke anauliza “Nani yuko sahihi kuhusu mahali pa
kuabudia?” Yesu anajibu, “Si Wayahudi wala Wasamaria walio sahihi linapokuja
suala la mtazamo mpana wa mambo. Hata hivyo, wokovu unatoka kwa Wayahudi.”)
1.
Tunajifunza nini kutoka kwa Yesu katika kupeleka injili
kwa watu wenye uhasama? (Yesu haachi kusema ukweli. Hata hivyo, hafanyi jaribio
la kumuudhi/kumtukana yule mwanamke.)
K.
Soma Yohana 4:25-26. Mwanamke Msamaria anasema kuwa
anaelewa mtazamo mpana wa kuabudu. Yesu anadondosha bomu gani jipya? (Yeye ni
Masihi! Sasa mwanamke huyu anakabiliana na kiunzi kingine cha imani.)
L.
Soma Yohana 4:27-30. Je, mwanamke amemkiri Yesu kama
Masihi? (Anadhani kwamba kuna uwezekao huo. Fikiria kwamba ulikuwa unazungumza
na Masihi!)
M.
Soma Yohana 4:39-42. Fikiria mazungumzo ya Yesu na
mwanamke Msamaria. Yesu anabadilishaje uhasama unaotokana na tamaduni
mbalimbali hadi kuamini kwamba yeye ni Masihi?
II.
Akida
A.
Soma Mathayo 8:5-6. Masuala gani ya tamaduni mbalimbali
yanapatikana hapa? (Akida ni Mrumi, na Warumi walitawala taifa la Kiyahudi.)
B.
Soma Mathayo 8:7-9. Akida anatufundisha nini kuhusu
kuunganisha tofauti za kitamaduni? (Anapingana na madai yoyote ya hadhi za
kitamaduni. Anakiri kwamba Yesu ndiye mamlaka ya kweli.)
C.
Soma Mathayo 8:10-12. Yesu anasema nini kuhusu hadhi ya
juu ya utamaduni wake? (Anasema kuwa imani ndilo jambo la msingi, sio
utamaduni.)
D.
Soma Mathayo 8:13. Angalia jinsi imani ilivyobadili mpango
wa Yesu. Je, imani yetu itabadili mpango wa Mungu kwa ajili yetu? (Yesu
alipanga “kwenda na kuponya” (Mathayo 8:7), badala yake alisema tu na mtumishi
akapona.)
III.
Mwanamke
A.
Soma Mathayo 15:21-23. Jiweke katika tukio hili. Je,
mwanamke huyu anayafanya maisha yasiwe ya furaha kwa Yesu na wanafunzi? (Kwa hakika,
anaendelea kuwafuata na kupiga kelele.)
1.
Kwa nini Yesu hamjibu? Je, mara kadhaa inaonekana
kwamba Yesu hakujibu?
B.
Soma Mathayo 15:24. Je, hii ni kweli? (Muda mfupi tu uliopita
tumesoma visa vya mwanamke Msamaria na akida wa Kirumi.)
1.
Ikiwa si kweli, kwa nini Yesu anasema hivyo?
C.
Soma Mathayo 15:25-26. Jiweke kwenye nafasi ya
mwanamke. Je, ungemfanya nini Yesu kwa kitendo cha kumwita binti yako “mbwa”
kwa sababu ya rangi/mbari/jamii yake?
1.
Tunafundishwa nini kuhusu uhusiano wa tamaduni
mbalimbali?
D.
Soma Mathayo 15:27-28. Kipi kilicho cha muhimu zaidi
kuliko utamaduni na mbari? (Imani!)
1.
Je, unapaswa kutumia njia ile ile kama aliyoitumia Yesu
kwa huyu mwanamke? (Yesu alikuwa anaijaribu imani yake. Sidhani kama tunapewa
wito wa kuijaribu imani kwa kuwatukana watu.)
2.
Nchini Marekani tunao watu wanaopenda kuzungumzia
kuhusu “kuudhiwa,” kana kwamba wana haki ya kuwazuia watu wengine kusema au
kutenda jambo lolote wanalolichukulia kuwa ni la “kuchukiza.” Mwanamke huyu
anatufundisha nini katika mada ya kuchukizwa? (Tunatakiwa kujikita kwenye jambo
la msingi, kuwaokoa watoto wetu na kuishika imani.)
IV.
Wakoma
A.
Soma Luka 17:11-13. Tutajifunza baadaye kwamba mmoja
kati ya wale kumi ni Msamaria. Kwa nini Wayahudi tisa wanajihusisha na
Msamaria? (Soma Mambo ya Walawi 13:45-46. Kwa sababu wana kitu kibaya sana –
wana ukoma na hakuna anayetaka kukaa nao.)
B.
Soma Luka 17:14. Waliponywaje? (Walimwamini Yesu, wakaelekea
kwa makuhani kuonesha kibali kuwa hawakuwa na ukoma tena, na walipokuwa
wakienda waliponywa. Walitekeleza maneno ya Yesu.)
C.
Soma Luka 17:15-16. Je, ungerudi na kumshukuru Mungu,
au ungekuwa unawaambia marafiki zako na wanafamilia kwamba sasa unaweza kuishi
pamoja nao na kuwa sehemu ya watu wa kawaida katika jamii?
D.
Soma Luka 17:17-19. Utagundua kwamba Yesu anamwita “mgeni.”
Je, tunapaswa kuwa vipofu katika tofauti za kimbari na kitamaduni? (Yesu
alifadhaishwa kwamba hakuna Myahudi hata mmoja aliyerejea kumshukuru. Alibaini suala
la kimbari/kijamii.)
1.
Je, huwa unakumbuka kumshukuru Mungu kwa kile
anachokutendea?
2.
Unadhani maneno ya Yesu “imani yako imekuokoa”
yanamaanisha nini? (Nadhani Yesu anamaanisha kwamba roho yake, na sio mwili
wake tu vimeponywa.)
E.
Rafiki, imani ni ya muhimu zaidi kuliko utamaduni au
mbari. Je, utadhamiria kuipa kipaumbele imani yako unaposhughulika na watu
wengine?
V. Juma lijalo: Petro na Watu wa Mataifa.
No comments:
Post a Comment