Sehemu ya Pili: Wakati wa Agano jipya iii/ Wakati wa Kanisa Baada ya Mitume (Post Apostolic Church)
Katika
somo lililopita nimeonyesha kwa kadri ya Maandiko kwamba, haupo
ushahidi wa Kibilia kuwa Mitume waliabudu katika siku iliyokuwa tofauti
na Sabato kama ilivyoagizwa na Bwana katika Amri zake. Tuliona kuwa
tokea wakati wa Yesu hadi wakati wa Mitume, hakukuwa na siku iliyokuwa
imeanzishwa rasmi kama siku ya ibada na Wakristo, Tofauti na Sabato kama
ilivyotuzwa na wayahudi. Kwakuwa hakuna maelekezo ndani ya Biblia juu
ya Badiriko hilo la siku ya kuabudu, kuanzia sasa na katika masomo
yanayofuata tutaigeukia Historia ya Ukristo ili kuona badiriko hili
lilianzaje na nini kilisababisha. Kabla ya kuangalia badiriko hili la
siku ya kuabudu, katika sehemu hii nitajaribu kwa ufupi kuonyesha kuwa
historia inaonyesha kwamba wafuasi wa Mitume wa Yesu nao walipokea
utaratibu huo huo wa siku ya kuabudu kama walivyorithi mafundisho ya
Yesu na Mitume. Hapa nitawanukuru wanahistoria mashuhuri wa karne ya nne
na ya Tano
SOCRATES CHOLASTICUS NA SOZOMEN (Karne ya Tano)
“Ingawa
makanisa YOTE ULIMWENGUNI yanasherehekea fumbo takatifu (Meza ya Bwana)
siku ya Sabato (Jumamosi) ya kila wiki, hata hivyo Wakristo wa
Alexandria na Rumi, kwa kufuatia tamaduni za kizamani, wamekoma kufanya
hivi. Wamisiri katika ujirani wa Alexandria na wakazi wa Thebais,
wanafanya makusanyiko yao ya kidini siku ya Sabato, lakini hawashiriki
fumbo kwa jinsi ilivyo kawaida miongoni mwa Wakristo kwa ujumla. Kwa
kuwa wao baada ya kula na kujishibisha wao wenyewe kwa chakula cha kila
namna siku ya jioni na kutoa sadaka zao, kisha ndipo hushiriki fumbo”
Socrates Scholasticus Ecclesiastical history 5 Uk 22
“Watu
wa Costantinopole, na karibia kila mahali hukusanyika pamoja siku ya
Sabato, na pia katika siku ya kwanza ya juma.,utamaduni ambao haufuatwi
katika kanisa la Rumi au Alexandria. Kuna miji mingi na vijiji katika
nchi ya Misri ambapo tofauti na utaratibu wa kila mahali, watu hukutana
pamoja siku ya sabato jioni, na pamoja na kwamba wamekwisha kula kabla,
hushiriki fumbo” Sozomen Ecclesiastical history 7 Uk 19
Hivyo
mpendwa utagundua kwamba hadi kufikia karne ya 5 bado Wakristo walikuwa
wakiabudu katika siku ya Sabato, Ingawa kama tutakavyoona katika somo
lijalo, tayari kulikuwa kumeshaanza utaratibu wa kuabudu siku ya kwanza
ya juma polepole. Hapa utagundua inatajwa Kanisa la Rumi liliacha
utaratibu wa Sabato ili kufuata taratibu za utamaduni wa zamani
(Upagani)—tutajifunza zaidi.
ORIGEN WA ALEXANDRIA
“Tuachane
na Utunzaji wa Sabato wa Kiyahudi, hebu tuangalie jinsi ulivyo utunzaji
sahihi wa Sabato unaotarajiwa kufanywa na Mkristo. Siku ya Sabato,
kusifanyike kazi yoyote ya kidunia, iachwe huru kwa kazi za Kiroho tuu.
Njoo Kanisani, Sikiliza masomo na mijadara mitakatifu, na ufikirie mambo
matakatifu. Fikiria maisha yajayo, hukumu ijayo. Yapuuzie mambo ya sasa
yanayoonekana kwa kutamani mambo yajayo yasiyoonekana. Huu ndio
utunzaji sahihi wa Sabato ya Kikristo.” Origen. Homily 23
Maelezo
haya yanatupatia mwanga kwamba, hata kama miji hii miwili ilikuwa
imeshaanza kuacha utunzaji wa Sabato kufikia Karne ya 5, siyo miji yote
katika nchi ya Misri iliyokuwa imeacha kabisa Sabato kama ilivyo katika
maandiko.
APOSTORIC CONSTITUTION (Karne ya Nne)
“Mwogope
Mungu machoni pako, na siku zote kumbuka amri kumi za Mungu…Itunze
Sabato, kwa kumheshimu yule aliyeacha kazi yake ya uumbaji, lakini
hakuacha kazi yake ya uangalizi. Ni pumziko kwa ajili ya kutafakari
Sheria ya Bwana…” Apostolic constitution 2 uk 36
Kunaushahidi
mwingi juu ya utuzaji wa Sabato kama siku ya ibada kwa wakristo wa
mwanzo. Hatuwezi kuleta mashahidi wote hapa, yatosha nukuru hizi
kuonyesha kwamba, kanisa la awali walizingatia na kutunza Sabato kama
ambavyo Biblia inaagiza. Hatuwezi kukana ukweli huu kwa matamanio tuu na
kulinda imani zetu. Haitasaidia au kubadirisha ukweli eti kwa kuwa
tumeshikilia misimamo yetu.
Katika
mada zilizopita tumeonyesha kuwa Mungu ndiye aliyeanza kustarehe katika
siku ya sabato kama kielelezo kwa Adam na Eva. Inafurahisha kuona kuwa
Andam na Eva waliumbwa katika siku ya 5 na siku yao ya kwanza duniani
hapa ilikuwa ni Sabato takatifu, wakiwa na Bwana wao walifurahia uumbaji
wa Mungu. Yapaswa na sisi tuitenge siku ya Sabato kama siku ya kuachana
na kazi zetu za kidunia, tumwabudu Mungu na kufurahia uumbaji wake.
Tumeona pia kuwa baada ya mwanadamu kusahau siku hii ya Sabato. Mungu
mwenyewe kwa kuwatumia Israel kama kielelezo alianza kuwafundisha siku
ya Sabato kuwa ni ya kupumuzika na kufanya ibada kwa Mungu. Kisha
tukaangalia kwamba, baadaye Mungu alitoa amri 10 katika kitabu cha
Kutoka 20:1-17, moja ya amri hiyo inasema “Ikumbuke siku ya sabato
uitakase….Maana kwa siku sita BWANA alifanya mbingu, na nchi, na bahari,
na vyote vilivyomo akastarehe siku ya saba; kwa hiyo BWANA akaibarikia
siku ya Sabato na kuitakasa” Kut. 4:8-11. Yesu pia alipokuja hapa
duniani, akatunza siku ya Sabato na maandiko yakasema alituachia
kielelezo 1Petro 2:21. Kwa kielelezo hicho, wanafunzi wake walidumu
kutunza sabato. Luka 23:55-56. Mdo 16:13 na mwisho tumeona katika somo
hili Miaka zaidi 300 baada ya Yesu kupaa mbinguni, Wafuasi wa Yesu
(Wakristo) walitunza Sabato na kuabudu katika siku hiyo kama siku ya
Ibada.
Ni
wito wangu kwako msomaji wangu kwamba, hautachagua kwenda kinyume na
Neno la Mungu na watakatifu wote katika zama za ukristo. Bila shaka wale
waliompenda Bwana, walimpenda kiasi cha kutii maangizo yake kama Yonana
anavyotuagiza “Kwa kuwa huu ndio upendo wa Mungu, kwamba tuzitii amri
Zake. Nazo amri Zake si nzito” 1Yohana 5:3
NA https://loudcrymediaministries.wordpress.com
No comments:
Post a Comment