Sehemu ya Pili:ii/ Wakati wa Mitume.
Katika
Luka 6:13 tunasoma “Kulipopambazuka akawaita wanafunzi Wake, naye
akachagua kumi na wawili, ambao pia aliwaita mitume:” Mitume hawa
walichaguliwa miongoni mwa Wayahudi. Watu ambao waliifahamu fika Torati
ya Bwana. Hivyo hatutegemei kwamba, kuhusiana na swala la Ibada
wangefanya kinyume na neno la Mungu.
Wanafunzi
hawa walikuwepo siku ile Yesu akihubiri hubiri lile refu mlimani.
Walimsikia vyema akianza kwa kusema “Heri walio masikini wa roho, maana
ufalme wa mbinguni ni wao” Mathayo 5:3. Bila shaka maneno haya
yaliwavuta sana kiasi cha kuwa watulivu na kusikiliza akiendelea na
maneno mengine. Na ndipo mara wakamsikia akisema “Msidhani kwamba
nimekuja kuondoa Torati au Manabii, sikuja kuondoa bali kutimiza. 18Kwa
maana,amin, nawaambia, mpaka mbingu na dunia zitakapopita, hakuna hata
herufi moja ndogo wala nukta itakayopotea kwa namna yo yote kutoka
kwenye Torati mpaka kila kitu kiwe kimetimia. 19Kwa
hiyo, ye yote atakayevunja mojawapo ya amri ndogo kuliko zote ya amri
hizi, naye akawafundisha wengine kufanya hivyo, ataitwa mdogo kabisa
katika Ufalme wa Mbinguni, lakini ye yote azitendaye na kuzifundisha
hizi amri ataitwa mkuu katika Ufalme ya Mbinguni.” (Biblia Kiswahili
Toleo la 2006, www.biblica.com.en-us/bible-versions/kiwahili-swahili bible )
Ni
jambo la kuvutia kuona kuwa Yesu hapa yuko wazi kabisa kiasi cha
kutofanya makosa ya kutokumwelewa. Anasema huduma yake siyo kubadirisha
Sheria ya Mungu, bali kuendenda kufuatana na Sheria hiyo. Ndiyo maana
tukaona katika somo lililopita Yesu akitimiza torati yote. Siyo hivyo tu.Yesu pia
anasema “au manabii”. Neno hili “Torani au manabii” lapaswa lieleweke
kwamba, wakati wa Yesu Biblia ya wakati huo iligawanyika katika sehemu
Mbili yaani Torati—ikiwa na maana ya vitabu vile 5 vya Sheria ya Musa,
na Manabii—hii ikiwa na maana ya Maandiko yote ya manabii wengine.
Wakati mwingine iliweza kutamukwa, Torati, Manabii na Zaburi. Hivyo Yesu
anakazia kwamba kuja kwake hapa siyo kutangua maandiko matakatifu yote.
Mwisho anakazia kwa kusema “ye yote atakayevunja mojawapo ya amri ndogo
kuliko zote ya amri hizi, naye akawafundisha wengine kufanya hivyo,
ataitwa mdogo kabisa katika Ufalme wa Mbinguni”
Mambo
haya yako wazi kabisa, Yesu anakataza wafuasi wake kuvunja amri za
Mungu. Hivyo basi tunaweza kuona kwamba, wanafunzi wake walimwelewa
vizuri sana na kamwe katika mafundisho yao hatuoni popote wakipuuzia
amri za Mungu. Wao wenyewe kwa kuwa walimwelewa Bwana wao waliendelea
kusisitiza fundisho hili kwa kusema “Kwa kuwa huu ndio upendo wa Mungu,
kwamba tuzitii amri Zake. Nazo amri Zake si nzito” 1Yohana 5:3. “Hivyo
basi, sheria yenyewe ni takatifu na amri ni takatifu na ya haki, tena ni
njema.” Warumi 6:12
Tukiwa
na uelewa huo wa wanafunzi wa Yesu juu ya amri za Mungu. Hebu tuangalie
mwendendo wao juu ya Sabato. Je kuna ushahidi wowote kwamba waliwahi
kukiuka maagizo ya Sabato kama siku ya Ibada?
Siku
ile aliyokufa Yesu, tunaambiwa kwamba “Ilikuwa siku ya Maandalio, nayo
Sabato ilikuwa karibu kuanza.” Luka 23:54. Biblia hapa kwa inarecodi kwa
usahihi kwamba, mpaka wakati wa kifo cha Yesu Bado sabato ilikuwa
ikitunzwa kama siku ya Kupumzika. Fungu linaloendelea linasomeka kwamba
“Wale wanawake waliokuwa wamekuja pamoja na Yesu wakimfuata kutoka
Galilaya,wakamfuata Yosefu, wakaliona kaburi na jinsi mwili wa Yesu
ulivyolazwa. 56Kisha
wakarudi nyumbani, wakaandaa manukato na marhamu ya kuupaka huo mwili.
Lakini wakapumzika siku ya Sabato kama ilivyoamriwa.” Luka 23:55-56
(Biblia Kiswahili Toleo la 2006, www.biblica.com.en-us/bible-versions/kiwahili-swahili bible )
Ikiwa
wakati wa uhai wa Yesu kunamafundisho aliyoyatoa kuhusu badiriko la
Sabato, basi tunategemea fundisho hilo lingekuwa limeeleweka sana kwa
wanafunzi wa Yesu. Kwao kama ilivyo siku hizi kwa wale wanaodai kuwa
wafuasi wa Yesu, siku ya sabato kesho yake wangekwenda kaburini kuupaka
mafuta mwili wa Yesu. Lakini Sabato ilikuwa na ya umuhimu mkubwa hata
kwa wanafunzi wake kiasi kwamba wasingeweza kwenda kaburini siku hiyo.
Licha ya kuwa ni Bwana wao aliyelala kaburini.
Kwanini
itendeke hivyo kwa wanafunzi wake? Bila shaka ni kwa sababu, kama
tulivyoona katika somo lililopita, Yesu alikuwa na kawaida ya kuabudu na
kutunza siku ya sabato kuwa takatifu, bwana wao alikuwa amekwisha
kuwaeleza kuwa “Mbingu na nchi zitaondoka. Lakini hakuna hata nukta moja
ya sheria ya Mungu itakayoondoshwa” na sasa mbingu zikingali zipo,
walielewa kuwa Sheria ya Bwana ingali ikisimama.
Baada
ya Yesu kufufuka, alipaa mbinguni. Habari za matendo ya wanafunzi
zimerekodiwa vizuri katika kitabu cha Matendo ya Mitume. Hapa tunaweza
kuona mwenendo wa mitume na wale mataifa waliokuwa wakiongolewa kwa
injili kama ilivyohubiriwa na mitume. Tuangalie Desturi ya Ibada zao,
zilifanyika katika siku ipi”
“Hata
siku ya sabato, tukatoka nje ya lango, tukaenda kando ya mto, ambapo
tukadhani ya kuwa, pana mahali pa kusali, tukaketi, tukasema na wanawake
waliokutana pale” Matendo 16:13. Hapa kwa uwazi kabisa siku ya sabato
inahusishwa na tendo la ibada, hii yaonyesha kwamba. Siku ya sabato
ilikuwa siku ya kumwabudu Mungu, hata wakati wa Mitume
“Paulo na Barnaba walipokuwa wakitoka nje ya sinagogi, watu wakamwomba wazungumze tena mambo hayo Sabato nyingine inayofuata. 43Baada
ya kusanyiko la Sinagogi kutawanyika, wengi wa Wayahudi na waongofu wa
dini ya Kiyahudi wakawafuata Paulo na Barnaba, nao wakazungumza na
kuwahimiza wadumu katika neema ya Mungu. 44Sabato
iliyofuata karibu watu wote wa mji ule walikuja kusikiliza neno la
Mungu” Matendo 14:42-44 (Biblia Kiswahili Toleo la 2006, www.biblica.com.en-us/bible-versions/kiwahili-swahili bible )
“Kila Sabato Paulo alikuwa akihojiana nao akijitahidi kuwavuta Wayahudi na Wayunani.” Matendo 18:4
Hapa
inaonekana Paulo alikuwa akifanya mafundisho mengi katika siku ya Ibada
Siku ya Sabato. Na tena wasikilizaji wake siyo Wayahudi tuu, bali hata
Wayunani ambao ni watu wa Mataifa.
Hivyo
tunaweza kuhitimisha kwamba Kitabu cha Matendo ya mitume ambalo ndilo
kanisa la awali kabisa baada ya Yesu kupaa mbinguni, kuna ushahidi wa
kutosha kwamba, Mitume hawakubadirisha siku ya Ibada kama ilivyoagizwa
katika sheria ya Bwani. Hii ilikuwa ni kutokana na onyo alilokuwa
amelitoa Yesu Mapema wakati wa kuanza kwa huduma yake.
“19Kwa
hiyo, ye yote atakayevunja mojawapo ya amri ndogo kuliko zote ya amri
hizi, naye akawafundisha wengine kufanya hivyo, ataitwa mdogo kabisa
katika Ufalme wa Mbinguni, lakini ye yote azitendaye na kuzifundisha
hizi amri ataitwa mkuu katika Ufalme ya Mbinguni.” Mathayo 5:19.
Mimi
ninapenda kuitwa mkuu katika ufalme wa Mbinguni, bila shaka na wewe
msomaji wangu. Ikiwa ni hivyo Tuombe Roho mtakatifu atusaidie kutovunja
amri za Mungu ikiwemo na Amri ya Utunzaji wa Sabato, na tuwafundishe
wengine kutenda hivyo
NA https://loudcrymediaministries.wordpress.com
No comments:
Post a Comment