NEWS | MWANZA:KITABU CHA AFYA NA UZIMA KINACHOSOMWA KWA SASA MAKANISA YOTE YA WAADVENTISTA WASABATO DUNIANI CHAZINDULIWA HAPO JANA KATIKA KANISA LA KIRUMBA SDA NA KIONGOZI WA WA UCHAPAJI WA SOUTH NYANZA KONFERENSI

Mkurugenzi wa uchapaji wa South Nyanza Conference, Pr Beatus Mlozi azindua kitabu kiitwacho "AFYA NA UZIMA" ambacho ni kitabu cha kimishonari cha mwaka, kanisani Kirumba sabato ya leo Julai 4, 2015.
MAPITIO YA KITABU
Afya na Uzima, Siri Zitakazobadilisha Maisha Yako
Katika Dunia ya sasa, Afya Bora ni tunu muhimu kuliko Utajiri na vyeo vya kisiasa.
Utajiri hauna faida kubwa, kama watu wanaomiliki utajiri watakuwa na Afya mbaya.
Kila mwaka, Soko la Dawa Duniani linakua kwa kiwango kikubwa, kwa sababu mitindo ya maisha ya watu wengi inakaribisha maradhi makubwa ama matatizo makubwa ya kiafya.
Mwaka huu 2015,Soko la Huduma za Afya linakisiwa kufikia Dola za Marekani trilioni tatu,ambazo zinaifanya Baishara ya Huduma za Afya kuwa moja ya sekta kubwa kabisa ya Uchumi Duniani.
Katika nchi zinazoendelea,hususan Tanzania,huduma za Afya hutumia zaidi ya asilimia 10 ya Pato zima la Ndani,kurejesha Afya za watu katika hali bora;lakini pasipo mafanikio.
Afya mbaya inawatisha watu wote,masikini na matajiri; na afya mbaya inaogopwa kuliko ugaidi na umasikini wa kutisha!
Kwa ujumla kitabu hiki,AFYA NA UZIMA,na siri zinazobadilisha Maisha,kilichoandikwa na waandishi wawili, Mark A.Finley na Peter N. Landless,kinawapa watu suluhu ya matatizo ya kiafya yanayoisumbua Dunia leo,wakati ambapo hata umri wa kuishi umeporomoka kiasi cha kutisha.
Mtu huitwa mzee leo katika umri wa miaka 45 tu! Kwanini mzee asiwe na umri kati ya miaka 113 na 122?
Sababu kubwa ya kushuka kwa wastani wa maisha ya watu kula vibaya na kubadili mtindo wa Maisha.
Kitabu hiki, AFYA NA UZIMA, kina siri zitakazobadilisha Maisha yako. Kitafute ukisome sasa.
Unaweza kupata nakala ya Kitabu hiki Makao Makuu ya Conference, au Duka lolote la vitabu hapa Tanzania.
Kitabu cha Afya na Uzima 
Mchungaji Mlozi mwenye suti nyeusi akiwa na waumini wa kanisa la kirumba sda katika kusisitiza umuhimu wa afya kwa njia ya kutambulisha kitabu hiki cha Afya na Uzima kwa kukiinua juu.

No comments:

Post a Comment