AMRI KUMI ZA MUNGU - UPENDO
Kutoka 20:3-17
Mpende Bwana Mungu wako, Kwa moyo wako wote, na Kwa Roho yako yote, na akili zako zote. Mathayo 22:37
[Upendo kati ya Mwanadamu na Mungu]
1
Usiwe na Miungu mingine ila mimi
2
Usijifanyie
sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu chochote kilicho juu mbinguni,
wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia.
Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, Bwana, Mungu wako, ni
Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha
tatu na cha nne cha wanichukiao, name nwarehemu maelfu elfu wanipendao,
na kuzishika Amri zangu
3
Usilitaje bure jina la BWANA, Mungu wako, maana Bwana hatamhesabia kuwa hana hatia mtu alitajaye jina lake bure
4
Ikumbuke
siku ya sabato uitakase. Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote,
lakini siku ya saba ni sabato ya BWANA, Mungu wako, siku hiyo usifanye
kazi yo yote, wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako,
wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya
malango yako. Maana, kwa siku sita Bwana alifanya mbingu, na nchi, na
bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya Saba; kwa hiyo BWANA
akaibarikia siku ya sabato akaitakasa.
|
Mpende Jirani yako kama nafsi yako.
Mathayo 22:39
[Upendo kati ya Mwanadamu na Mwenzie]
5
Waheshimu baba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na BWANA, Mungu wako.
6
Usiue
7
Usizini
8
Usiibe
9
Usimshuhudie jirani yako uongo
10
Usitamani
nyumba ya jirani yako, usitamani mke wa jirani yako, wala mtumwa wake,
wala mjakazi wake, wala ng’ombe wake, wala punda wake, wala chochote
alicho nacho jirani yako.
|
Na Mwinjilist: Eliezer Y. Mwangosi
Email: eliezer.mwangosi@yahoo.com
Mobile Phone: 0767 210 299
No comments:
Post a Comment