(Luka 12 & 19)
Somo hili limetafsiriwa
kutoka katika Copr. 2011, Bruce N. Cameron, J.D. Marejeo yote ya maandiko
yametoka kwenye tafsiri ya New International Version (NIV), copr. 1973, 1978,
1984 International Bible Society, isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo. Nukuu
kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya NIV inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji wa
Biblia wa Zondervan. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi
(kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sehemu
nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Kama huwa una kawaida ya
kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na hukulipata kwa juma moja, unaweza
kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na
http://www.GoBible.org
kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa,
Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.
Utangulizi: Je, unapenda watu wakuzungumzie vizuri kwa
kiwango kikubwa? Mimi ninapenda sana. Ninapokuwa nimefanya makosa, jambo
ninalolifikiria sana huwa ni kuhusu hadhi yangu. Katika miaka yangu mingi ya
kujifunza Biblia, nimejifunza kwamba ninapaswa kujihusisha sana na jinsi Mungu
anavyonichukulia. Sehemu ya kujihusisha na kile watu wengine wanachokifikiria
ni vizuri, endapo lengo ni kuwashawishi watu wengine wamwendee Mungu. Lakini,
juma hili nilikuwa na mazungumzo na mtu mwenye kumcha Mungu sana aliyeniambia
kwamba alikuwa mbaya kuliko nilivyokuwa nikimchukulia. Ninahisi nawe pia
utasema vivyo hivyo – kwamba wewe ni mbaya kuliko jinsi hadhi yako ilivyo. Je,
jambo hilo linasema nini kuhusu jinsi Mungu anavyokuchukulia? Hebu tuchimbue
kile Biblia inachokifundisha kuhusu jambo hili!
I.
Msiogope
A.
Soma Luka 12:4-5. Ni nani huyu awezaye kututupa jehanum?
(Nadhani Yesu anamzungumzia Mungu.)
1.
Nani awezaye “kuua mwili” pekee? (Wanadamu wengine.)
2.
Yesu anamaanisha nini? (Tunapaswa kumwogopa Mungu zaidi
kuliko tunavyoweza kuwaogopa wanadamu.)
B.
Soma Luka 12:6-7. Je, Mungu anakufahamu? (Ndiyo! Mungu
hamsahau hata shomoro. Anafahamu idadi ya nywele kichwani mwangu!)
1.
Kwa nini Yesu anatuambia tumwogope Mungu awezaye kututupa
katika jehanum, na kisha anatuambia “msiogope?” (Yesu anajenga hoja dhidi ya
woga. Anasema kwamba endapo tutamwogopa mtu yeyote, basi anapaswa kuwa ni
Mungu. Lakini, Mungu anatupenda na kutujali.)
C.
Hebu turejee nyuma na tuanzie kusoma Luka 12:1-3. Nani anayefahamu
kile tulichokisema gizani na katika vyumba vya ndani? (Mungu!)
1.
Kwa nini unafiki ni upumbavu mkubwa? Jambo hili
linahusikaje na suala la kuwaogopa wanadamu? (Unafiki ni kusema jambo moja
hadharani na kutenda jambo jingine faraghani. Yesu anasema kwamba huu ni
upumbavu kwa sababu Mungu anayafahamu maisha yetu. Kwa nini tuwafiche wanadamu –
ambao hawawezi kututupa jehanum, lakini tunaridhika Mungu anapofahamu?)
2.
Jibu moja ni kwamba tunajisikia vizuri wanadamu wengine
wanapofikiri kwamba sisi ni bora kuliko jinsi ambavyo tupo kiuhalisia. Yesu anazungumzia
nini kuhusu kitendo hicho? (Mambo mabaya yatabainika.)
D.
Soma Luka 12:8-9. Hebu tupitie tena swali la mwisho. Ikiwa
inaonekana vyema kuwaonesha wanadamu wengine wakufikirie vile usivyo, je,
tunasema kuwa nani ni wa muhimu zaidi: Mungu, watu wengine au sisi? (Watu
wengine na sisi.)
1.
Ikiwa ninadhani kwamba mimi ni wa muhimu zaidi, na
mawazo ya watu kuwa ya muhimu zaidi kuliko mawazo ya Mungu, hii inahusianaje na
kauli ya Yesu kwamba tunapaswa kumkiri Mungu mbele za wanadamu? (Nadhani
anachokimaanisha Yesu ni kwamba vipaumbele vyetu vimepitwa na wakati.)
E.
Soma Luka 12:9-10. Je, unakumbuka nyakati za nyuma
ambapo hukumzungumzia Mungu kwa sababu hukutaka kufedheheka? Je, huko ni “kumkana
Mungu?”
II.
Uoga Sahihi
A.
Angalia tena Luka 12:10. Je, unaweza kuona mwelekeo wa
hoja ya Yesu? Unafiki ni kupendelea mawazo ya wanadamu dhini ya mawazo ya
Mungu. Kumkana Mungu (au kushindwa kumkiri) ni kuyaweka mawazo ya wanadamu
mbele ya Mungu. Mawazo haya yanaonesha tunawaogopa wanadamu zaidi ya vile
tunavyomwogopa Mungu. Yesu anafundisha kwamba mtazamo huu hauna mantiki. Je,
Luka 12:10 ni onyo au faraja? (Ikiwa unaona, kama nionavyo mimi, kwamba maoni
ya Yesu yanazungumzia dhambi zetu, habari njema ni kwamba Yesu anasema kuwa
dhambi hizi zinaweza kusamehewa.)
1.
Je, kuna onyo lolote? (Kufuru dhidi ya Roho Mtakatifu
haitasamehewa!)
B.
Soma Mathayo 12:30-32 na Marko 3:28-30. Unadhani inamaanisha
nini kumkufuru Roho Mtakatifu? (Nadhani Yesu anasema kwamba mitazamo mingine
haina maana. Katika kitabu cha Luka, tatizo ni kufikiri kwamba maoni ya watu
wengine ni ya muhimu zaidi kuliko mawazo ya Mungu. Katika kitabu cha Mathayo na
Marko tatizo ni kuiita kazi ya Roho Mtakatifu kuwa ni ya Shetani. Sidhani kama
Yesu anachora msitari kwenye mchanga na kusema “ukivuka msitari huu, kamwe
huwezi kusamehewa,” badala yake, anasema kuwa, “Ikiwa unafichaficha kila kitu,
huna matumaini ya kupata jibu sahihi.”)
III.
Ulafi/Uroho
A.
Soma Luka 12:13-15. Vipi kama ndugu yake anakiuka haki
za urithi za mtu huyu? (Yesu anasema kuwa huu si ujumbe mkuu – yupo hapa kuokoa
roho zetu sio mifuko yetu.)
1.
Je, hii ni mitazamo mingine ya maisha “iliyopinduliwa
juu chini?” Mtazamo wetu upo juu ya vitu na si kwa Mungu?
B.
Soma Luka 12:16-20. Je, kuna ubaya kuwa tajiri? Je,
tunapaswa kujiandaa na kustaafu kwetu? (Kumbukumbu la Torati 28 na mashujaa wa
Agano la Kale vinaashiria kwamba mtu kuwa tajiri kunaendana na kuishi maisha
sahihi. Hesabu 8:23-26 inaashiria kwamba Mungu anaamini katika kustaafu.)
C.
Soma Luka 12:20-21. Tatizo ni lipi? (Ikiwa tajiri huyu
atafariki usiku ule, atakuwa amepoteza kila kitu alichokifanyia kazi na
kukipangia.)
1.
Hii inahusianaje na unafiki na makufuru dhidhi ya Roho
Mtakatifu? (Nadhani huu ni mfano mwingine wa kupindua mambo mawazoni mwetu. Mtu
huyu anajali sana mustakabali wake kifedha kuliko mustakabali wake na Mungu. Ni
sahihi kujali kile watu wengine wanachokifikiri, ni sahihi kuwaogopa wanadamu,
ni sahihi kujiandaa kwa ajili ya uzee, lakini lazima tuwe na mtazamo sahihi:
Mtazamo wa Mungu ni wa muhimu zaidi. Kumwogopa/kumcha Mungu (ambaye anatupenda)
ni kipengele cha muhimu sana maishani. Hii inamaanisha kuwa urafiki wetu na
Mungu ni sehemu ya muhimu sana ya mpango wetu wa siku zijazo, si uhusiano wetu
na fedha.)
IV.
Ubepari/Ukabaila
A.
Soma Luka 19:11. Je, watu walikuwa sahihi kuhusu kile
ambacho kingetokea? (Yesu alikuwepo, lakini Ufalme wa Mungu haukuonekana mara
moja.)
B.
Soma Luka 19:12-14. Kwa nini Yesu anaongezea taarifa
hii kuhusu watawaliwa kumchukia mfalme mtarajiwa? Hii inahusianaje na matarajio
ya watu ya uongo kuhusu Ufalme wa Mungu? (Walitaka Yesu atetee uwezo wake,
awaangushe Warumi, na kuanzisha Ufalme wa Mungu.)
1.
Kitu chochote kinachohusiana na tafakari inayopinduliwa
juu chini kinaonekana kuzoeleka hapa? (Kwa mara nyingine, watu wanajikita
kwenye jambo lisilo sahihi.)
C.
Soma Luka 19:15-19. Je, Yesu ni bepari? Kwa nini
hakumwambia mtu aliyepewa mafungu kumi kwamba anapaswa kutoa mafungu 2.5 kwa
mtu aliyepewa mafungu matano ili kwamba wawe na kiasi sawa: mafungu 7.5?
D.
Soma Luka 19:20-23. Mtu mwenye fungu moja anatoa
malalamiko gani kumhusu mfalme? (Analalamika kwamba mfalme ni bepari na kwamba
anamwogopa.)
1.
Ikiwa huu ni mfano kumhusu Mungu, je, mtu huyu
anamwogopa Mungu? (Ndiyo, lakini aina hii ya hofu si sahihi.)
2.
Utagundua kwamba alihifadhi fungu lake vizuri kwenye
leso. Je, hii inaashiria nini?
E.
Soma Luka 19:24-25. Je, unakubaliana na wapinzani?
1.
Utaona kwamba mtu aliyefanikiwa anapewa fedha za mtu
mwenye fungu moja ambaye hakushughulika vyema na fedha zake. Unawezaje
kulinganisha jambo hilo na kisa cha tajiri (tulichojifunza hivi punde)
aliyeamua kustaafu na kufurahia utajiri wake? (Tajiri anafurahia fedha zake
mwenyewe.)
F.
Soma Luka 19:26-27. Kisa ni hiki hapa! Mtu mvivu
anayechukia ubepari anatakiwa kutoa fedha zake na kumpa mtu tajiri sana. Maadui
wa mfalme wanaletwa na kuuawa. Hivyo sivyo ambavyo umezoea kumsikia Yesu
akisema, sawa?
1.
Je, “mina” ni nini? (Ni fedha kwa mujibu wa Luka 19:15.
Ni kiasi cha ujira wa miezi mitatu.)
2.
Je, unadhani kisa hiki kinahusu fedha?
3.
Unadhani mfalme na maadui ni akina nani kwenye huo
mfano? (Yesu anaonekana kuwa ndiye Mfalme na Wayahudi ni maadui zake. Walidhani
Yesu angewapindua Warumi, na kwa kuwa hakufanya hivyo, walikuwa maadui wa kile
alichokuwa anakifikiria akilini mwake. Utagundua kwamba Yerusalemu iliangamizwa
miongo kadhaa iliyofuatia.)
G.
Hebu tuone kama tunaweza kuyaunganisha mambo haya. Ikiwa
Yesu ni Mfalme, na wale waliomkataa ni maadui zake, je, kweli “minas” zinawakilisha
fedha? (Nadhani zinaweza kuwakilisha. Lakini, sidhani kama huo ndio ujumbe
mkuu. Zinawakilisha talanta zinazotumika kuuendeleza Ufalme wa Mungu.)
H.
Rafiki, unaweza kuona jinsi visa tofauti tofauti kwenye
somo letu vinavyohusiana? Kipengele cha muhimu kabisa maishani ni uhusiano wetu
na Mungu! Je, utadhamiria leo kukuza talanta zako ili kuuendeleza Ufalme wa
Mungu?
V. Juma lijalo: Ufalme wa Mungu.
MWANZA:BILIONI MOJA NA NUSU ZATUMIKA KUJENGA HOSPITAL YA WAADVENTISTA WA
SABATO YA MWANZA (MAMC)
Hospitali ya Waadventista Wa Sabato ya Mwanza (MAMC) inavyoonekana kwa
sasa.
Hospitali ya Waadventista wa Sabato, Mwanza Adventist Medical
Centre(MAMC),sasa iko katika hatua za mwisho za Ujenzi.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Afya ya Kanisa la Waadventista wa Sabato
Jimbo Kuu la Kaskazini mwa Tanzania (NTUC), Dk Silas Kabhele, amesema
zaidi ya shilingi bilioni moja na nusu za Tanzania zimetumika kujenga
Hospitali hiyo.
Dk.Kabhele ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Afya katika Jimbo la
Kusini mwa Ziwa Nyanza(SNC) amesema hivi karibuni kwamba sasa
zinahitajika takriban shilingi milioni 600 kukamilisha ujenzi.
Hospitali hiyo ya Gorofa tano tayari paa limeezekwa,kuta zote za nje
zimepigwa lipu na kwamba hata baadhi ya kuta za ndani zimepigwa lipu.
Hospitali ya Pasiansi ikikamilika itafanana hivi
Copy and WIN : http://ow.ly/KNICZ
Copy and WIN : http://ow.ly/KNICZ
No comments:
Post a Comment