(Yakobo
1:12-21)
Somo hili limetafsiriwa
kutoka katika Copr. 2011, Bruce N. Cameron, J.D. Marejeo yote ya maandiko
yametoka kwenye tafsiri ya New International Version (NIV), copr. 1973, 1978,
1984 International Bible Society, isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo. Nukuu
kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya NIV inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji wa
Biblia wa Zondervan. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi
(kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sehemu
nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Kama huwa una kawaida ya
kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na hukulipata kwa juma moja, unaweza
kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na
http://www.GoBible.org
kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa,
Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.
Utangulizi: Hebu tupitie tena masomo yetu mawili yaliyopita.
Yakobo anawaandikia Wakristo wa Kiyahudi waliokimbia makwao kutokana na mateso.
Yakobo anawaambia kuwa waitafute furaha katika majaribu. Wale walioyakimbia
makazi yao huenda hawakuweza kuchukua mali zao zote. Hivyo, jambo linalofuata
Yakobo anawaambia kuwa wawe na fahari “katika mazingira ya unyenyekevu.” Furaha
na fahari kwa wale wanaoshughulika/wanaokabiliana na matatizo makubwa. Haya ni
mafundisho yenye changamoto. Kama unaweza kuwa na furaha na kuona fahari
katikati ya matatizo, basi jambo hilo litakuwa la pekee! Hebu tuzame kwenye
somo letu la Biblia ili tuone Yakobo anaelezea suluhisho gani linalofuatia!
I.
Taji ya uzima
A.
Soma Yakobo 1:12. Baada ya hili tatizo thawabu gani
inafuatia? (“Taji ya uzima!”)
1.
Unalipataje taji hili? Unaupataje uzima wa milele?
Yakobo anatupatia uwezekano wa namna mbili:
a.
Kulishinda jaribu; au,
b.
Kumpenda Mungu. Je, unadhani ni jambo moja, yote
mawili, au si lolote kati ya hayo?
B.
Soma Tito 3:4-7. Je, mafungu haya yanatoa mwangaza gani
katika Yakobo 1:12? (Tito anasema hatuokolewi “kutokana na matendo ya haki
tuliyoyatenda.” Hiyo inamaanisha kuwa “kulishinda jaribu” si jibu sahihi ikiwa
“jaribu” ni aina fulani hivi ya matendo. Tito anasema kuwa tuliokolewa “wema na
upendo wa Mungu Mwokozi wetu ulipofunuliwa.” Kumpenda Mungu aliyetupenda kwanza
ndilo linalopaswa kuwa jibu sahihi.)
1.
Ikiwa pia unapenda “kulishinda jaribu” ndilo jibu
sahihi, unadhani “jaribu” linahusisha jambo gani? (Jaribio la imani ndilo
litakalofanya kazi. Utakumbuka juma lililopita Yakobo aliandika kuwa “imani” ni
ya muhimu katika kupokea vitu kutoka kwa Mungu. Yakobo 1:6-7.)
II.
Kishawishi/jaribu
A.
Soma Yakobo 1:13. Fikiria tena kuhusu historia ya wale
ambao Yakobo anawaandikia. Kwa nini walishawishika kufikiri kuwa Mungu alikuwa
akiwajaribu? (Wao ni waongofu wapya kwenye Ukristo. Mara baada ya kuongolewa,
wanatakiwa kukimbia. Katika makao yao mapya wao ni wahamiaji masikini. Nani ana
makosa kutokana na majaribu waliyonayo sasa? (Unaweza kuona mahali wanapoweza
kushawishika kumlaumu Mungu. Hii ndio sababu ya Yakobo kuandika kuwa Mungu
atawavika taji!)
B.
Soma Yakobo 1:14. Tunajaribiwaje? (Tunafahamu kutoka
katika kisa cha Hawa (Mwanzo 3:1-6) kuwa Shetani pamoja na wenzi wetu wanaweza
kutujaribu. Lakini, fungu hili linasema kuwa tunajitia majaribuni sisi
wenyewe.)
1.
Je, hii inamaanisha kuwa tuna mwelekeo wa asili dhidi
ya dhambi? (Ndiyo!)
2.
Soma Isaya 64:6. Fungu hili linasema nini kuhusu
matendo yetu? (Yanafanana na nguo zilizotiwa unajisi. Kwa dhahiri, tunalo tatizo.)
C.
Angalia tena Yakobo 1:14. Je, haya “majaribu
tunayojitia majaribuni sisi wenyewe” yana nguvu kiasi gani? (Hakika yana nguvu
kiasi cha kutosha “kutuingiza dhambini.”)
D.
Soma Yakobo 1:15. Je, umewahi kuuona mto mkubwa na
kujiuliza kuwa ulianzaje anzaje? Je, dhambi inayotusababishia mauti inaanzia
wapi? (Inaanza na matamanio yetu maovu. Inaanzia mawazoni mwetu.)
1.
Kwa uzoefu wako jambo hili linaonekana kuwani sahihi au
baya? Ni mara ngapi “umejikwaa” dhambini? Ilitokea tu kwa isivyo bahati. Mara
ngapi dhambi yako ni matokeo ya wewe kuifikiria sana, au labda kufikiria juu ya
aina ya dhambi ya kiwango cha chini?
E.
Soma Mathayo 15:17-19. Yesu anasema kuwa chanzo cha
dhambi ni nini? (“Moyo.” Yesu anaposema, “moyo” anamaanisha mawazo yetu, tamaa
zetu. Yakobo na Yesu wanakubaliana kuwa dhambi ina mwelekeo unaotabirika.
Kwanza tunalifikiria na kulitafakari wazo akilini mwetu. Baada ya kulifikiria
vya kutosha tunaanza kulifanyia kazi. Baada ya kipindi fulani dhambi “inakua na
kukomaa” (Yakobo 1:15) na tukiendelea kupiga hatua zaidi, dhambi inatupa
umauti.)
F.
Soma Warumi 8:5-8. Tunapaswa kufanya nini kuhusu tamaa
zetu ovu? (Usiyaweke mawazo yako kwenye mambo hayo.)
1.
Je, unadhani “kuyaweka mawazo yako” inamaanisha nini?
Je, inamaanisha kuwa usilifikirie jambo ovu linalokusababishia matatizo?
2.
Soma Warumi 7:7-11. Chanzo cha kutamani ni kipi?
(Dhambi pamoja na amri ya kutotamani.)
3.
Fikiria jambo hili. Tukiyaacha mawazo yetu yajikite
kwenye jambo ovu, hiyo ndio njia isababishayo kutenda dhambi. Lakini,
tukizingatia amri inayotuambia tusitende jambo ovu, hiyo huzaa tamaa mbaya. Je,
suluhisho ni lipi? (Ikiwa uelewa wangu uko sahihi, tunapaswa kuepuka kufikiria
juu ya dhambi, na kuepuka kuifikiria amri inayokuambia usitende dhambi.)
G.
Soma Warumi 8:5 tena. Suluhisho la pambano la mawazo ni
lipi? (Badala ya kujikita kwenye dhambi zako – ama dhambi au katazo – badala
yake fikiria kile atuwaziacho Mungu. Jikite kwenye kile unachoweza kukitenda
kuuendeleza Ufalme wa Mungu.)
H.
Soma Yakobo 1:16. Angalia muktadha wake. Unadhani
Yakobo anawaza juu ya udanganyifu gani? (Muda mfupi uliopita Yakobo amekanusha
wazo kwamba Mungu anatujaribu. Muktadha unaashiria kuwa tusidanganyike na wazo
kwamba Mungu atatujaribu.)
I.
Soma Yakobo 1:17. Yakobo anaandika kuhusu thawabu za
namna gani? Je, muktadha unaashiria nini? (Muktadha unaashiria kuwa bado
tunazungumzia kuhusu majaribu. Kama niko sahihi, hii inaunga mkono wazo la
kwamba hatupaswi kujikita kwenye dhambi, hatupaswi kujikita kwenye amri
inayotusababisha tutake kutenda dhambi, hatupaswi kujikita kwenye matatizo
yetu, badala yake tunapaswa kujikita kwenye mibaraka mikuu ambayo Mungu
ametupatia na jinsi tunavyoweza kuiendeleza kazi ya Mungu.)
1.
Je, tafsiri yangu juu ya jambo hili italeta mantiki
yoyote kwa watu waliofukuzwa kutoka makwao na sasa ni masikini? (Je, unaweza
kuona kuwa hoja ya Yakobo inaingia hapa kikamilifu? Yakobo anasema kuwa furaha
na fahari vinaweza kuonekana katika mazingira kama hayo. Furaha na fahari ni
thawabu. Jikite kwenye thawabu za Mungu.)
III.
Karama ya Uzima
A.
Soma Yakobo 1:18. Kuzaliwa gani kunarejewa hapa? (Soma
1 Petro 1:3-4. Yakobo hazungumzii juu ya kuzaliwa kwetu, anazungumzia juu ya
kuokolewa kwetu.)
B.
Angalia tena Yakobo 1:18. Tunaokolewaje? (“Kwa njia ya
neno la kweli.”)
1.
Je, “neno la kweli” ni lipi? (Yohana 1:1 inatuambia
kuwa Yesu ni “Neno,” lakini nadhani Yakobo anamaanisha jambo hili kwa mapana
zaidi – mafundisho juu ya Yesu.)
2.
Je, “mavuno ya kwanza” ni mazuri? (Fausset anatuambia
“Mazao yote ya nchi yalitolewa wakfu kwa Mungu kwa kuyaweka wakfu mavuno ya
kwanza.” Yakobo anawahamasisha hawa Wakristo wa awali kwa kusema kuwa wao ni wa
wa pekee kwa Mungu, wao ndio mwanzo wa mavuno. Nakutia moyo!)
a.
Je, ujumbe wa jumla kwa hawa Wakristo wanaoteswa ni
upi? (Nyie ni wa pekee. Nyie ni wa kwanza. Majaribu yenu yanawapatia mtazamo wa
ukomavu unaoruhusu furaha. Mungu hakuleta matatizo haya, Mungu anawapatia
thawabu nzuri pekee.)
IV.
Hekima Kivitendo
A.
Soma Yakobo 1:19-20. Tulijadili mafungu haya katika
somo la kwanza na tukahitimisha kuwa huu ni ushauri unaotupatia utawala mkubwa
wa hisia. Soma tena Yakobo 1:13. Suala la pekee kwa hawa Wakristo wa awali ni
lipi? (Wanaweza kudhani kwamba kwa kuwa Yesu aliteseka na kufa, Mungu alikuwa
anawapa mateso, manyanyaso na umasikini. Kimsingi Yakobo anasema “Hii si kweli.
Mungu anatoa thawabu nzuri pekee. Hii ni kazi ya Shetani. Acha ushauri huu
uzame akilini. Tafakari, badala ya kuzungumza. Usikasirike haraka.”)
B.
Soma Yakobo 1:21. Yakobo anaandika, “Liwezalo kuziokoa
roho zenu.” Kutuokoa kutoka kwenye nini? (Hapo awali tulijifunza kuwa hatuwezi
kuupata uzima wa milele kwa matendo yetu. Lazima hii imaanishe kuwa kulikiri
neno la Mungu, kuachana na “unajisi wote wa kimaadili na uovu uliotapakaa
sana,” hutuokoa dhidi ya matatizo.)
1.
Kwa nini Yakobo anatuambia “tupokee kwa upole” neno la
Mungu? (Fundisho la Yakobo linaonekana kukinzana sana. Anawaambia kuwa mateso
huleta furaha. Tunaweza kudhani kuwa “unajisi wa kimaadili” huleta furaha,
lakini kiukweli huleta matatizo. Yakobo anasema kuwa tunatakiwa kuweka kando
fahari yetu na kuyakiri maneno yatakayotupatia furaha na amani.)
C.
Rafiki, vipi kuhusu wewe? Je, uko radhi kuyakubali
maneno ya Yakobo yanayoonekana kukinzana na ujumbe wa ulimwengu? Je, uko radhi,
kuanzia sasa, kuupatia ushauri wake nafasi maishani mwako?
V. Juma lijalo: Being and Doing.
No comments:
Post a Comment