Watu mbalimbali wamekuwa wakichanganyikiwa
kuhusu siku ya sabato kuwa ni ipi katika juma lakini leo tutaacha vitabu
vikuu vya imani nyingi pekee vitupatie ufumbuzi wa jambo hili.
Tuanze na biblia Mungu anasema mahali fulani
kuwa sabato ni siku ya saba, Kutoka.20:8-11, “Ikumbuke SIKU YA SABATO
uitakase. Siku sita fanya kazi utende mambo yako yote; lakini SIKU YA
SABA NI SABATO YA BWANA, Mungu wako siku hiyo usifanye kazi yo yote,
wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi
wako. Wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango
yako. Maana, kwa siku sita BWANA alifanya mbingu, na nchi, na bahari,
na vyote vilivyomo, akastarehe SIKU YA SABA; kwa hiyo BWANA akaibarikia
siku ya sabato akaitakasa.” Hapa tunaona kuwa siku ya SABA NI SABATO ya
BWANA MUNGU, hivyo katika juma moja la siku sita basi siku moja ni
sabato ya BWANA. Katika siku hiyo Mungu anasema usifanye kazi yako yo
yote wewe, mali zako hata watu wa nyumbani kwako.
Lakini je, katika juma siku ya saba ni ipi? Au
kwa maana nyingine siku ya sabato ni ipi? Biblia inatoa jibu kuwa sabato
ni SIKU YA JUMAMOSI, Mathayo.28:1,5 inasema “Hata SABATO ilipokwisha,
ikipambazuka SIKU YA KWANZA ya juma, Mariamu Magdalene, na Mariamu Yule
wa pili, walikwenda kulitazama kaburi. Malaika akawajibu, akawaambia
wale wanawake, Msiogope ninyi; kwa maana najua ya kuwa mnamtafuta Yesu
aliyesulibiwa. Hayupo hapa; kwani AMEFUFUKA kama alivyosema.” Kumbe
sabato yaani siku ya saba ni siku inayotangulia kabla ya siku ya kwanza
ya juma. Katika biblia ya Kiswahili cha kisasa ya habari njema fungu
hili linasomeka vizuri kabisa kuwa “Baada ya SABATO, karibu na
mapambazuko ya SIKU ILE YA JUMAPILI, Maria Magdalene na yule Maria
mwingine walikwenda kutazama lile kaburi.” Hapa biblia inaonesha kuwa
siku ya sabato ni siku moja kabla ya Jumapili, maana sabato ikiisha
jumapili huanza. Je, siku hiyo ni ipi? Jibu ni rahisi sana nalo ni
JUMAMOSI.
Hadi leo, watu wote wanajua kuwa Yesu aliteswa
na kufa siku ya Ijumaa, akalala kaburini siku ya Jumamosi na Jumapili
akafufuka. Siku hii ya mateso na kifo cha Yesu inaitwa IJUMAA KUU, ni
siku ya IJUMAA. Kipindi kile siku hii iliitwa SIKU YA MAANDALIO YA
SABATO, Luka. 23:53-54 “Akaushusha(mwili wa Yesu), akauzinga sanda ya
kitani, akauweka katika kaburi lililochongwa mwambani, ambalo hajalazwa
mtu bado ndani yake. Na SIKU ILE ILIKUWA SIKU YA MAANDALIO, na SABATO
ikaanza kuingia.” Hivyo siku moja kabla ya Sabato inaitwa siku ya
Maandalio yaani Ijumaa nayo ilikuwa siku ya kujiandaa maana siku ya
sabato hawakufanya kazi yoyote. Biblia ya Kiswahili cha kisasa ya habari
njema inasema, “Siku hiyo ilikuwa IJUMAA, na maandalio ya siku ya
SABATO yalikuwa yanaanza”. Kwahiyo sabato ni siku iliyo katikati ya
IJUMAA NA JUMAPILI ambayo ni Jumamosi si ndiyo?
Hata Kurani nayo inashuhudia kuwa sabato ni siku
ya saba yaani Jumamosi nayo inatakiwa kutumika kwajili ya ibada, katika
surat Al-Baqarah(2) kifungu sha 65 imendikwa; “Na kwa yakini mmekwisha
kujua khabari za) wale walioasi miongoni mwenu katika (amri ya
kuihishimu) jumamosi. Basi tukawaambia: “kuweni manyani wadhalilifu”.
Hapa tunaona kuwa Kurani inasema siku ya jumamosi ni siku inayotakiwa
kuheshimiwa na kutofanya hivyo ni uasi yaani ni dhambi. Pia surat
Al-Aaraf(7) kifungu cha 163a inakazia kuwa “Na waulizeni habari za mji
ambao ulikuwa kando ya bahari;(watu wa mji huo) walipokuwa wakivunja
(sheria ya) Jumamosi (ambayo waliambiwa wasifanye kazi katika siku hiyo,
wafanye ibada tu.” Hapa tunaona Kurani ikiunga mkono biblia kwamba siku
ya sabato yaani jumamosi ni siku ya kutofanya kazi kabisa bali ni siku
ya kufanya ibada tu.
Nawe msomaji wa ujumbe huu haijalishi imani yako
ni ipi au itikadi yako ni ipi Biblia na Kurani vinakutaka leo urudishe
utukufu wa Bwana katika sabato yake takatifu siku ya Jumamosi wala si
katika siku nyingine yoyote. Nenda katika kanisa lolote jumamosi ya juma
hili, uungane na waabuduo halisi wamwabuduo Mungu katika Roho na Kweli.
Na MUJAYA MUJAYA, 0767578122.
No comments:
Post a Comment