Zaidi ya watu 150 wamebatizwa
na kujiunga na kanisa la Waadventista wa Sabato tarehe 23 Agosti 2014
mjini Moshi. Mkutano huo unaendeshwa na Makamu wa Mwenyekiti wa kanisa
la Waadventista wa Sabato ulimwenguni Mchungaji Geoffrey Gabriel Mbwana
akishirikiana na Mchungaji Caleb J. Migombo wote wakitokea nchini
Marekani. Mkutano huo ni wa siku 21 kuanzia tarehe 16/08 - 06/09/2014 na
unafanyika katika viwanja vya mashujaa mjini Moshi. Sambamba na mkutano
huo pia kuna huduma mbalimbali zinatolewa zikiwepo huduma za ushauri
nasaa, mafundisho ya Ujasiliamali na mafunzo ya Komputa. Kabla ya
mahubiri wasikilizaji wanapata muda mzuri wa kusikiliza masomo ya Afya
na Kaya na Familia.
Mchungaji Geoffrey Mbwana akihubiri
Hapa akionyesha kielelezo cha Mwana kondoo
Zaidi ya watu mia moja na hamsini wamebatizwa kama unavyowaona wakiwa wamevalia vazi jeupe.
No comments:
Post a Comment