MOROGORO: KITABU CHA MWAKA 2017 "PENDO LISILO KIFANI" CHAZINDULIWA NA MWENYEKITI WA UNIONI JIMBO LA KUSINI MWA TANZANIA MCH. MARK W. MAREKANA, KINUNUE KWA TSH 2,000 TU NAWE UGAWE BURE KWA MARAFIKI

Kanisa la waadventista wa Sabato Union ya Kusini mwa Tanzania lazindua kitabu kipya cha mwaka 2017. Huduma hii ilifanywa na Mwenyekiti wa Union Pr Marekana kwa ushirikiano na wachungaji wengine.
Aidha huduma hii ilihudhuriwa na maelfu ya waumini waliokusanyika katika ibada ya Sabato tar 22/10/2016 katika viwanja vya Misufini mjini Morogoro, akiwemo Mkurugenzi wa Nyumba za uchapishaji wa makao makuu ya kanisa Pr. Wilma toka Marekani.
Vitabu hivi kwa Sasa vinapatikana katika Ofisi za majimbo (conference) yote Tanzania kwa sh 2,000 tu za kitanzania.
Wito Wangu Leo nunua nakala nyingi na kuzisambaza Bure kwa Rafiki zako.
Usiionee haya injili ni uweza wa Mungu uletao wokovu.  

Habari/picha na Richard J. Bananga

No comments:

Post a Comment