MUIMBAJI, BLOGGER NA MC EDMUND MIPAWA ASHEHEREKEA SIKU YAKE YA KUZALIWA KATIKA UFUKWE WA MSASANI KWENYE TUKIO LA IMBA KWA AKILI

Siku ya Agosti 28, 2016 ilikuwa maalum kwa tukio la kukutana kwa waimbaji wa nyimbo za injili kwa ajili ya kupeana uzoefu wa mambo kadhaa hasa ya kimziki lakini ikiwemo ubunifu wa kazi kabla na baada ya kuitoa studio na hatimae kwa wasikilizaji. 
Lakini pia siku hiyo ilikuwa muhimu pia kwa mdau wetu kijana mchapakazi na mshereheshaji pia blogger Mr Edmund Mipawa ambaye siku hiyo ilikuwa maalum kwa kuzaliwa kwake akitimiza miaka kadhaa. Siku hiyo waimbaji na waalikwa wote walipata fursa ya kumpongeza kwa kumuimbia nyimbo kadhaa huku pia wakimlisha keki na furaha isiyokifani ilitawala. 
Kushoto ni Mrs Martin Ngussa alipokuwa kwenye tukio la kumlisha keki Eddy
Edmund alipokuwa akisema machache kabla ya kukata keki
Muda wa kukata keki uliwadia...
Kushoto ni Mr Martin Ngussa ambaye ni mratibu wa tukio la Imba kwa akili na kulia ni Edmund

No comments:

Post a Comment