LESONI JUMAMOSI AGOSTI 27: YESU ALIWAFANYA WAMWAMINI

Sabato Mchana

Soma Kwa Ajili ya Somo la Juma Hili: Mwa. 15:6, Hes. 14:11, 1 Kor. 3:1–9, Dan. 6:1–3, Neh. 2:1–9, Kum. 4:1–9, Mdo. 2:42–47

Fungu la Kukariri: “‘Lakini habari zake zikazidi kuenea, wakakutanika makutano mengi wamsikilize na kuponywa magonjwa yao.’” (Luka 5: 15).

Kwa miaka kadhaa, Kanisa la Waadventista Wasabato katika eneo Fulani lilikuwa likitoa kifungua kinywa kwa muda wa siku tano kwa juma katika shule ya awali ya eneo lile.

 Ingawa serikali ya nchi ile haikuwa ya kidini, lakini ilipitisha sheria kutoa pesa kwa kila shule ya serikali ili kuwa na mchungaji, shule pamoja na jamii walilitaka kanisa la Waadventista kutoa mwalimu na Mchungaji mmoja, ni nadra sana kuliomba dhehebu moja tu kufanya hivyo. Jukumu la Mchungaji ni kuwasaidia wanafunzi na jamii nzima ya hapo shuleni, mahitaji ya kimwili, Kihisia, na kiroho. Fursa hii ilikua yakushangaza.

“ Nina furahia uhusiano wa kipekee na maalumu tulionao na kanisa lako,” Mkuu wa shule alimwambia Mchungaji ambaye alikuwa akiitembelea shule, “ Natamani madhehebu mengine, yafanye kama unavyofanya.” Wakati Mchungaji alipokuwa anaondoka katika jamii ile, Afisa Uhusiano wa shule ile alimshukuru kwa kile kanisa lilichokua likifanya na kumuomba kama angeweza kuhudhuria Sabato moja.

Juma hili tutachunguza suala la kuishinda Imani ya watu ambao sisi tunahitaji kuwahudumia na kuwaleta kwa Kristo.
Somo la juma hili limetafsiriwa na Naetwe E.Kimweri pamoja na Agape P. Mrindoko.

No comments:

Post a Comment