KIKUNDI CHA THE HEALING VOICE KUTIMIZA MWAKA MMOJA, LEO WATASHIRIKI HAFLA FUPI PAMOJA NA WAIMBAJI WENZAO KATIKA PICNIC YA PAMOJA

 Akizungumza na injilileo Blog katika studio za blog hii, 
mratibu wa huduma wa kikundi cha The Healing Voice Mr Baraka Ogillo amesema kikundi hiki kilianzishwa mwaka jana 2015 Septemba 5 na leo itakuwa ni hafla fupi ya kusheherekea mwaka huo huku siku ya kesho kikundi kitakuwa kinatimiza mwaka mmoja wa huduma ya uimbaji.
Kikundi kina waimbaji kumi na saba, watano sauti ya kwanza, sauti ya pili wanne sauti ya tatu watano na bezi watatu.
Kwa mwaka mmoja waimbaji hawa toka kanisa la Waadventisa wa Sabato Ushindi wamepata mafanikio ikiwemo kufanya audio mbili na Santuri muonekano moja na waliweza kutembelea kituo cha waliathirika na madawa ya kulenya kilichopo Tegeta DSM kinachoitwa CHANGAMOTO NI MATUMAINI.
Baraka Ogillo mratibu wa huduma The Healing Voice
Changamoto ya kiuchumi ndio kubwa katika kikundi na malengo yao ni kufanya uinjilisti kama ndio lengo kuu la kuanzisha kikundi hiki na lengo lingine ni kufanya mahubiri sehemu mbalimbali mwanzoni mwa mwaka unaoanza Jumatatu Septemba 5, 2016 .

No comments:

Post a Comment