KILIMANJARO: MCHUNGAJI DR LEKUNDAYO AMEWATAKA WACHUNGAJI NA WAUMINI WOTE KUTUMIKA KWA UAMINIFU KATIKA KAZI YA INJILI BILA KUJALI CHANGAMOTO ZINAZOWEZA KUJITOKEZA

 Kiongozi Wa kanisa la Waadventista Wa Sabato Jimbo Kuu kaskazini mwa Tanzania Mchungaji na Dr. Godwin Lekundayo amewataka wachungaji na waumini wote kutumika kwa uaminifu katika kazi ya injili bila kujali changamoto zinazoweza kujitokeza.Dr Lekundayo ameyasema hayo jana katika kanisa la Waadventista Wa Sabato Njoro Mkoani Kilimanjaro, wakati alipokuwa katika Huduma ya Kuwatenga Rasmi wachungaji 6 kwa ajili ya kazi ya injili.Aidha Dr Lekundayo aliwaasa wachungaji hao kufanya kazi kwa kuwatembelea waumini katika nyumba zao bila kujali Tabaka,umri,utajiri,umaskini ama ukabila Kwa kuwa hata Yesu alitumikia watu wote kwa uaminifu.



 Habari na Abel Kinyongo 

No comments:

Post a Comment