IMEFIKA SIKU YA VIJANA WA KANISA WAADVENTISTA WA SABATO DUNIANI KUONESHA MATENDO YA HURUMA, VIJANA WAASWA KUSHIRIKI TUKIO HILI KUBWA JIJINI ARUSHA

Vijana wa kanisa la Waadventista Wa sabato jijini Arusha wameaswa kujitoa katika kuihudumia jamii na kuwa kielelezo bora ili vijana wengine waige tabia hiyo kwani kuzidi kufanya hivyo kutawafanya wengi wamjue Yesu nakujiunga na kanisa.

Akizungumza na Morningstar Redio hii leo katika wiki ya matendo ya huruma yanayoendelea katika ulimwengu mzima yanayofanywa na kanisa la Waadventista Wa sabato, Mkurungenzi wa idara ya vijana katika jimbo la kasikazini Mashariki mwa TanzaniaNETC Mchungaji John Kimbute amesema kuwa, ili jamii imfahamu Yesu nilazima vijana kujitoa kikamilifu wakiiga mfano wa Yesu kwa kuwaona wenye mahitaji mbali mbali na kuwasaidia.

Aidha nao vijana walio shiriki katika zoezi la kufanya usafi katika maeneo ya stand jijini Arusha wamesema kuwa kanisa limeanzisha mfumo mzuri unao wafanya kujua namna ya kuifikia jamii sio tu kwa fedha bali kuwafanya vijana kutumia nguvu zao katika kuisaidia jamii
Nao wakazi wajiji la Arusha walio shuhudia vijana hao wakifanya huduma mbalimbali katika maeneo hayo ikiwemo kufyeka eneo la makaburi ya stand, kuzoa taka zilizo zunguka maeneo hayo pamoja na kufagia maeneo yanayo zunguka eneo la uwanjwa wa shehk amri abeid wamelipongeza kanisa la Waadventista Wa sabato kwani wamekuwa mfano wa kuigwa .

No comments:

Post a Comment