NENO LA LEO - SIMAMA; BADO KUNA TUMAINI

Zaburi 40:1-2 "Nalimgoja Bwana kwa saburi, akaniinamia akakisikia kilio changu. Akanipandisha toka shimo la uharibifu, toka udongo wa utelezi; Akaisimamisha miguu yangu mwambani, akaziimarisha hatua zangu."

Ni jambo la kawaida katika kizazi chetu kushudia watu wengi wakipitia maisha ya kukatisha tamaa na kuvunjika moyo, mwanadamu amezungukwa na kila aina ya mitego, ambayo wengi huishia kunasa kwenye matope ya utelezi na hatimaye kushindwa kujinasua. 

Maisha ya Daudi ni mfano wa maisha ya watu wengi wa kizazi hiki, bila kujali wanajiita watu wa Mungu au laa, wengi wanapitiwa na mishale ya yule adui, na hatimaye kupitia changamoto za maisha yenye majeraha na uchungu mioyoni. 

Bila kujali hatua za miguu yako iliposimama, iwe ni kwenye utelezi wa dhambi; au shimo refu la matatizo, Mungu yuko tayari kukutoa na kukupandisha juu na hatimaye kukupatia ushindi kama alivyompatia Daudi. 

Yesu Kristo alikufa msalabani ili kutuokoa kutoka katika kila mitengo na tanzi za adui shetani. Ni wakati uliokubalika kupokea wokovu na kusimama katika tumaini la ushindi daima. 

UPENDO WA MUNGU UKATAMALAKI KWA KILA MMOJA WETU - NAWATAKIA SIKU NJEMA. 

Na: Ev. Eliezer Mwangosi
Simu: 0767210299

No comments:

Post a Comment