Leo nimeona ni vema nitoe majibu ya swali lililoulizwa na wakristo
wengi juu ya chanzo cha sikukuu ya Krismas ya tarehe 25 Desemba.
Swali:
Ni nini Chanzo cha sikukuu ya Krismass ya tarehe 25 Desemba? Je ni kweli Yesu alizaliwa tarehe hiyo?
Jibu:
Wakristo wengi wanaamini kuwa Yesu hakuzaliwa tarehe 25 December, kwa
sababu Mariamu alipata uja uzito kati ya Mwezi wa sita (Juni) mwishoni –
Hivyo kama kawaida ya binadamu, uja uzito unachukuwa miezi tisa ili
mtoto azaliwe, hivyo ni wazi Yesu alizaliwa majira ya mwezi wa Februali.
Ila hakuna Andiko la Biblia wala Historia iliyoweka kumbukumbu ya
tarehe ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo.
Kwenye Biblia tunaikuta
tarehe 25 December, kuwa ni sikukuu iliyokuwa inasherehekewa na wapagani
wa Babeli ambako Waisraeli walichukuliwa mateka. Hivyo sikukuu ya 25
Desemba ilikuweko kabla ya Kuzaliwa Yesu, na ilikuwa sikukuu ya wapagani
wa Babebli wakisherehekea kuzaliwa kwa Mtoto wa Mungu JUA aliyeitwa
TAMUZ.
Kulikuwa na Mfalme wa babeli aliyeitwa , na mke wake
ambaye pia aliitwa Malkia wa Mfalme jina lake aliitwa baada ya Mfalme
Nimrudi kufariki, Mke wa mfalme akabeba mimba nje ya Ndoa. Ili kuficha
kitendo hicho cha mke wa mfalme kubeba mimba wakati mume wake amefariki,
akatunga UONGO kuwa Mume wake HAKUFA ila alibadilika kuwa Jua (SUN),
hivyo mionzi ya Jua wanayoiona ndiyo iliyomdunga Mimba. Wababeli kwa
kuwa walikuwa waabudu mizimu waliamini Uongo huo na kuanza Kuliheshimu
Jua (SUN) kama Mungu wao.
Usiku wa kuamkia Tarehe 25 Desemba,
Semiramis akazaa Mtoto aliyemwita TAMUZ, ambaye baba yake ni Mungu Jua.
Imani yao ilienda mbali zaidi hadi kuamini kuwa tendo la Semiramisi
kuzaa na Mungu jua yeye pia ni Mungu Mke na Mtoto wao Tamuz akaitwa
Mungwa Mwana. Kuanzia kipindi hicho wapagani wa Babeli tarehe 25 mwezi
wa 12, waliweka sherehe kubwa ya kuzaliwa kwa Mungu Mwana Tamuz.
Biblia inatoa maelezo juu ya jambo hilo la kufanya sherehe ambayo mfalme
aliitumia kufungua baadhi wafungwa, kama msamaha wakati wa sikukuu -
Yeremia 52:31 “Hata ikawa, katika mwaka wa thelathini na saba wa
kuhamishwa siku ya ishirini na tano ya mwezi, chake Yehoyakini,
mfalme wa Yuda, akamtoa gerezani.”
Nabii Yeremia aliandika kitabu
hicho zamani kabla ya Yesu kuzaliwa, taifa la babeli lilikuwa na
Desturi ya kuweka huru wafungwa katika siku hii ya Kuzaliwa kwa Tamuz
tarehe 25 Desemba. Enzi hizo haikuwa inaitwa Krismass huenda iliitwa
Tamuz–Mass.
Baada ya Yesu kuzaliwa, hapakuwa na Sikukuu ya
Krismass hata mitume hawakuwahi kusherehekea sikukuu hii, bali tunaona
baada ya miaka mingi kupita karibia zaidi ya miaka 300 Mfalme Constatino
wa Dola ya Kirumi aliyekuwa anaabudu JUA alimua kuwa Mkristo, lakini
hakutaka kuacha Desturi za kuifanyia sherehe miungu yake. Hivyo akaamuru
sherehe ya kuzaliwaMungu Mwana Tamuz iendelee kusherehekewa ila
wakristo waambiwe kuwa ni siku ya kuzaliwa Yesu Kristokinachoitwa “The
Compact History of Roma cathoric church” kinaeleza juu ya tangazo la
Mfalme Constantino kwa wakristo kuanza kuadhimisha sikukuu za kipagani
ikiwemo Ibada ya JUA ya siku ya Kwanza (SUN-DAY) badala ya Ibada ya Siku
ya SABA, historia inaeleza kuwa alitoa maagizo hayo akiwa bado mpagani
(Kabla ya kubatizwa), tangazo hilo lilitolewa mwaka 325AD.
Historia inasema, ilikuwa ni mwaka ndipo kanisa lilipoamua kwamba, ya
kuwa na sikukuu ya kipagani mjini Rome ” au The Birthday of
theinvincible/unconquered Sun, iliyosherekekewa tarehe , sasa tarehe
hiyo iwe si kwa kuzaliwa jua, bali iwe siku ya kuzaliwa mwana (son) wa
Mungu – Yesu Kristo. Kwa mara ya kwanza kanisa lilikuwa linaendesha Misa
tu, lakini baadaye mtindo wa sherehe za kipagani ikaingizwa hadi leo
inaendelea – ikitawaliwa na Vinywaji (Vileo), Vyakula na starehe za kila
namna.
MASWALI YA CHANGAMOTO:
1. Kwa nini Mungu
hakuona haja ya kuwa na siku ya kuadhimisha kuzaliwa kwa Yesu Kristo?
Hata hakuiweka wazi tarehe na siku ya kuzaliwa kwa Yesu?
2. Ilikuwaje Mitume na Kanisa la awali hawakuwa na wazo hilo la sherehe ya Krismasi?
3. Kwanini wakristo walazimishwe kusherehekea sikukuu ya kuzaliwa
Yesu katika tarehe ya Kuzaliwa Mwana wa Mungu JUA? Na mfalme ambaye wala
hakuwa Mkristo wakati huo?
4. Kwa nini wakristo wasiweke
Tarehe ya kwao ambayo inaendana na mwezi hata kama Tarehe haijulikani?
Make miezi tisa kutoka June ni February / March.
MUNGU AWABARIKI WOTE MNAPOENDELEA KUTAFAKARI JUU YA UKWELI HUU UNAOTUSAIDIA KUKUA KIROHO.
Ev. Eliezer Mwangosi
Eliezer.mwangosi@yahoo.com
No comments:
Post a Comment