Oktoba 30
Jitunze
nafsi yako, na mafundisho yako. Dumu katika mambo hayo; maana kwa
kufanya hivyo utajiokoa nafsi yako na wale wakusikiao pia. 1 Timotheo
4:16.
Agizo
hilo lililotolewa kwa Timotheo linapaswa kuzingatiwa katika kila
nyumba, na kuwa ndiyo mamlaka ya kufundishia katika kila familia na kila
shule.... Lengo kuu kuliko yote la vijana wetu lisingekuwa kujitahidi
sana kupata kitu fulani kipya. Hapakuwa na kitu kama hicho katika fikra
na kazi ya Timotheo. Yawapasa kukumbuka kwamba, mikononi mwa yule adui
wa mema yote, maarifa peke yake yanaweza kuwa uwezo wa kuwaangamiza
wenyewe. Alikuwa ni yule kiumbe mwenye akili nyingi sana, yule
aliyekalia cheo cha juu miongoni mwa halaiki ile ya malaika, ambaye
mwishowe aligeuka na kuwa mwasi; na wengi wa wale walio na mafanikio
makubwa kiakili sasa wanatekwa kwa uwezo wake [Shetani]. Vijana
wangejiweka wenyewe chini ya mafundisho ya Maandiko Matakatifu, na
kuyaweka kila siku katika mawazo na maisha yao kwa matendo. Hapo ndipo
watakuwa nazo sifa za tabia zinazowekwa katika daraja la juu kabisa
katika majumba yale ya kifalme kule mbinguni. Watajificha wenyewe ndani
ya Mungu, na maisha yao yatashuhudia utukufu wake. ----- YI, Mei 5,
1898. "Jitunze nafsi yako, na mafundisho yako." Wewe mwenyewe
unahitaji kuangaliwa kwanza. Jitoe kwanza wewe mwenyewe kwa Bwana ili
upate kutakaswa kwa ajili ya kazi yake. Kielelezo chako cha utauwa
kitakuwa na nguvu kwa ajili ya ile kweli kuliko ufasaha mkuu sana
usioambatana na maisha mazuri. Tengeneza taa ya roho yako, na kuijaza
mafuta ya Roho. Tafuta kwake Kristo neema, yaani, ufahamu ulio wazi kama
ule, ambayo itakuwezesha kufanya kazi kwa mafanikio. Jifunze kwake
maana ya kuwashughulikia wale aliotoa uzima wake kwa ajili yao. Mtenda
kazi mwenye talanta nyingi anaweza kufanya kazi kidogo tu, isipokuwa
kama Kristo ameumbika ndani yake, tumaini na nguvu ya uzima. ----- 7BC
916. Utu uzima ulio mkamilifu na wenye tabia nzuri hauji kwa nasibu.
Ni matokeo ya kujenga tabia katika miaka ile ya mwanzo ya ujana, ni
kujizoeza [kuitii] sheria ya Mungu nyumbani. ----- YI, Mei 5, 1898.
Mungu anangoja kuwatia nguvu [kuwavuvia] vijana kwa uweza ule unaotoka
juu, ili wale wote wanaosimama chini ya bendera ile ya Yesu Kristo yenye
alama ya damu wapate kufanya kazi ile ya kuwaita, kuwaonya, na
kuwaongoza watu katika njia zile zilizo salama, na kuikita miguu ya
wengi juu ya ule Mwamba wa Kale. ----- Letter 66, 1894.
No comments:
Post a Comment