SOMO: NAMNA YA KUWA MWAMINIFUMUHUBIRI: MWINJILISTI MOFFATI Kuna
mambo mengine inatupasa kuomba kwa bidii sana fungu Yeremia 29:11-13.
Suala la maombi katika biblia lilikuwa ni la muhimu sana na mashujaa
wengi walishinda kwa kuomba kwa bidii sana na tena kwa imani.Mtu
ambaye haombi kwa bidii huyo hupata kwashakoo ya kiroho hata mambo yake
hayaendi vizuri,hata katika kuimarisha mahusiano yetu na Mungu ni
muhimu pia kusoma kwa bidii Mithali 4:13,2 Walawi 7:14-16.Mwinjilisti
Moffati ni moja wa Wainjilisti wanaotumiwa na Mungu katika suala la
injili,akitokea kanisa la Ushindi Sda Dsm aliweza kuanza Juma hili la
Uwakili siku ya Jumapili ya tarehe 4 Octoba,2015 na kukiwa na maombi kwa
wahitaji mbalimbali kila siku na hata leo siku ya jumatano ni kwa ajili
ya maombi ya kufunga na kuomba.Ili
ukubaliwe na Bwana toa sadaka iliyo kamilifu na ili ukubaliwe kwenye
ndoa,elimu,uchumba,maisha,mafanikio yoyote (Kutoka 25:1-2) Sadaka
inayokubalika na Bwana ni ile unayotoa kwa furaha na moyo wa upendo na
wala sio ya kunung'unika na lawama,ukitoa sadaka iliyokamilifu nyumba
italindwa na Bwana na weka imani yako kwenye vitendo. Kabla ya kuzaa toa
sadaka hata kama pia umepata mtoto mpeleke kwa Bwana na mtolee sadaka
ya shukrani.Uaminifu
wetu na uwe katika vitendo hasa kuwahurumia maskini Mithali 19:17
lakini pia kinyume cha hayo wale ambao ni masikini tukiwanyima
tulichonacho basi Bwana hatatusikia sisi Mithali 21:13.Penda kuwaza
chanya katika kazi ya Bwana kwani kazi hii inalipa na ombi la leo
lilikuwa ni Bwana afanye moyo wa kutoa sadaka na pia kuweza kutunza
sabato.>>SOMA ZAIDI HAPA<<
No comments:
Post a Comment