Kanisa la Kimara SDA kwa muonekano wa nje.
Na idara ya Mawasiliano-Kimara
Katika
moja ya njozi kubwa ya kanisa la Waadventista wasabato ni kupeleka
ujumbe kwa kila mtu,lakini ujumbe unakuwa rahisi pale tuu unapoanzia
kwenye familia zetu,hayo yamesemwa na moja ya Wazee wa Kanisa la Kimara
SDA,Mr.Tumaini Masige na akisisitiza kuwa Familia kama kitovu cha
uinjilisti,Roho mtakatifu anataka kuponya kwanza familia,na kuponywa
huku kutaleta matunda kama vile;-KUIMARIKA KIROHO,ambapo mtu kupata ujasiri wa kuitangaza kweli ya neno la Mungu na pia atakuwa na moyo wa kusoma maandiko matakatifu.
KUIMARIKA
KIUCHUMI-Mwanafamilia atajua jinsi gani aboreshe mapato yake kwa kuanza
na kumpa Mungu dhaka na sadaka,na hapo milango ya Mbinguni katika
maswala ya uchumi yatainuka.Huduma za familia lengo lake ni kuimarisha
familia kama kituo cha ufundishaji wa nidhamu na maadili ambayo ndio
msingi wa kuelekea kuwa raia mwema wa mbinguni.
Juma hili tutatafakari ni vyanzo gani vinavyosababisha Jina la Bwana lisiinuliwe,Dan 4:1
*******KARIBU UJUMUIKE NASI********
No comments:
Post a Comment