��Israeli
ni taifa ambalo Mungu alilipendelea, kwa kulifanya taifa teule kati ya
mataifa mengine. Walipoamua kumuacha Mungu na kuanza kuishi maisha ya
dhambi, Mungu naye aliwaacha, wakaingia katika maisha ya laana,
wakapigwa kwa magonjwa, njaa na mwishowe kutekwa na kuteswa, wakiishi maisha ya dhiki utumwani.
��Kwa
miaka mingi wakaishi maisha ya mateso na kudharauliwa. Hatimaye Mungu
aliye mwingi wa rehema, akawakumbuka, akawatoa katika mikono ya watesi,
akawaponya magonjwa na jeraha zao zote. Wakainuliwa kutoka katika shimo
la uharibifu hadi mlima wa Baraka.
��Kama
ilivyokuwa kwa taifa la Israeli ndivyo ilivyo katika kizazi chetu,
kadri uovu unavyozidi duniani ndivyo Watoto, Vijana na Wazee,
wanavyozidi kujeruhiwa na maisha. Watu wa dini na wasio na dini, maskini
kwa matajiri, wasomi kwa wasio wasomi, wenye vyeo na wasio na vyeo,
taratibu lakini kwa uhakika, wanakutana na mishare ya maisha kwa namna
tofauti.
��Tunashuhudia
matajiri na warembo wakioza vitandani kwa cancer, visukari, ukimwi,
kupooza, huku wengine wakihaha kutafuta vi senti wapate kipande cha
mhogo, huku vilio vya mabinti na wavulana waliotapeliwa na wachumba
'FAKE' vikizidi kuongezeka baada ya kubwagwa, miaka nayo ikichanja mbuga
bila huruma. Wazee nao wakichechemea na ndoa zilizo ndoano kama sio
kuachana au kulala na usiniguse. Wenye vyeo wakilala makuburini kulinda
vyeo, hata hivyo wanaondolewa kwa nguvu, vilio na laana vinasikika kila
kona.
�� Wapendwa;
Japo kuna utusitusi mkubwa namna hii katika kizazi hiki; bado REHEMA za
Mungu zingalipo, haijalishi umeumizwa na kujeruhiwa kiasi gani;
Haijalishi umedharauliwa na kubezwa kiasi gani; Bila kujali changamoto
imedumu muda mrefu na ukaamini haiwezekani; Leo Bwana wa Majeshi Mfalme
wa Wafalme anasema - INAWEZEKANA NA ATAKUPONYA.
��Amini
tu, huu ni wakati wa kuinuliwa na kupokea Baraka za Bwana sawasawa na
ahadi zake. Kama kuna kirusi chochote cha Dhambi, kitakachokutenga na
Upendo wa Mungu, amua kukiacha, hakuna dhambi yenye faida wala shetani
ana jipya, ni mitego na mishale ileile kila siku, mwambie shetani leo
Bye byeeee. USHINDI KWA DAMU YA YESU NI HAKIKA.
WEMA WA MUNGU UKAWAZUNGUKE DAIMA NA MUWE NA AMANI NA BARAKA TELE.
Na: Eliezer Mwangosi - Tel. 0767210299. Email: eliezer.mwangosi@yahoo.com.
No comments:
Post a Comment