(Kwanini wajane ni wengi kuliko wagane??)
1. Umri mdogo wa kikomo cha maisha “life expectancy” – Kama unafahamu hili jambo linaloitwa “life expectancy” utakubaliana na mimi kwamba umri wa mwanaume wa kuishi ni mdogo sana ukilinganisha na mke wake, hususani kusini mwa jangwa la sahara. Kwa hiyo wanawake wanapewa nafasi kubwa ya kuishi muda mrefu kuliko waume zao.
1. Umri mdogo wa kikomo cha maisha “life expectancy” – Kama unafahamu hili jambo linaloitwa “life expectancy” utakubaliana na mimi kwamba umri wa mwanaume wa kuishi ni mdogo sana ukilinganisha na mke wake, hususani kusini mwa jangwa la sahara. Kwa hiyo wanawake wanapewa nafasi kubwa ya kuishi muda mrefu kuliko waume zao.
2. Ugumu katika kufunguka – Utakubaliana
na mimi kwamba wanaume ni wagumu sana ten asana kufunguka na
kushirikisha mambo yao, wao wako tayari wafe na tai shingoni wakijifanya
hawaumii au hawasikii shida. Mkiwa na ishu kwenye ndo mkaitwa sehemu
muyaongee yeye kamwe hamumpati, anakwambia mambo yetu tutasuluhisha
wenyewe wakati ndani yanamla na kummaliza. Na kwa mtaji huu watakufa
sana tu
3. Ugumu katika kusamehe –
Kusamehe sio tu kwa faida ya anayesamehewa bali pia kwa afya yenyewe
unayesamehe. Mzigo unaotokana na kusamehe hutuumiza sana mioyo yetu,
hata kama mara nyingine tunajifanya hatuna shida yeyote. Unaposamehe
unaachilia mzigo mkubwa, wanaume wao ni wagumu sna kusamehe. Wako tayari
wakubebe moyoni miaka, na tena watakukumbusha uchungu wao kila
wanapokuona. Hii inawala sana bila wao kujua.
4. Tabia hatarishi – Wanaume
wengi kwenye ndoa ndio wanaoongoza kushiriki tabia hatarishi kama vile
ulevi, anasa, ngono holela na hii huwaweka karibu zaidi na jeneza kuliko
wake zao waliowaacha nyumbani wakiwadanganya kuwa wako mkutanoni
mkoani.
5. Ugumu katika kujali afya –
Ni rahisi sana mwanaume akajisikia vibaya lakini asiende hospitalini
kuangalia afya, hata pale anapohimizwa kwenda bado anaweza kukwepa au
kubisha au hata kusema kuwa ameshakwenda au ameshakunywa dawa kumbe
mwongo. Wako pia ambao wanaweza kupewa dawa na wasizitumie.
6. Msongo wa mawazo –
Wanaume ndio wabebaji wakubwa wa shehena za msongo wa mawazo “stress”
ingawa kwa nje wanajitahisi sana kuonyesha kuwa mambo yako shwari wakati
wanatafunwa ndani. Kaulize hospitalini, wanaokufa kwa presha ya kupanda
au ya kushuka, stroke, kusimama kwa moyo, kupasuka kwa mishipa ya damu,
matatizo ya mifupa, au kuumwa sana kichwa, halafu uliza ni jinsia gani.
Maisha sio mabaya kiasi hicho, maisha ni mazuri. Chagua kuishi – Chris Mauki
No comments:
Post a Comment