Kama haukumfahamu marehemu enzi za uhai wake, wasifu wake huu hapa...

 KUZALIWA
  • Tarehe 25-05-1952, Majita, wilaya ya Musoma Vijijini, Mkoa wa Mara.
ELIMU
  • 1962-1968 - I-VII, Shule ya msingi Nyakahonja mkoani Mwanza
  • 1969-1972 - I-IV, Shule ya Sekondari Kigoma.
  • 1973-1974 - V-VI, Shule ya Sekondari Mkwawa.
  • 1976-1979 - Shahada ya kwanza kitivo cha Ardhi, Chuo kikuu cha Dar es Salaam
  • Baadaye Alijiendeleza masomo ya elimu ya juu zaidi katika chuo kikuu cha Kaisaslaughten nchini Ujerumani katika masuala ya usanifu majengo.
AJIRA
  • Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kama afisa mipango Miji (Town Planning Officer)
  • Baadaye alijiajiri kama mshauri mwelekezi katika masuala ya usanifu majengokazi ambayo alikuwa akiifanya hadi mauti ilipomkuta.
  • Baadhi ya kazi kubwa ambazo marehemu alizifanya ni pamoja na Usanifu majengo ya sasa ya makanisa ya Waadventista wasabato Ushindi na Mwananyamala, Jengo la kituo cha Redio na Runinga ya Morning Star.
NDOA NA FAMILIA
  • Alifunga ndoa na mama Monica Jigabha na wamefanikiwa kupata watoto watatu (3), Wakiume 1 na Wakike 2 na mjukuu 1 wa kiume.
MAISHA YA KIROHO
  • Alibatizwa mwaka 1999 katika kundi la Mikocheni B, ambalo kwa kipindi hicho lilikuwa chini ya usimamizi wa Kanisa la Waadventista wasabato Mwenge.
MARADHI
  • Alianza kuugua mnamo Julai 15, 2015 ugonjwa wa Shinikizo la damu (BP), Kisukari na homa ya ini na kwa nyakati tofauti alipata matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili hadi alipofariki dunia Jumapili ya Tarehe 23-08-2015 saa 11 jioni.
BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIBARIKIWE.

No comments:

Post a Comment