KAMBI LA MTAA WA KIMARA, SOMO LA IBADA KWA MCHANA WA LEO "KUSONGA MBELE KWA IMANI"

Imani ni kuwa na hakika na mambo yatarajiwayo na bayana na mambo yasiyoonekana,katika kambi la mtaa wa Kimara leo siku ya ijumaa,somo la mchana huu limetolewa na Mchungaji Robson Nkoko ambaye amekuwa mhutubu mkuu katika kambi hili akitokea Mbeya akiwa ni Mwenyekiti wa Konferensi ya Nyanda za juu kusini mwa Tanzania(SHC).
Mungu ni mweza wa yote na katika hili,Mchungaji Nkoko ametoa wito kwa waumini kutohofia chochote chini dunia hii kwa ni Mungu yu pamoja nasi hajashindwa wala hatashindwa,alishinda wakati wa Musa akiwaongoza wana wa Israel toka Misri kwenda nchi ya ahadi na Mungu akimwagiza Musa kuwa awaambie wana wa Israel wasonge mbele.


Mchungaji Robson Nkoko akisema jambo katika mkutano wa kambi la mtaa wa Kimara ni katika viwanja vya kanisa la King'ongo jijini Dar Es Salaam.

No comments:

Post a Comment