Sehemu ya Kwanza: Katika Agano la Kale
Baada ya Kumaliza uumbaji wake Biblia katika Kitabu cha Mwanzo 2:1-3
“Basi
mbingu na nchi zikamalizika, na jeshi lake lote. Na siku ya saba Mungu
akamaliza kazi yake yote aliyoifanya; akastarehe siku ya saba. Akaacha
kufanya kazi yake yote aliyoifanya. Mungu akaibarikia siku ya saba,
akaitakasa kwa sababu katika siku hiyo Mungu alistarehe, akaacha kufanya
kazi yake yote aliyoiumba na kuifanya”
Hapa kuna mambo muhimu ya Kuzingatia.
Jambo
la Kwana ni kwamba, Mungu alistarehe katika Siku ya Saba baada ya Siku
sita za Uumbaji. Hapa hatuambiwi kwamba Mungu alipumzika katika siku ya
Saba kuashiria kwamba alichoka. Kwa hakika Mungu wetu hachoki, Biblia
inatuambia “Je wew hukujua?, Hukusikia? Yeye Mungu wa Milele, Bwana.
Muumba wa miisho ya dunia, hazimii wala hachoki; akili zake
hazichunguziki” Isaya 40:28. Kitendo cha Kustarehe hakinamaana kwamba
Mungu alikuwa ametulia tuli bila kazi yoyote. Yesu anasema “..Baba yangu
anatenda kazi hata sasa. Nami ninatenda kazi Yohana 5:17. Kazi
inayoyotajwa hapo kwamba Mungu aliiacha ni Kazi ya Uumbaji., “aakaacha
kufanya kazi yake yote aliyoiumba na kuifanya” Mzo2:3. Hivyo basi ni
sahihi kusema Kitendo cha Mungu kustarehe kinaashiria kufurahia Kazi
yake ya uumbaji kwani neno linasema, “Mungu akaona kila kitu
alichokifanya, na tazama ni chema sana” Mwanzo 1:30. Jambo hili
laashiria kufurahishwa na kazi aliyokuwa akiifanya.
Jambo
la pili Mungu aliibariki siku ya Saba Neno kubariki laashilia upendeleo
fulani Mungu alioufanya kwa ajili ya siku hii ya saba. Mara kwa mara
tunaona Baraka zikitamkwa kwa watu katika biblia, ni jambo la kushangaza
kwamba Mungu anatamka baraka kwa siku ya saba. Hii ni lazima mtu
anaposikia jambo hili ni vizuri azingatie na kujiuliza kwa nini? Bila
shaka ni kwa sababu Mungu alikusudia kuifanya kuwa ni siku ya pekee siku
ya Saba
Jambo
la Tatu, Mungu aliitakasa. Neno hili kutakasa ni neno la Kidini,
kutakasa ni kuweka kando kwa matumizi maalumu kwa maswala ya kidini tuu.
Hivyo hapa yaonyesha kuwa Siku ya Saba ilitengwa kwa ajili ya matumizi,
matakatifu
Tunajua
kwamba, wakati wa uumabaji, Mungu aliweka Jua, Mwezi na Nyota na
Makusudi ya kuumba vitu hivyi Mungu anasema “nayo iwe ndiyo dalili, na
majira na siku na miaka;” Mwanzo 1:14. Kisha Mungu kwa ufahamu
aliowapatia wanadamu, waliweza kufanya mahesabu haya, Mwaka mmoja una
siku 360 au 365 na Robo, (hii ni sawa na miezi 12), Siku moja ina Masaa
24, Saa moja ina dakika 60, dakika moja ina sekunde 60. Yaonekana kwamba
zamani kabisa kabla hata ya maendeleo ya sayansi na uvumbuzi wa
Telescope tayari kulikuwa na elimu hii ya uajimu, mfano Wababeli
walikuwa na elimu hii ya unajimu, Mwanahistoria Morey katika kitabuchake
Ancient People ukurasa wa 26,27 anasema “Nabu-rimannus na Kidinnu,
wanajimu wa kibabeli mashuhuri walitengeneza jedwali la mwenendo wa jua
kwa kuhusiana na mwezi na waliwenza pia kupiga mahesabu ya mzunguko wa
dunia na kupima ulefu wa mwaka na kupata kuwa ni siku 365 na masaa 6 na
dakika 15 na sekunde 41”
Hivyo
twaona kuwa ni wasi mwanadamu anajua sababu za majira yote kama ilivyo
katika kalenda zetu leo, ni jambo moja tu ambalo mwanadamu hajui sababu
yake, KWANINI JUMA MOJA LINA SIKU SABA? Hii ni kwa sababu, jambo la wiki
kuwa na siku saba linatoka kwa Mungu pekee na siyo kwa Mwana damu.
Mwanzo
wa wiki moja yenye siku saba tunaupata pekee katika kitabu cha Mwanzo
sura ya kwaza. MUNGU ALIUMBA MBINGU NA NCHI KWA SIKU 7. Hatuambiwi
popote katika historia kwamba Mwanadamu aliwahi kupanga utaratibu wa
siku 7 za wiki. Kwa nini isiwe siku 8, siku 9 siku 10 au siku 11. Ni kwa
sababu Mungu mwenyekwe alifanya kazi siku 6 akastarehe siku ya 7. Hivyo
kama kunajambo pekee ambalo mwanadamu hajasahau toka kwa Muumba wake ni
wiki moja yenye siku 7
Niwazi
kwamba ikiwa siku saba (7) hazijasahaulika katika historia, tunaweza
kuhitimisha kuwa mwanadamu amekuwa akitunza siku ya saba kama siku ya
mapumziko, siku ya kustarehe na kuacha kazi zake zote kama Mungu
alivyofanya, lakini pia kama siku takatifu iliyotakaswa na Bwana na
kuwekwa kwa ajili ya matumizi matakatifu. Hii ni kwasababu Jambo hili
liliamuliwa na Mungu tokea uumbaji, na wale wote walioshikamana na
Bwana, hatunashaka kwamba walitimiza Jambo hili
KUSAHAULIKA KWA SIKU YA SABA KAMA SIKU TAKATIFU YA IBADA
Kwakuwa
Biblia inatuambia juu ya kuongezeka kwa maasi duniani katika Kitabu cha
Mwanzo sura ya 6 na hatimaye kughariishwa. Ni wazi kwamba kwa sababu ya
uovu huo wanadamu hawakumuheshimu Mungu wala kumwabudu. Ndiyo maana
biblia inasema, “Bwana akaona yakuwa maovu ya mwanadamu ni makubwa
duniani, na kwamba kila kusudi analowaza moyoni mwake, ni baya tu siku
zote” Mzo 6:5. Usitegemee kuwa katika hali hii kulikuwa na jambo lolote
la ibada. Hivyo ni katika wakati huu ambapo siku ya saba kama takatifu
kwa Bwana na siku ya ibada ilisahaulika usoni pa dunia.
BWANA AREJESHA SIKU YA SABA KAMA SIKU TAKATIFU YA IBADA.
Mungu
alipokuwa akiwaongoza Israeli kutoka Misri kwenda kanaani,
wakiwajangwani na Mungu Mwenyewe amewakusudia kuwa Taifa takatifu,
warudishe ufahamu wa Mungu kwa wakazi wa Dunia, alianza kurejesha kweli
zote zilizopotea na kuanza kuwafundisha tena kuitunza takatifu siku ya
Saba.
“Akawaambia ndilo neno alilonena Bwana, kesho ni Starehe takatifu, sabato takatifu kwa Bwana…”Mwanzo 16:23
Hapa
tuwaona kuwa ni Mungu mwenyewe anayeanza kuwafundisha juu ya siku hii ya
saba. Ni wazi kuwa walikuwa hawaifahamu baada ya kuwa wamekaa utumwani
Misri kwa miaka 430. Mungu ndiye mwanzilishi wa Sabato, naye ndiye
Mwalimu wetu, hapa tunaona anaanza kuwafundisha watu wake juu ya
Utunzaji wa siku ya Sabato kama siku takatifu kwa Bwana. Zingatia hapa
neno linasema “ ni sabato takatifu kwa Bwana”, maana yake ni kwamba, ni
siku ya kuitumiza kwa ajili ya Bwana tuu, Kufanya mambo ya ibada,
kumwabudu Mungu.
Mungu
pia alimwagiza Munsa akisema “Mtafanya kazi siku sita, lakini siku ya
saba ni Sabato ya kustarehe kabisa, Kusanyiko takatifu,, msifanye kazi
ya namna yoyote, ni SABATO KWA BWANA, katika makao yenu yote.” Lawi
23:3. Kumbe siku ya Sabato imetajwa hapa wazi kuwa ni siku ya Ibada.
Wakati
Waisraeli wakiwa jangwani Mungu aliwapatia Maagizo mengi ikiwa ni
pamoja na utaratibu wa ibada na huduma katika hema ya Kukutania (Kutoka
25-36; Lawi 1-10). Hii ilikuwa pamoja na utaratibu mzima wa jinsi ya
kuondoa dhambi katika wana wa Israel, Kulikuwa na Sadaka za amani, na
Sadaka za ondoleo la dhambi zilizoletwa hemani na baadaye katika hekalu.
Mahusiano ya wao kwa wao kama jamii ya watu wa Mungu (Lawi 18-19).
Usafi na masuala ya Afya kwa Taifa la Mungu. (Lawi 11; Kumb. 23:12-14).
Maagizo haya yote, Bwana alimwambia Musa ayaandike katika kitabu cha
Torati, na yatunzwe pembeni mwa Sanduku la agano. (Kumb. 31:26). Baadhi
ya maagizo haya, mfano sadaka ya ondoleo la dhambi, yalikuwa kivuli cha
Mambo yajao, Sadaka kamili ya ondoleo la dhambi kwa ulimwengu
mzima—“Mwana kondoo wa mungu aichukuaye dhambi ya ulimwengu” (Yohana
1:29; Waebrania sura ya 7-10)
Baadaye
Mungu Mwenyewe alishuka katika Mlima wa Sinai na Kuwapatia maagizo watu
wake, maagizo ambayo ndiyo yangekuwa msingi wa maadili na uchaji Mungu
wa dhati, AMRI 10 ZA MUNGU. Neno linasema “Bwana akamwambia Musa, tazama
mimi naja kwako katika wingu zito ili watu hawa wasikie nitakaposema
nawe, nao wapate kukuamini wewe nawe hata milele. Musa akamwambia Bwana
hayo maneno ya watu. Bwana akamwambia Musa, enenda kwa watu hawa,
ukawatakase leo a kesho, wakazifue nguo zao. Wawe tayari kwa siku ya
tatu; maana siku ya tatu Bwana atashuka katika mlima wa Sinai machoni pa
watu hawa wote” (Kut. 19:9-11), “Bwana akaushukia mlima, juu ya kilele
cha mlima…” Kut. 19:20
Hapa
neno la Mungu lina weka wazi tofauti ya maagizo yote aliyotoa Mungu kwa
watu wake. Wakati ambapo mambo mengine yote Mungu alimwagiza Musa
ayapeleke kwa watu na baadaye kumwagiza ayaandike katika kitabu cha
Torati, Siyo hivyo kwa amri 10 za Mungu. Hizi zilikuwa ni takatifu mno,
kiasi cha kutomruhusu Mwana damu kuzinena wala kuziandika. Ilibidi Mungu
mwenyewe ashuke kusema na watu. Na kasha baadaye yeye mwenyewe
kuziandika katika mbao za Mawe. (Kut. 24:12, 31:18)
Katika amri hizo tunapata maranyingine Munfu akisisitiza juu ya siku ya Saba kama siku takatifu kwa Bwana
“Ikumbuke
siku ya sabato uitakase…” Bwana anaanza kwa kusema “Ikumbuke”, hii
inaashiria kwamba ilikuwa imesahaulika, la sivyo itakumbukwaje kitu
ambacho hakikuwepo? “siku sita fanya kazi, utende mambo yakeo yot;
lakini siku ya saba, ni sabato ya Bwana, Mungu wako, siku hiyo usifanye
kati yoyote….” Kasha Bwana anaeleza sababu ya kutoa amri hii “maana kwa
siku sita, BWANA alifanya mvingu na nchi, na bahari na vyote vilivyomo,
akastarehe siku ya saba; kwa hiyo BWNA akaibarikia siku ya sabato
akaitakasa.” Kut. 20:8-11
Zingatia
hapa kwamba sababu ya kukumbuka siku ya saba inaelezewa na Mungu
mwenyewe kuwa ni kukumbuka kuwa Mungu aliumba kwa siku sita, nay eye
mwenyewe akatoa mfano w kustarehe katika siku hiyo, na kuitakasa, yaani
kuifanya kwa ajili ya matumizi matakatifu tuu.
Hapa
tuwezi kusema sabato ilitolewa kwa Waisrael tu, kwani sababu za kutolewa
kwake zinavuka mipaka ya Israeli zamani wakati wa uumbaji. Kabla
halijakuweko taifa la Israel
Mungu
alitarajia kuwa, watu wa Mataifa yote wangemwabudu yeye na kuitunza
sabato. Anasema hivyo katika Isaya 56:5-7 “Na wageni walioambatana na
Bwana ili kumhudumu, na kulipenda jina la Bwana, kuwa watumishi wake;
kila aishikaye Sabato asiivunje, na kulishika sana agano langu;
nitawaleta hao nao hata mlima wangu mtakatifu, na kuwafurahisha katika
nyumba yangu ya sala”
Ona hapa kuwa Sabato inahusishwa na Nyumba ya Sala kuonyesha kuwa ilikuwa siku ya Ibada kote katika agano la Kale.
Tunaweza
kuhitimisha kwa ujasili kwamba Mungu aliiweka siku ya saba kuwa sabato
takatifu ya ibada kwa Mungu. Katika sikuhiyo tuaacha kazi zote na
kukumbuka kuwa Yeye ndiye muumbaji wetu. Mungu alikusudia kuwa kupitia
utunzaji wa sabato watu wasingeweza kumsahao yeye kuwa muumbaji na
kugeukia hadithi za uongo za uibukaji(Evolution). Swala la utunzaji wa
sabato lilifanywa kuwa ni swala la kuonyesha utii kwa Mungu muumbaji na
kutambua kuwa Mungu ndiye anayetawala juu yetu.
NA https://loudcrymediaministries.wordpress.com
No comments:
Post a Comment