USICHOKIFAHAMU JUU YA KITABU CHA "PENDO LISILO KIFANI" SEHEMU YA KWANZA


Miongoni mwa maswali yanayoulizwa na wengi leo ni juu ya hali ya kusikitisha ya Dunia yetu. Je tumefikaje huko? Hali hii ya Uovu ilianzaje? Wako wengi waliojaribu kutoa majibu lakini yaliyojengwa katika Sayansi na Falsafa. Hata hivyo yanatofautiana sana na kushindwa kukidhi hasa hitaji lenyewe, na kuibua swali jipya kabisa; Ni wapi basi tutapata ukweli halisi?

Kitabu cha Pendo Lisilo Kifani, ambacho kimsingi kimejengwa katika Maandiko Matakatifu, yaani Biblia, kimesheheni majibu ya kweli halisi ya maswali yanayohusiana na mstakabali wako na wa Dunia hii.

Mwandishi, kwa karama ya Mungu, anaeleza juu ya Mwanzo ambao ulikuwa mkamilifu usio na kasoro au dhambi, maelezo ambayo kwa hakika yanagusa sana hisia.

Utashangaa kusoma jinsi dunia hii ilivyokuwa mara baada ya kuumbwa, mwanadamu wa kwanza akikutana na kuzungumza na Mungu katika mazingira mwanana kabisa, yenye maua, mito, wanyama, na ndege wa namna namna.

Ile siri ya Uovu kuibuka ndani ya kiumbe mkamilifu imejadiliwa kwa kina.  Hata hivyo kinachogusa zaidi ni jinsi Mungu alivyofanya hima kuwatahadharisha Adamu na Hawa ili wasiingie dhambi, na zaidi sana kile alichofanya kwa gharama kubwa kuhakikisha kwamba njia inapatikana ya kumtoa Mwanadamu katika dhambi na athari zake na kuikomesha taabu kabisa.  Uajabu wa Pendo lisilo kifani uliodhihirishwa katika kifo cha Yesu, ndio hasa kiini cha kitabu hiki, utafurahi na kunufaika sana kusoma kisa hiki cha ajabu cha kumwokoa mwanadamu.


 Maelezo na
MchungajEzekiah Chaboma.
Meneja usambazaji wa vitabu  

Kanisa la waadventista wa Sabato, Union ya kusini mwa Tanzania.




No comments:

Post a Comment