SAMWEL MWAZINI: "Kinachonikera ni waimbaji kukosa nidhamu, kutafuta kushindana Zaidi ya Injili Kwanza"

Huyu ni Muimbaji, Mtunzi na Mwalimu wa nyimbo za injili nchini Tanzania. Amekuwa ni muimbaji mwenye mafanikio ya mapema na tunaamini bado ataendelea kuwa bora siku zinavyozidi kwenda. Amefanikiwa kupata tuzo ya muimbaji bora wa kiume, tuzo ambazo ziliandaliwa na kituo cha Runinga nchini Tanzania, Morning Star (MSTV).

Akikabidhiwa Tuzo ya Muimbaji bora wa Kiume
Tuzo ya "Glorious Music Award" aliyochukua
Tarehe kama ya leo anakumbuka siku yake ya kuzaliwa, hivyo tumeamua kumtafuta na kufanya naye mahojiano ili kuwapa nafasi wale waliokuwa hawamfahamu au kumfahamu kidogo wamfahamu kiundani.
Yafuatayo ni sehemu ya mazungumzo yetu, kati ya Injilileo (IL) na Samwel Mwazini (SM).

IL: Mambo vipi?
SM: Shwari kaka, Nambie...

IL: Hongera kwanza kwa kukumbuka siku yako ya kuzaliwa...
SM: Asante Sana brother

IL: Ilikuwa ni lini vileee...? 
SM: Ilikua Alhamis, 27 Jan 1994

IL: Wewe ni wangapi katika familia na mpo wangapi?
SM: Mimi ni firstborn (wa kwanza), Kati ya watoto 4, Wote wavulana

IL: Mzee anaitwa nani?
SM: Wilfred Jumanne Mwazini

IL: Nini siri yako katika uimbaji?
SM: Siri ni maombi, kuthubutu na mazoezi

IL: Una utofauti gani na waimbaji wengine uliwahi kuwaona au kukutana nao?
SM: Hilo ni swali gumu. Labda watu wanao niona ndo waseme

IL: Naomba nipate Historia yako ya uimbaji kwa ufupi...
SM: Nilianza kuimba nikiwa nyumbani na baba na mama tangu mdogo Sana. Niliipokua na miaka 6 nilianza kuimba Christ Messengers pale Ikizu High School ambayo ni choir ya staff at the same time nikawa naimba group na wanafunzi inaitwa Golden Singers. At the same time nilikua na group nyingine na rafiki zangu Wawili Masinde Mutabhi na Masatu. Niliendelea hivo hadi nilipofika darasa la Tano nikahamia Dar. Nikaanza kuimba kwaya ya kanisa la Kongowe Parapanda huku nikiwa na group yangu inayoitwa Soldiers of Christ ambayo iliundwa na mimi na wadogo zangu na rafiki zetu wengine. Lakini pia niliipokua Sekondari niliimba ASSA na TM music pia. Advance nilianza Kuwa kama solo artist hadi Sasa hapa nilipo. Kuna vikund pia kama Holy Reunion, Harmony Brothers na vingine ambayo nimeshiriki.
Akiwa katika kipindi cha Runinga ya Morning Star na mtangazaji Jacob Mang'ombe
IL: Uimbaji una asilimia ngapi katika maisha yako?
SM: Uimbaji Una almost 60 %

IL: Vipi kuhusu kunufaika na uimbaji wako, Je, hadi sasa umepata faida gani katika uimbaji hadi kuhitaji kuendelea siku hadi siku?
SM: Muziki umiongezea furaha na marafiki. Umenifanya nimjue Mungu pia. Kwa kipato bado

IL: Je, unaweza kupiga vyombo vya muziki na kusoma muziki?
SM: Yeah naweza kwa kiasi fulani, Piano na guitar bass na rhythm kidogo
Akiwa anapiga Gitaa na muimbaji mwenzake Barret Mapunda katika studio bora ya Vocapella
IL: Umefundisha kwaya na Vikundi gani hadi sasa?
SM: Duu, Nimefundisha kwaya ya Parapanda ambayo ni kwaya ya kanisa, Nimefundisha ASSA DAPWAZA, Soldiers of Christ, Holy Reunion, kwaya ya vijana Kongowe na saizi nafundisha Nyerere Campus Choir chuo kikuu cha Dar es Salaam.

IL: Kwa Tanzania unampenda muimbaji gani na unatamani pia ufikie mafanikio yake aliyopata katika uimbaji?
 SM: Napenda Baraka Mbega na Angel Magoti
Samwel Mwazini akiwa na muimbaji mwenzie Angel Magoti
 IL: Nje ya nchi ya Tanzania je, ni muimbaji gani ambaye anakufanya ufanye bidii siku hadi siku...?
SM: Nje ya nchi ni Guy Penrod
Guy Penrod
IL: Kuna msaada gani katika uimbaji unahitaji kutoka kwa watu wengine ili ufikie mafanikio uliyojiwekea kimuziki?
SM: Msaada ni support ya maombi na ushirikiano wa kila namna. Lakini pia ushauri

IL: Nini kina kukera katika tasnia nzima ya muziki wa Injili?
SM: Kinachonikera ni waimbaji kukosa nidhamu kutafuta kushindana Zaidi ya Injili Kwanza. Lakini pia waimbaji wengi tuko shalow ki maandiko hatusomi, Hii ni Hatar kwa afya zetu kiroho.

IL: Mungu akikupa nafasi, unatamani familia ya watoto wangapi na je, ni tamanio lako mama yao na watoto kuwa waimbaji kama wewe?
SM: 4 childrens. Wakiwa waimbaji ntafurahi pia

IL: Tumtegemee Samwel yupi miaka mitano ijayo katika uimbaji?
SM: Natamani kufanya Muziki WA kikristo ambao utamgusa kila mtu ulimwenguni. So naomba ushirikiano Wenu Sana na maombi

IL: Unaweza kukumbuka hadi leo, umeandika nyimbo ngapi?
SM: Duu sikumbuki, Ila ni Kati ya 30 had 50.

IL: Tabia ya baadhi ya walimu kuiba nyimbo za wenzao unaisemaje na je imewahi kukukuta labda wewe kuiba au kuibiwa?
SM: Hahaha hiyo ipo

IL: Vipi, kuhusu muziki wetu wa Injili, ubora unapanda au unashuka?
SM: Ubora wa Muziki unapanda siku hadi siku. Ila tuboreshe jumbe Za nyimbo 

IL: Je, waandaaji wa muziki wananafasi ya kukuza muziki huu, na unatoa wito gani kwao? 
SM: Waaandaaji wa Muziki wanakazi Kubwa kuhakikisha hawatoi kazi za hovyo. Kama Muimbaji hajajiandaa vizuri msaidieni ili Kazi iwe bora. Tusifanye bora liende

IL: Kwakuwa unakumbuka siku yako ya kuzaliwa bila shaka una watu pia wa kuwashukuru...naomba nikupe nafasi hiyo tafadhali...
SM: Aisee namshukuru Mungu Kwanza, baba yangu na wanafamilia wengine na marafiki wote kwa kushiriki Nami siku hii

IL: Neno lako la mwisho kwa wapenzi na mashabiki wako ni lipi...?
SM: Neno LA mwisho ni hili. MUNGU TUFUNDISHE KUHESABU SIKU ZETU TUTENDE YAKUPENDEZAYO ILI TUFAE KWA UFALME WAKO

IL: Asante kwa muda wako Sam, nikutakie maisha marefu na mema...Mungu akubariki sana, HAPPY BIRTHDAY.     

No comments:

Post a Comment