UNAJITAMBUA?
NENO LA MUNGU KUPITIA MWINJILISTI JOSEPH MALIMA KABUCHE
YONA 1:8-9 ; 2PETRO 2:9
Hebu jitazame mwenyewe,jitathmini mwenyewe,kimtazamo,kimavazi,kiimani,
kiutendaji kiroho katika uhalisia huo hebu jiulize swali hili, wewe,
mimi ni nani?
Kujijtambua maishani ni jambo la muhimu sana. Ukijitambua utajua uwezo
na udhaifu wako mwenyewe hivyo utafanya maamuzi sahihi baada ya
kujitambua.
Ni vizuri kutambua kuwa wewe ni mwanadamu, tena ni mwanamke au
mwanamume; lakini kutambua wewe ni nani kwa jamii yako kama mwanamume au
mwanamke ni muhimu sana.
Ukijitambua mwenyewe, utajitambulisha hivyo katika jamii inayokuzunguka.
Wengi wetu hatujitambui hivyo hatujitambulishi vyema katika jamii
tunamoishi. Wakristo wengi hatujitambui binafsi sisi ni nani hivyo
hatujitambulishi hivyo katika jamii.
Wakati Fulani Ibrahimu katika biblia hakujitambua akaogopa watu
akamtambulisha Mkewe kama dada yake. Upo wakati katika biblia Eliya
hakujitambua akakimbia mbele ya mwanamke fedhuli Yezebeli. Lakini je!
Katika biblia Petro alimkana YESU mara tatu tena mbele ya vijakazi tu.
Mimi na wewe tumeitwa kuwa watu wa pekee katika ulimwengu huu kwani sisi ni:-
• UZAO MTEULE
• UKUHANI WA KIFALME
• TAIFA TAKATIFU
• WATU WA MILKI YA MUNGU
Twapaswa kuzitangaza fadhili za yeye(Kristo) aliyetuita tutoke gizani(dhambini). Tafakari kisa cha binti mateka katika biblia 2wafalme 5:1-10. Binti huyu alikuwa:-
Mateka, alifanya kazi kwa uaminifu kwani alimtegemea Mungu na kumwamini na aliwaamini manabii wake.Aliaminika pale nyumbani hivyo ujumbe wake pia uliaminika. Alijua Mungu ni mponyaji kupitia Nabii wake na hivyo hakuwa na mashaka.
WEWE,MIMI NI NANI, TUNAITWA TUJITAMBUE ILI TUWE NURU KWA ULIMWENGU

Bibi Neema Majula(Masterguide) -miaka 78 |
Mshauri wa Vijana Masterguide-Charles Masolwa Malunde |
Mlee mtoto katika njia impasayo |
Masterguide na Mwinjilisti Joseph Malima Kabuche |
No comments:
Post a Comment