MAGUGU SDA CHURCH
  • Home
  • Audio
  • Habari
  • KWAYA
  • LESSON
  • MAHUBIRI
  • VIDEO

NEWS | MKUTANO MKUU WA KANISA LA WAADVENTISTA WASABATO 2015 WAENDELEA SAN ANTONIO

 Baadhi ya Viongozi wa Union 35 zilizopitishwa jana Mkutano Mkuu wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato Duniani umeingia katika siku ya pili hii leo ambapo maelfu ya waumini wameendelea kuhudhuria mkutano huo unaofanyika San Antonio Texas huko Marekani. Mkutano huo ambao ni wa 60 toka kuanzishwa kwa mikutano mikuu ya kanisa hilo ulimwenguni umeanza rasmi hapo jana kwa mapokezi maalumu wa Unioni mpya 35 kutoka sehemu mbalimbali duniani ambapo Unioni ya kusini mwa Tanzania,Union ya kaskazini mwa Tanzania na Unioni nne za Divisheni ya Africa Mashariki na Kati ni miongoni mwa union hizo zilizopokelewa. Katika siku ya kwanza ya mkutano huo umehitimishwa kwa kuchagua kamati ya uchaguzi yenye wajumbe zaidi ya 250 huku Tanzania ikiwakilishwa na Mwenyekiti wa Union ya Kusini mwa Tanzania Magulilo Mwakalonge na Mwenykiti wa Union ya Kaskazin mwa Tanzania Mch Godwin Lekundayo na mshiriki mmoja ambapo mapema hii leo kamati hiyo ilianza kazi yake. Mkutano mkuu wa kanisa la Wadventista Wa Sabato Ulimwenguni umeanza rasmi hapo jana na unatarajiwa kuhitimishwa Julai 11 mwaka huu kauli mbiu ya mkutano huo ni Inuka uangaze Yesu anakuja.


at July 05, 2015
Email ThisBlogThis!Share to XShare to FacebookShare to Pinterest
Labels: Habari

No comments:

Post a Comment

Newer Post Older Post Home
Subscribe to: Post Comments (Atom)

Search This Blog

About Me

magugu
View my complete profile

TOVUTI RAFIKI

  • MTANGAZAJI
    UHAMIAJI WA KIMATAIFA WAONGEZEKA KWA KASI - *Takwimu za hivi karibuni zinaonesha kuwa uhamiaji wa kimataifa umeongezeka kwa kasi katika nchi nyingi zilizoendelea na zilizoko katika Umoja wa Ushi...
    1 hour ago
  • Lesoni ya Kiswahili
    Somo la 12: Mungu ni Mwaminifu - *Somo limetafsiriwa na Mgune Masatu* *(Joshua 23)* Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2025, Bruce N. Cameron, J.D. Kwa wanaotumia lugha ...
    5 days ago
  • INJILILEO BLOG
    PICHA ZA MATUKIO SABATO YA WAGENI KANISA LA WAADVENTISTA WASABATO KIMANGA -
    8 years ago

Blog Archive

Labels

  • Audio
  • Habari
  • Kwaya
  • Lesson
  • Mahubiri
  • Video

Report Abuse

Blog Archive

VIDEO OF THE MONTH

Featured Posts

FOLLOW ME ON INSTAGRAM

Instagram

WATEMBELEAJI

Awesome Inc. theme. Powered by Blogger.