Japo hali za vijana wengi kiroho ni tete, bado Mungu anatoa msisitizo kwa Vijana kuwa na sifa zifuatazo.
1. WANA NGUVU: Nguvu za ujana hazipo kwa ajili ya kupigana Masumbwi, wala kuzungusha viuno kwenye muziki wa dansi, sio nguvu za kuvunja majumba na kupora Mali za watu, bali nguvu za Ujana zipo kwa ajili kufanya kazi halali za kujikimu na kuendeleza kazi ya Mungu.
2. NENO LA MUNGU LINAKAA NDANI YAO: Hapa ndipo pana UTAPELI kwa Vijana wengi, utasikia vijana wakichangia mijadala ya biblia, wanasoma na kukalili mafugu ya biblia, lakini mioyo yao Imejaa uchafu wa mawazo ya uzinifu na uasherati, muda mwingi wanashinda wakivinjari kwenye mitandao, wakilisha bongo zao maneno ya Mapenzi hadi hawawezi tena kujizuia. Nadharia ya neno la Mungu ni kubwa kuliko vitendo, Neno halina nafasi ndani yao, neno liko midomoni sio moyoni yanakotoka maamuzi.
3. WAMEMSHINDA MUOVU: Kujiita Mtu wa Mungu, Muislam au Mkristo, huku umezama katika mambo ya Dunia, ni kushindwa na muovu. Ni sawa na Kipofu anayehisi kuona huku ametobolewa macho, ndio maana utakuta Kijana anayejiita mshika dini anadai tendo la Ngono kabla ya kufunga Ndoa, akijifariji kuwa eti hawezi kuuziwa mbuzi kwenye Gunia, hizo ni lugha za mapepo ya Ngono, kuhalalisha uzinifu.
Ulevi wa madawa, pombe, bangi, wizi, uvivu, kushinda kwenye pool table, kamali na utapeli, uongo, uzushi, ukahaba, kutembea nusu uchi, kuwa kidumu cha mume au mke wa mtu nk, hayo yote ni maisha ya kushindwa kabisa na yule muovu, ni kipofu asiyeona ambaye mwisho wa safari yake ni Kutumbukia shimoni.
NEEMA YA MUNGU IKAWE JUU YENU ILI MUWE NA USHINDI KWA KILA UOVU NA KUISHI MAISHA MATAKATIFU.
NAWATAKIA SIKU NJEMA YENYE MAFANIKIO TELE, AMANI MOYONI NA FURAHA DAIMA.
Na. Ev. Eliezer Mwangosi - 0767210299. Email: eliezer.mwangosi@yahoo.com
No comments:
Post a Comment