Ibada bila nyimbo za sifa haijakamilika, kazi kubwa inayotendwa na malaika katika ibada MBINGUNI ni nyimbo.
Pamoja na kusifu nyimbo za injili :-• HUONYA
• HUPALIZA MAOMBI
• HUUISHA
• HUGANGA NA KUAMSHA MATUMAINI UPYA KWA MOYO ULIOVUNJIKA
NA KUKATA TAMAA
• HUPALIZA MAOMBI
• HUUISHA
• HUGANGA NA KUAMSHA MATUMAINI UPYA KWA MOYO ULIOVUNJIKA
NA KUKATA TAMAA
Maelfu ya watu waliofurika katika sikukuu za vibanda(makambi) jana
tarehe 22/07/2015 katika kanisa la WAADVENTISTA WASABATO MABATINI
walibarikiwa na huduma ya nyimbo zilizoimbwa na kwaya mbili,
Kwaya ya WAADVENTISTA WASABATO TEMEKE YA JIJINI DAR ES SALAAM ambao ndio
wageni rasmi wa Kambi hilo na KIRUMBA ADVENTISTI KWAYA ya Jijini Mwanza
Tanzania ambao walialikwa kutoa huduma ya Uimbaji kwa siku moja.
KIRUMBA ADVENTIST KWAYA inaongozwa na walimu Paschal Vedastus Makalai, Dr. Darlington Onditi na mwalimu Amos Omary Kapesa.
Katika program hii ya uimbaji TEMEKE SDA KWAYA ilikuwa ndio nafasi yao
ya kuitambulisha santuri muonekano kanda ya ziwa yenye jina “NIPE NENO”.
Baadhi ya kwaya ambazo zimekuwa mbaraka katika kambi hili ni kama vile:-
• Mabatini SDA Kwaya, Agano Adventist, Mashiri Adventist, Bugando SDA Kwaya na nyingine nyingi.
• Mabatini SDA Kwaya, Agano Adventist, Mashiri Adventist, Bugando SDA Kwaya na nyingine nyingi.
Mbali na huduma ya nyimbo, BWANA amemchagua mchungaji BEATUS MLOZI WA JIJINI MWANZA kuwa mnenaji mkuu wa kambi hili.
POKEA BARAKA UNAPOKUWA UKISOMA HABARI HII..
Kwaya ya Temeke sda wakihudumu kwa njia ya nyimbo |
Kwaya ya Kirumba sda wakihudumua kwa njia nyimbo |
|
Kwaya ya Temeke na Kirumba wakiimba Haleluya kuu credit:Kirumba sda church |
No comments:
Post a Comment