Mchungaji wa mtaa wa Nyakato na
Mwenyekiti wa kamati kuu inayoratibu mahubiri makubwa Jijini Mwanza
Ibrahimu Alex Juma amesema, zaidi ya Wahudumu 300 kutoka sehemu zote za
Union ya Kaskazini mwa Tanzania wamekwisha wasili na kukabidhiwa kwa
wenyeji wao.
Takribani vituo 180 Vitafanya huduma
ya uponyaji wa kimwili, kiakili na kiroho. Na mahubiri hayo yatafanyika
kwa muda wa wiki tatu.
Mhazini wa Union ya kaskazini mwa
Tanzania Ndugu Dickson Matiko amesema kwa siku 21 tufundishe neno la
Mungu, misingi ya Imani yetu, tutumie Biblia katika mahubiri yetu. Pia
Mhazini huyo amesema kama isemavyo katika Mathayo 24:14 kwamba, Tena
habari njema ya ufalme itahubiriwa ulimwenguni mwote kuwa ushuhuda kwa
mataifa yote na hapo ndipo ule mwisho utakapokuja. Hivyo Hata na sisi
tunatakiwa kuwa nuru kwa wengine ili tuweze kuwaangazia Habari njema.
Awali kabla ya kumkaribisha ndugu
Matiko Katibu wa kamati ya mahubiri makubwa Jijini Mwanza Philip Joseph
kwa kushirikiana na wataalam wa kurusha mahubiri kwa njia ya mtandao.
amesema, “Lengo la kuweka mahubiri hayo kwa njia ya mtandao ni kumsaidia
hata na Yule aliye mbali na Jiji la Mwanza kupata injili mtandaoni”.
Pia ameendelea kusema “Mahubiri
yamewekwa mtandaoni ili kuweza kumfikia mtu yeyote aliye ndani na nje ya
nchi ya Tanzania, kwa wale watakaoamini na kumpokea Yesu Kristo kama
Bwana na mwokozi wa maisha yao wataelekezwa kanisa la waadventista Wa
sabato lililo karibu nao”.
Aidha Joseph amesema mahubiri hayo
yamewekwa katika ukurasa wa Facebook na Twitter. Mwisho aliwaomba watu
wa Jiji la mwanza kutumia Teknolojia habari na Mawasiliano kwa
kujielimisha na kumtukuza Mungu.
Mahubiri hayo pia yanapatikana kwa
njia ya mtandao wa kijamii ujulikanao kama facebook au kwa kufungua
anuani ya mahubiri hayo ambayo ni www.Mwanzaevangelism.org
Aidha matiko amesema kwa wale wasio
kuwa na elimu ya kufungua mtandao watatumia njia nyingine kama vile
kusikiliza Redio, Wasafiri wa daladala na wao watapata kusikia masomo
Hayo . Pia mwenyekiti wa Union ya kaskazini Dr. Godwin Lekundayo na
katibu wa Union Pr. Davis Fue wataungana nasi katika kazi hii kubwa ya
jiji la Mwanza
Na: Aston J. Mmamba
Mkurugenzi wa Mawasiliano SNC
No comments:
Post a Comment