6 SUCCESS LESSONS TO LEARN FROM BILL GATES!

To be the best, you have to learn from the best. Success is a journey, one that starts from many miles away but people only notice when you’ve passed through the hurdles.
There are so many lessons to learn from Bill Gates, and it would help shape your path to success.
1. FAILURE IS NEVER THE END
Every successful person has failed at one point in time and Bill Gates isn’t any different. His first company Traf-O-Data failed because the product Traf-O-Data 8008 which was meant to read traffic tapes and process data wouldn’t work when they tried to sell it to a local county. Bill Gates didn’t stop at this venture and still went on to be the wealthiest man in the world, meaning failure is only possible when you give up.
2. LEARN FROM EACH FAILURE
Learning from a failure is a key ingredient to success, and it’s one Bill Gates rode on to success. Bill Gates and the co-founder of Microsoft, Paul Allen never gave up, they learnt from the mistakes of Traf-O-Data, and today they are the founders of one of the most successful companies in the world – Microsoft. According to Paul Allen: “Even though Traf-O-Data wasn’t a roaring success, it was seminal in preparing us to make Microsoft’s first product a couple of years later”.
In 2011, Paul Allen told Newsweek: “Since then, I have made my share of business mistakes, but Traf-O-Data remains my favorite mistake because it confirmed to me that every failure contains the seeds of your next success.

3. SEEK FOR KNOWLEDGE
People are too lazy to seek for knowledge these days, and you can hardly be successful when you lack knowledge. Bill Gates has always been an avid reader right from his childhood days; he was curious for knowledge and that curiosity helped him become one of the most successful programmers the world would ever know.
According to Bill Gates: “I really had a lot of dreams when I was a kid, and I think a great deal of that grew out of the fact that I had a chance to read a lot.”
Knowledge and curiosity go hand in hand, and they are essential for success.
4. DRIVE/AIM
Never set limitations to your thinking, and that’s one trait that pushed Bill Gates to success. Inasmuch as Traf-O-Data didn’t succeed, the thinking behind it wasn’t average; it was extraordinary and beyond normal. Microsoft was born out of that pattern of thinking.
Paul Allen described Bill Gates as one with a drive for success and a highly competitive and persistent person.
5. FOCUS
You can’t succeed if you are carried away or easily distracted from your goal. Focus is one of the highlights of Bill Gates success, and according to Paul Allen: “Where I was curious to study everything in sight, Bill would focus on one task at a time with total discipline. You could see it when he programmed—he’d sit with a marker clenched in his mouth, tapping his feet and rocking, impervious to distraction.”
6. HAVE A GREAT TEAM
You can hardly ever do it alone, having a great team is really important. Every great president is as good as his cabinet; every CEO is as good as his workforce. According to Paul Allen: “Bill never wanted to lose talented people. ‘If this guy leaves,’ he’d say to me, ‘we’ll lose all our momentum.’”

These six characters have an important influence on Bill Gates road to success: it’s never too late; you can build your way to success too. Start today.
Jake        
elcre

NENO LA LEO | KURUDI KWA YESU

Kurudi kwa Yesu ☝💃
DALILI ZOTE ZINaONESHA DUNIA IKO MWISHON NA TUMEKARIBIA SNA KURUDI NYUMBANI (MBINGUNI)MATUKIO makubwa na ya kutisha yanayotokea leo Duniani ni dalili ya jambo kubwa ambalo liko mbele yetu, nalo ni mwisho wa Dunia. .Maadili yameporomoka sana katika Dunia na hasa katika miji mikubwa. , ulevi,uzinzi,wizi,ujambazi, ushoga ..upendo kupungua..watu kupenda pesa kuliko utu etc ni mambo aliyotabiri yesu Kuwa yatafanyika kabla hajrudi..ni dalili tosha dunia iko Karibu kufika mwisho;. Tuna kazi ya kufanya kuwaonya wakaaji wote wa dunia wasije wakaanguka na kuangamia pamoja na Dunia.But jambo Jema sana ni kwamba YESU atakuja tena kama Mfalme wa Wafalme kila jicho litamuona hapo atakaposhuka katika mawingu ya Mbinguni na utukufu mwingi. Hili ndilo tumaini letu kubwa; kama ilivyo ahadi yake tunatazamia Mbingu mpya na Nchi mpya ambapo hapatakuwepo na maumivu tena wala vilio, wala maombolezo, maana atayafanya yote kuwa mapya Mbinguni Hakutakuwa na machozi tena, hamna maumivu tena, na hakuna huzuni tena (Ufunuo 21:4). Hakutakuwa na utengano tena, kwa sababu ya kifo kitashindwa. Jambo bora juu ya mbinguni ni uwepo wa Bwana na Mwokozi wetu Tutaonana n Yesu uso kwa uso ambaye alitupenda, na alijitoa sadaka mwenyewe ili tuweze kufurahia uwepo wake katika mbingu milele
Watu wote wanaalikwa ili wayarithi mambo haya makubwa ambayo MUNGU ametuandalia, ni mambo ya ajabu ambayo jicho la mwanadamu halijawahi kuyaona wala sikio kusikia. Mambo mazuri ambayo MUNGU amewaandalia wale wote wampendao;
Watu wote wanaalikwa ili wayarithi mambo haya makubwa ambayo MUNGU ametuandalia, ni mambo ya ajabu ambayo jicho la mwanadamu halijawahi kuyaona wala sikio kusikia. Mambo mazuri ambayo MUNGU amewaandalia wale wote wampendao; (2Wakoritho 2:9)

NENO LA LEO: HATARI ILIYO MBELE YETU

 Mithali 16:25 "Iko njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu; Lakini mwisho wake ni njia za mauti."

Wapendwa tunaishi nyakati mbaya sana, nyakati za usiku wa giza nene, wengi wana macho lakini yameshapofuka hayaoni, na wengi wana masikio lakini yamejaa matope wala hawasikii. Wengi wanakufa ghafla bila matumaini.

Hebu jiulize! Ni kweli watu hawazisomi na kuzielewa AMRI za Mungu, Kama zilivyoandikwa kwa ujumla katika, Kutoka 20:1-17?  Je ni kweli watu hawajui kazi aliyokuja kuifanya Yesu kama ya KUOKOA (Kuwapatia Ushindi wa Dhambi), Mathayo 1:21?

Kama kweli vijana na wazee wana macho yanayo ona, na masikio yasiyo na matope; Uzinifu na Uasherati unatoka wapi? Majungu, maneno ya hila na Uongo, hisia mbaya, ulevi, visasi, uonevu, vinatoka wapi?, bila kusahau kwenda kwa waganga wa umizimu kutafuta ulinzi na kuondoa mikosi, kuitumia siku ya SABA ya juma kinyume na agizo la Mungu na mafundisho ya Yesu, na kuwa ndiyo siku ya Starehe, Sherehe na kila ufisadi na uchafu?.

Wakati Shetani anatangaza Ushindi, kwa kuwajeruhi wengi na kuwachukua mateka, akitumia umizimu na manabii, mitume, walimu na watumishi kwa udanganyifu juu ya kweli ya Mungu; Bado tumaini la kuokolewa lipo - FANYA UAMUZI LEO. Hebu kila mmoja aithibitishe imani yake kwa neno la Kweli la Mungu.

Hizi ni nyakati za mwisho: Mungu ambariki kila mmoja anapozitafakari njia zake na kufanya UAMUZI SAHIHI.

NAWATAKIA JUMATANO NJEMA, IWE YA BARAKA TELE.

Na: Ev. Eliezer Mwangosi
Simu: 0767 210 299 - Email... Eliezer.mwangosi@yahoo.com.


Somo La 12 | Mkombozi Wa Ayubu [#Mwongozo Wa Biblia]

Somo limetafsiriwa na Mgune Masatu


(Ayubu 10 & 19, Yohana 1 & 12, Wagalatia 2)

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2011, Bruce N. Cameron, J.D. Marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya New International Version (NIV), copr. 1973, 1978, 1984 International Bible Society, isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo. Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya NIV inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji wa Biblia wa Zondervan. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sehemu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na hukulipata kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

Utangulizi: Ayubu anatufundisha nini kuhusu neema na matendo? Sehemu kuu ya neema ni kwamba Mungu anatuokoa, hatuko kwenye nafasi ya kujiokoa sisi wenyewe. Kwa hakika, kisa cha Ayubu kinatuonesha kwamba hatuna uhodari wa kutosha kuweza kukabiliana na Shetani. Tafakari jinsi Mungu alivyoleta utofauti katika maisha ya Ayubu. Tuliona kwamba Ayubu alianza akiwa mtu mkuu na akamalizia kwa kuwa mtu mkuu – lakini yote haya yanatokana na Mungu. Pia tulijifunza kutoka kwa Ayubu kwamba Mungu anatutaka tutende vyema, wakati Shetani ni mchochezi wa maumivu. Hivyo, lengo la torati ya Mungu ni kutusaidia ili tuweze kuishi vizuri. Tunapomtegemea Mungu tunajifungamanisha na Yeye apendaye na mwenye uwezo wa kutubariki. Hebu tuchimbue somo letu la Biblia ili tujifunze zaidi kuhusu neema!

I.                   Mkombozi Wetu

A.                Soma Ayubu 19:25. Hebu tuangalie muktadha wa kauli ya Ayubu. Ayubu anaendeleaje kwa sasa katika hiki kisa chake? (Soma Ayubu 19:20-21. Ayubu ana hali mbaya sana kiafya.)

1.                  Kwa nini Ayubu anatoa kauli yake juu ya kuishi kwa Mkombozi [Mtetezi] wake katika muktadha huo? (Ayubu anaamini kuwa Mungu yupo, na kwamba katika hatua fulani Mungu atamwokoa.)

B.                 Soma Ayubu 19:26-27. Ayubu anawezaje kumwona Mungu “katika mwili [wa Ayubu] wakati “ngozi yake imeharibiwa?” (Lazima hii inarejea imani ya Ayubu kwamba baada ya kufa, ataishi tena, katika mwili na damu. Yote haya yatafanyika mbele za Mungu.)

1.                  Ayubu pia anasema kuwa atamwona Mungu, na sio mtu “mwingine.” Kuna uwezekano mdogo kwamba Ayubu anafikiri kuwa yeye pekee ndiye atakayemwona Mungu katika siku zijazo, je, unadhani Ayubu anamaanisha nini anapokana kwamba hakuna mtu “mwingine” atakayemwona Mungu badala yake?

a.                   Je, huwa unajiuliza kwamba “wewe,” kwa uhalisia wako, ndiye utakayekwenda mbinguni? (Nadhani hiki ndicho anachokizungumzia Ayubu. Itakuwa ni yeye, na si sehemu yake nyingine, atakayesimama mbele ya Mungu baada ya kifo chake.)

C.                 Soma Ayubu 19:28-29. Jambo gani jingine analoamini Ayubu kwamba litatokea baada ya kifo? (Hukumu. Ayubu anasema kuwa anapaswa kuishi huku akitambua habari za hukumu.)

1.                  Kwa nini ni vizuri – kuishi huku ukitambua kwamba kuna hukumu inakuja?

II.                Mungu Pamoja Nasi


A.                Soma Ayubu 10:2-3. Hii inaturejesha kwenye mada ya Ayubu: Sistahili yote haya, ninahitaji kusikilizwa ambapo Mungu analeta mashtaka dhidi yangu ili nami niweze kuyakanusha. Ayubu anasema maneno gani ya ziada yanayojenga msingi wa hoja ya marafiki wake wanne? (Kwamba Mungu anawapendelea waovu. Wanakosewa kwa niaba ya Mungu. Hili ni shambulizi kwenye haki ya Mungu.)

B.                 Soma Ayubu 10:4. Jambo gani linaendelea mawazoni mwa Ayubu linalomfanya aseme maneno haya kwa Mungu? Hii inahusianaje na mada yake na mada ya marafiki wake ambayo tumeijadili hivi punde? (Ayubu anapendekeza njia nyingine ya kuelezea kitendo cha wazi cha Mungu kutokutenda haki – Mungu haangalii mambo kwa namna ile ile wanaonavyo wanadamu. Si haki ya Mungu ambayo ina kasoro, bali ni mtazamo wa Mungu. Kamwe Mungu hajawahi kuwa mwanadamu.)

1.                  Hii ni hoja ambayo huwa ninaisikia mara zote. Hitimisho langu ni kwamba jambo fulani lina kasoro kwa kuwa sijawahi kupitia uzoefu kama ambao ameupitia mtu ambaye ninamhukumu. Unadhani hii ni kweli? Je, kweli huna uwezo wa kufanya uamuzi sahihi ikiwa hujapitia uzoefu wa mtu unayemhukumu?

C.                 Soma Yohana 1:1-5. Je, huyu “Neno” ni Mungu? (Ndiyo! Naye Neno “alikuwa “Mungu,” huyo “mwanzo” alikuwako, na “vitu vyote” vilifanyika kwa huyo. Yeye ndiye asili [chanzo] ya uzima.)

D.                Soma Yohana 1:10-14. Huyu “Neno” ni nani? (Soma Yohana 1:29. Neno ni Yesu!)

E.                 Angalia tena Yohana 1:14. Maneno haya yanazungumziaje madai ya Ayubu kwamba mtazamo wa Mungu juu ya maisha yetu una kasoro? Kwamba Mungu haelewi uzoefu wa wanadamu kwa sababu kamwe Mungu hajawahi kuwa mwanadamu? (Kwa dhahiri hilo si kweli katika zama za leo. Yesu “alifanyika mwili” na “akakaa kwetu.”)

1.                  Kati ya misamiati yote ambayo Yohana angeweza kuitumia kumwelezea Yesu, kwa nini alichagua msamiati wa “Neno?” (Utakumbuka tulihitimisha kwamba tatizo la Ayubu na marafiki wake ni kwamba hawakuelewa kikamilifu kweli zote. Walikuwa wanatizama kupitia kwenye “uakisi hafifu,” au kama inavyobainishwa katika 1 Wakorintho 13:12 kwamba, “kuona kwa kioo kwa jinsi ya fumbo.” Yesu alikuja kutusaidia ili “tumwone” Mungu vizuri na kwa wazi zaidi.)

2.                  Je, ingesaidia endapo Ayubu angeweza kusoma vitabu vya injili wakati alipokuwa akiyapitia mateso yake? (Angetambua mustakabali wake kupitia kwa Yesu. Yesu, yeye asiye na dhambi, aliteswa na kuuawa ikiwa ni matokeo ya pambano kati ya Mungu na Shetani. Ayubu aliteseka kwa sababu ya pambano hilo hilo!)

F.                  Soma Isaya 53:4-7. Hii inatuambia nini kuhusu mateso ya Yesu? (Ayubu anasema, “nateseka isivyo haki.” Yesu aliteseka kwa ajili ya dhambi zetu wote, zikiwezo dhambi za Ayubu.)

1.                  Tunapopitia mateso, tunapaswa kuwaza [kutafakari] nini?

G.                Nataka kurejea katika Yohana 1:5. Ayubu anasema kuwa Mungu haelewi uzoefu wa wanadamu. Kutokuelewa kwa kweli ku wapi? (Kumo ndani yetu. Sisi ni “giza” na tunalo tatizo la kumwelewa kikamilifu Mungu wetu mkuu na mwenye utukufu.)

III.             Mungu Anatuokoa


A.                Soma Wagalatia 2:11-14. Inaonekana tatizo lililopo ni kwamba Petro alikuwa akila na watu wa Mataifa, lakini kutokana na mashinikizo ya kidini, aliacha. Zingatia zaidi kifungu cha 14. Ni kwa jinsi gani hili ni swali sahihi kabisa kwa Petro? Je, tatizo si kwamba Petro anarejea alikotoka kwa kuishi kama Myahudi? (Hii haileti mantiki kwangu. Ukiangalia kwa undani zaidi, Paulo anaonekana kusema kwamba ikiwa msitari kati ya Wayahudi na Mataifa umefutwa, basi hakuna sababu ya Petro kuacha kula na Mataifa au kwa kuwaambia Mataifa kuwa wanapaswa kuishi kama Wayahudi.)

B.                 Soma Wagalatia 2:15-16. Kwa mujibu wa kifungu hiki, Paulo anarejea “torati” gani? (Kwa dhahiri inaonekana kuwa ni sheria ya mapokeo inayoshughulikia na mtu unayepaswa kula naye na jinsi unavyopaswa kula.)

C.                 Soma Warumi 7:6-7. Sheria gani inarejewa hapa? (Sehemu ya Amri Kumi inayozuia “kutamani” (Kutoka 20:17).)

D.                Soma Wagalatia 2:17-21. Sababu moja iliyomfanya Yesu atufie ni ipi? (Kutuhesabia haki. “tumesulubiwa pamoja na Yesu” na hivyo “hatuishi tena, bali Krisho anakaa” ndani yetu! Ahadi hii inahusika kwenye torati yote, ya aina yoyote, kwa namna yoyote ile utakayoielezea!)

IV.             Mwanzilishi wa Mateso Ashindwa

A.                Soma Yohana 12:30-31. Tunapoangalia kisa cha Ayubu na Yesu, ni nani aliyesababisha mateso yote haya? (Shetani.)

1.                  Yesu anaposema “sasa mkuu wa ulimwengu huu atatupwa nje,” anamaanisha kipindi gani? “Sasa” ni lini?

2.                  Yesu pia anasema “sasa hukumu ya ulimwengu huu ipo.” “Sasa” ni lini?

B.                 Soma Yohana 12:47. Utaona Yesu anasema kuwa hakuja “ili kuuhukumu ulimwengu,” bali kuuokoa. Hii inatusaidiaje kuelewa kauli ya Yohana 12:31 kuhusu kumtupa nje Shetani “sasa” na wakati wa hukumu kuwa ni “sasa?” (Kwa kuwa Yesu anasema kwamba hakuja kuuhukumu ulimwengu, lazima atakuwa anazungumzia jambo lililo nje ya ulimwengu. Nadhani Yesu anazungumzia mazingira kama ambayo tunayasoma katika Ayubu 1:6-7. Kwa kuishi maisha yasiyo na dhambi, kwa kuyashinda madai ya Shetani, kwa kuonesha kwamba katika pambano kati ya wema na uovu Mungu (wema) yuko sahihi na Shetani (uovu) hayuko sahihi, Mungu amemtupa nje Shetani kutoka kwenye baraza la mbinguni na ulimwengu umetoa hukumu juu ya kile kinachoendelea hapa ulimwenguni.)

1.                  Ni kwa jinsi gani Ayubu anafanana na Yesu? (Wote ni mashujaa wa wema dhidi ya uovu.)

2.                  Ayubu alishinda. Yesu aliishinda hukumu yote. Kwa nini ni muhimu kwako na kwangu kupitia uzoefu wa “Ayubu?” Ushindi tayari umeshapatikana? (Utakumbuka fundisho la kwanza tulilojifunza kutoka kwa Ayubu ni kwamba lazima tumtumaini Mungu. Kwa nini? Kwa sababu hatuoni vizuri taswira yote. Sina jibu la swali hili zaidi ya kusema, “Sijui kwa nini bado tunaweza kupitia uzoefu wa Ayubu, lakini kumtumaini Mungu ndilo jibu pekee la wazi.)


C.                 Rafiki, Mungu alishinda na kupata ushindi! Kama ambavyo Ayubu hakuweza kumshinda Shetani, vivyo hivi sisi nasi hatuwezi kufanya lolote bila Mungu. Mungu alifanyika kuwa mwanadamu. Anafahamu vizuri sana jinsi ilivyo kuishi katika ulimwengu uliojaa dhambi. Alikufa kwa ajili ya dhambi zetu na kutupatia uzima wa milele. “Najua ya kuwa Mtetezi wangu yu hai! (Ayubu 19:25.) Rafiki, je, utaipokea zawadi ya Mungu ya kuwa Mkombozi wako na kukupatia njia ya kutokea kwenye huu ulimwengu uliojaa dhambi?


V.                Juma lijalo: Tabia ya Ayubu.

TUKO LIVE SASA TUKO UKUMBI WA SABASABA JIJINI DAR ES SALAAM AMBAPO TUKIO LA KUWAPONGEZA WAPENDWA WETU MR & MRS MCHUNGAJI MAPIMA


 Sasa waweza lipata Tukio hili mojamoja toka ukumbi wa Sabasaba hapa jijini Dar Es Salaam, ingia kwenye wa facebook wa injilileo kwa kubofya hapa>>
LIVE TOKA UKUMBI WA SABASABA

PROGRAMU TUMISHI YA KUWEZESHA WATU KUJUA MAKANISA YALIPO SASA IKO GOOGLE PLAY STORE

 TusaliPamojaApp ni App (PROGRAMU TUMISHI)  maalumu kwa ajili ya kuonesha direction /mahali kanisa lilipo kwa mtu asiyejua eneo kanisa lilipo. Mtu ni yule ambaye eidha ni mgeni kabisa eneo husika kiasi kwamba hata jina la kanisa halijui ama ni mgeni mwenyeji anayejua jina la kanisa ila hajui jinsi ya kufika kanisani hapo. Basi kupitia app hii ataweza kujua mahali kanisa lilipo. Jinsi ya kuipata App hii, ingia playstore kisha andika TusaliPamojaApp bila kuacha space ,App itakuja utaidownload na kuinstall kwa simu yako au kifaa chako cha Android. Au utaweza kudownload kwa kutumia link hii hapa chini https://play.google.com/store/apps/details?id=com.pacoster.tusalipamojaapp

NDOA: HONGERA SANA MCHUNGAJI DOMINIC MAPIMA KWA KUFUNGA PINGU ZA MAISHA NA NEEMA MARWA LEO, TUNAWAOMBEA BWANA AWARIKI NYOTE NA NYUMBA YENU.

KWAYA YA KANISA YA USHINDI SDA IMETOA HUDUMA YA UIMBAJI LEO KATIKA KANISA LA MZIZIMA SDA






 Picha na Chabo Maphoto

KWAYA YA MZIZIMA SDA NA DR PASCHAL DANIEL WALIWEZA KUIMBA KATIKA KWAYA DAY SIKU YA LEO





Dr. Paschal Daniel aliweza kuimba katika Siku maalum ya kwaya mchana wa leo katika viwanja vya shule ya msingi Zanaki ambapo lipo kanisa la Mzizima.

WAIMBAJI TOKA NEW JERUSALEM BROTHERS WAMESHIRIKI KATIKA KWAYA DAY LEO MZIZIMA SDA

 Sabato ya leo imekuwa yenye mbaraka kwani wapendwa hawa waliweza kuimba wimbo kwenye viwanja vya shule ya Msingi Zanaki ya jijini Dar Es Salaam ambako lipo kanisa Mzizima sda.





NIFAHAMU MIMI, IFAHAMU BORN TO PRAISE

 Kikundi cha uimbaji cha Born to Praise kimeanza mwaka 2012 hadi leo kinaendelea na huduma ya uimbaji, wafahamu waimbaji wa kikundi hiki hapa hapa @injilileoblog
Na leo tutakuwa Bambino


USICHOKIFAHAMU JUU YA KITABU CHA "PENDO LISILO KIFANI" SEHEMU YA PILI

 
Mwandishi amejadili pia juu ya yale ambayo mwanadamu yeyote, haidhuru awe katika hali gani, akiyafanya atakuwa na sifa ya kuondolewa katika ulimwengu huu wa adha na kuishi katika ulimwengu usio na hata chembe ya taabu. Kundi linaloishi duniani hata leo bila hofu yoyote ya chochote kwani limewekwa huru.

Pendo Lisilo Kifani inakupatia Muonjo wa Wakati Taabu Itakapokoma.  Kwa kusoma kitabu hiki unawezeshwa kuona japo kwa mtupo wa jicho aina ya maisha katika ulimwengu wa raha usiokuwa hata na chembe ya taabu. Maelezo ya mwandishi yanastaajabisha sana.

Ni shauku kuu ya mwandishi kwamba kwa kukisoma kitabu hiki ujue namna ya kuishi kwa tumaini na amani katika ulimwengu huu wa shida, lakini zaidi kwa kufuata maelekezo yake uwezeshwe kuishi kwa namna ambayo utakuwa na sifa za kuishi katika ulimwengu ule usio na taabu wala shida.

Hiki ni kitabu ambacho kwa hakika kila mwanadamu aliyewahi kupata taabu yoyote anakihitaji sana.  Kwa bei ya shilingi elfu mbili tu utapata nakala hii ya ajabu.  Tafadhali dhihirisha pendo lako kwa wanafamilia na marafiki zako kwa kuwanunulia nakala kila mmoja wao nawe utashangaa jinsi watakavyo neemeka.


Maelezo na
MchungajEzekiah Chaboma.
Meneja usambazaji wa vitabu  

Kanisa la waadventista wa Sabato, Union ya kusini mwa Tanzania.

USICHOKIFAHAMU JUU YA KITABU CHA "PENDO LISILO KIFANI" SEHEMU YA KWANZA


Miongoni mwa maswali yanayoulizwa na wengi leo ni juu ya hali ya kusikitisha ya Dunia yetu. Je tumefikaje huko? Hali hii ya Uovu ilianzaje? Wako wengi waliojaribu kutoa majibu lakini yaliyojengwa katika Sayansi na Falsafa. Hata hivyo yanatofautiana sana na kushindwa kukidhi hasa hitaji lenyewe, na kuibua swali jipya kabisa; Ni wapi basi tutapata ukweli halisi?

Kitabu cha Pendo Lisilo Kifani, ambacho kimsingi kimejengwa katika Maandiko Matakatifu, yaani Biblia, kimesheheni majibu ya kweli halisi ya maswali yanayohusiana na mstakabali wako na wa Dunia hii.

Mwandishi, kwa karama ya Mungu, anaeleza juu ya Mwanzo ambao ulikuwa mkamilifu usio na kasoro au dhambi, maelezo ambayo kwa hakika yanagusa sana hisia.

Utashangaa kusoma jinsi dunia hii ilivyokuwa mara baada ya kuumbwa, mwanadamu wa kwanza akikutana na kuzungumza na Mungu katika mazingira mwanana kabisa, yenye maua, mito, wanyama, na ndege wa namna namna.

Ile siri ya Uovu kuibuka ndani ya kiumbe mkamilifu imejadiliwa kwa kina.  Hata hivyo kinachogusa zaidi ni jinsi Mungu alivyofanya hima kuwatahadharisha Adamu na Hawa ili wasiingie dhambi, na zaidi sana kile alichofanya kwa gharama kubwa kuhakikisha kwamba njia inapatikana ya kumtoa Mwanadamu katika dhambi na athari zake na kuikomesha taabu kabisa.  Uajabu wa Pendo lisilo kifani uliodhihirishwa katika kifo cha Yesu, ndio hasa kiini cha kitabu hiki, utafurahi na kunufaika sana kusoma kisa hiki cha ajabu cha kumwokoa mwanadamu.


 Maelezo na
MchungajEzekiah Chaboma.
Meneja usambazaji wa vitabu  

Kanisa la waadventista wa Sabato, Union ya kusini mwa Tanzania.




AMBASSADORS OF CHRIST KUFANYA TAMASHA DISEMBA 24, 2016...WATAKUWA WAKIAZIMISHA MIAKA 20 YA HUDUMA YA UIMBAJI, LITAFANYIKA RWANDA NA HAKUNA KIINGILIO

HII SIO YA KUKOSA, TUNAMALIZA MWAKA TUKIMTUKUZA MUNGU KWA SAUTI ZETU

Somo La 11 | Kutoka Katika Upepo Wa Kisulisuli [#Mwongozo Wa Biblia]

Somo limetafsiriwa na Mgune Masatu


(Ayubu 38 - 42)

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2011, Bruce N. Cameron, J.D. Marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya New International Version (NIV), copr. 1973, 1978, 1984 International Bible Society, isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo. Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya NIV inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji wa Biblia wa Zondervan. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sehemu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na hukulipata kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

Utangulizi: Tunazifahamu hoja, je, ni kweli? Marafiki wa Ayubu wanajenga hoja kwenye kanuni ya kawaida: kwamba kutokutii husababisha matatizo na utii huleta mibaraka. Lazima Ayubu atakuwa hakuwa mtiifu kwa sababu anakabiliwa na matatizo mengi. Ayubu anapinga kwa kutoa madai kuwa yeye ni mwenye haki na kwamba hastahili mateso anayoyapitia. Haki haikutendeka kwake na anamtaka Mungu ampe nafasi ya kumsikiliza ili aweze kuelezea mashtaka dhidi yake. Tukiwa kama hadhira inayofahamu ukweli, tunaweza kusema kwamba pande zote mbili zinasema ukweli. Marafiki wako sahihi juu ya kanuni za kawaida, na Ayubu yuko sahihi juu ya haki yake. Juma hili, Mungu anaingilia kati. Hebu tuzame kwenye somo letu la Biblia ili tusikilize kile anachokisema Mungu!

I.                   Mashtaka ya Mungu

A.                Soma Ayubu 38:1-3. Kuna habari gani njema kwenye ujumbe huu kutoka kwa Mungu? (Inaonekana kama vile Ayubu anaelekea kuupata usikivu ambao amekuwa akiuomba.)

1.                  Mungu anasema kuwa Ayubu anatia “giza” mashauri ya Mungu kwa “maneno yasiyo na maarifa.” Nilidhani tulihitimisha kwamba Ayubu alikuwa sahihi juu ya yeye kuwa mwenye haki. Kwa kuwa Mungu anapaswa kuwa sahihi, je, Mungu anazungumzia jambo gani? (Ayubu hana uelewa wa habari kamili.)

2.                  Ayubu anatiaje mazungumzo “giza”? (Anabainisha kwa lugha nyepesi, na kufunika kwa njia ya giza. Ayubu anabainisha kutokuelewa kwake, hivyo mawazo yake yanatatanisha (yanatia giza) kweli zilizopo.)

3.                  Mungu anajibu “katika upepo wa kisulisuli.” Unadhani Ayubu alikuwa katika hali gani? (Utakumbuka kwamba upepo uliwaua watoto wa Ayubu. Ayubu 1:18-19.)

B.                 Soma Ayubu 38:4-7 na Ayubu 39:19-20. Majibu kwa maswali ya Mungu ni yapi? (Hapana. Ayubu hakuiumba dunia au mnyama yoyote.)

1.                  Nimechomoa baadhi ya maswali kutoka sura ya 38 na 39. Maswali yote ya Mungu yaliyosalia yapo kwenye mwelekeo wa aina moja. Kama ungekuwa mwanasheria wa Ayubu, na kwamba mashtaka haya yalikuwa halisi, je, ungesema nini? (Ningepinga kwa mujibu wa uhusiano. Alichokiomba Ayubu ni kwamba mashtaka dhidi yake yawekwe hadharani ili aweze kuyajibu. Maswali haya yanakabiliana na umahiri wa Ayubu maishani.)


C.                 Soma Ayubu 40:1-2. kama ungekuwa mwanasheria wa Mungu, ungejibuje kwenye pingamizi la uhusiano? Swali hili linaashiria nini juu ya jibu la Mungu? (Madai ya Ayubu ya kutaka kusikilizwa yana nadharia isiyo ya kweli. Nadharia hiyo ni kwamba Mungu anawajibika kisheria kumjibu Ayubu. Maswali ya Mungu yanaitia changamoto nadharia hii. Ayubu ni nani hadi amuulize Mungu maswali? Mwanadamu ana uzoefu na umahiri wa namna gani kiasi cha kumpa Mungu changamoto? “Je, mwenye hoja atashindana na Mwenyezi Mungu?”

II.                Jibu la Ayubu kwa Maswali ya Mungu ya Kiuchunguzi

A.                Soma Ayubu 40:3-5. Unalichukuliaje jibu la Ayubu? Amekuwa akidai kwamba mashtaka dhidi yake yabainishwe. Jambo hili linaendanaje na nafasi ya Ayubu ya awali? (Ayubu ameyaondoa madai yake ya kutaka kusikilizwa. Ametambua kwamba hastahili kudai yote hayo kutoka kwa Mungu.)

1.                  Je, hili ni fundisho kwa ajili yetu leo? Tunapojaribiwa kusema kwamba Mungu hatendi haki, je, tunapaswa tu kuweka mikono yetu kwenye vinywa vyetu na kukaa kimya?

a.                   Maelezo ya kitabu cha Mwanzo juu ya Uumbaji na Anguko yanaonesha kuwa Mungu aliwapatia wanadamu uhuru wa kuchagua. Tunaweza kumkataa Mungu. Je, uhuru wetu wa kuchagua tuliopewa na Mungu unaendana na wazo la kwamba Mungu anapoonekana kutuangusha, tunapaswa kufunika vinywa vyetu na kukaa kimya?

B.                 Soma Ayubu 40:8. Je, umewahi kusikia jambo hili? (Soma Ayubu 8:1-3, Ayubu 34:5 na Ayubu 34:12. Ikiwa marafiki wanasikiliza maswali ya Mungu ya kiuchunguzi, yumkini wanapiga kelele na kushangilia “Endelea Mungu, mwambie! Hiki ndicho ambacho kwa hakika tumekuwa tukimwambia Ayubu.”)

C.                 Soma Ayubu 40:11-14. Nataka nijikite kwenye fungu la 14. Tunapotenda dhambi, je, tunamkosea nani? (Katika Zaburi 51:3-4 Daudi anasema “Nimekutenda dhambi Wewe peke yako.” Tunaweza kuwadhuru watu wengine kutokana na dhambi zetu, lakini dhambi i dhidi ya Mungu peke yake.)

1.                  Mungu anaposema katika Ayubu 40:11-14 kwamba anaweza kumpondaponda mtu mwovu mwenye kiburi, inaleta mantiki kwamba anafanya hivi kutokana na dhambi yetu dhidi Yake. Kuna fundisho gani katika Ayubu 40:14? (Kuhesabiwa haki kwa njia ya imani. Kama ilivyokuwa kwa Ayubu, hatuwezi kukabiliana na Mungu. Kamwe “mkono wetu wa kuume” hauwezi kutuokoa. Tumaini letu pekee lipo kwenye kile ambacho Yesu ametutendea.

D.                Soma Ayubu 41:11. Mungu anasema nini juu ya mtazamo kwamba Mungu anawajibika kwa namna fulani hivi kwa wanadamu?

1.                  Hadi sasa hoja ya Mungu imekuwa ikihusu uwezo na mamlaka. Kwa dhahiri, Mungu anavyo vyote viwili. Je, uwezo unapaswa kutoa majibu kwa vitendo visivyo vya haki?

III.             Hitimisho la Ayubu

A.                Soma Ayubu 42:1-3. Ubashiri wangu ni kwamba takribani kila mtu alijibu swali lililotangulia la “Ndiyo, uwezo unapaswa kuwajibika kwa vitendo visivyo vya haki.” Je, sasa Ayubu anatoa jibu gani? (Kama ambavyo kwa ujumla ni kweli kwamba matendo sahihi huleta mibaraka na matendo mabaya huleta matatizo, vivyo hivyo kwa ujumla ni kweli kwamba uwezo na mamlaka vinapaswa kuwa vya haki. Hata hivyo, katika hii hali mahsusi, Ayubu anasema “sikufahamu.” Tunawezaje kumwita Mungu aje atoe maelezo wakati hatujui kweli zote?

B.                 Soma Ayubu 42:4-6. Nini kinamfanya Ayubu aseme, “najichukia nafsi yangu, na kutubu katika mavumbi na majivu?” (Ayubu anakutana na Mungu wa Ulimwengu.)


1.                  Je, Mungu ana haja ya kujibu viwango vyetu? (Hapana. Mungu anasema kuwa aliumba kila kitu. Hafananishwi na mwanadamu mwenye uwezo mkuu na mamlaka. Kiuhalisia aliumba na anamiliki kila kitu. Hawajibiki kwa wanadamu. Hahitaji kujielezea.)

2.                  Ikiwa unakubaliana kwamba Mungu hahitaji kujielezea kwetu, je, unatoa maelezo gani juu ya Ayubu 1 & 2? Kwa nini Mungu anatufunulia kisa chote? (Kwa sababu Mungu anatupenda. Kwa kuwa anatupenda, anataka turidhike na maamuzi yake, kivyovyote vile hawajibiki kwetu, lakini kutokana na upendo wake anatupatia maelezo.)

IV.             Marafiki

A.                Soma tena Ayubu 42:6. Unadhani marafiki wa Ayubu wanafikiria nini katika hatua hii? (Bila shaka wanajisikia furaha maneno yao kuthibitishwa kutokana na kile alichokisema Mungu. Inaonekana walikuwa sahihi, na sasa Ayubu ametubu.)

B.                 Soma Ayubu 42:7-8. Mambo yamebadilika! Sasa, nani yuko sahihi? (Mungu anasema kuwa marafiki “hamkunena yaliyo sawa katika habari zangu, kama alivyonena mtumishi wangu Ayubu.” Hivyo, Ayubu yupo karibu zaidi na ukweli kuliko marafiki.)

1.                  Hii inawezaje kuwa kweli kwa sababu Ayubu alishatubu (Ayubu 42:6)? Kibaya zaidi ni kwamba, katika somo letu Mungu alianza kwa kusema kuwa Ayubu alikuwa “anatia giza” mashauri ya Mungu kwa “maneno yasiyo na maarifa” (Ayubu 38:2). Unaelezeaje jambo hili? (Mambo mawili. Kwanza, Ayubu yuko kwenye tishio na hii inawafanya watu waseme mambo ambayo katika hali ya kawaida wasingeyasema. Marafiki hawako chini ya tishio na hawana huruma kiasi hicho. Pili, Ayubu yuko sahihi kwamba yeye ni mtu mwenye haki ambaye hastahili mambo yaliyomtokea. Ingawa marafiki wanasema ukweli wa jumla, kanuni ya jumla huwa haihusiki nyakati zote. Hawamwakilishi Mungu wanapochukulia kwamba mambo magumu yanayotokea maishani kila mara yanaakisi kutokuwa na utiifu kwa Mungu.)

C.                 Soma Waebrania 11:35-38. Ukisoma muktadha wa hivi vifungu, utaona kwamba baadhi ya mashujaa wa imani waliteseka na kupitia mambo ya kutisha. Ni kwa jinsi gani wanafanana na Ayubu? Hii inapaswa kuathirije mtazamo wetu juu ya kanuni ya jumla?

D.                Soma tena Ayubu 42:7. Mungu anazungumza na marafiki wangapi? (Elifazi na marafiki wake wawili, Bildadi na Sofari.)

1.                  Marafiki wangapi walikuwa wanahojiana (wanabishana) na Ayubu? (Soma Ayubu 2:11 na Ayubu 32:1-4. Pamoja na marafiki watatu wa awali, tulitumia somo zima kujadili hoja ya Elihu iliyojaa hasira dhidi ya Ayubu.)

E.                 Kwa nini Mungu hamhukumu Elihu au kumtaka amsihi Ayubu amwombee? (Tulipojifunza kauli za Elihu juma lililopita, tuliona kwamba baadhi ya kauli zilikuwa sawa (zilifanana) na zile zilizotolewa na marafiki watatu wazee. Lakini, kauli nyingine zilikuwa tofauti. Kwa mfano, katika Ayubu 32:8-9 na Ayubu 32:18-19 Elihu anadai kwamba Roho Mtakatifu ananena kupitia kwake. Hapo awali hatukusoma hoja zote za Elihu, lakini katika Ayubu 36:22-23 Elihu anajenga hoja kwamba wanadamu hawana nafasi ya kumshtaki Mungu kwamba ametenda mambo mabaya. Ukipitia kwa haraka haraka Ayubu 36:26-37:24, utaona kwamba Elihu anatoa kauli ile ile ya “Mungu ni Mungu na wewe si Mungu,” kauli ambayo Mungu anaitoa katika sura inayofuata. Mambo ya muhimu kuzingatia ni kwamba Elihu anatarajia mambo ambayo Mungu atayasema, na nadhani hiyo ndio sababu hahukumiwi.)

F.                  Rafiki, nadhani fundisho kwetu ni kwamba tusifanye haraka kuwahukumu watu wengine pale tunapotumia mantiki ya kibinadamu, badala ya kuichunguza dhambi halisi. Elihu anatufundisha kwamba njia bora ya kuithibitisha tabia ya Mungu ni kujielekeza kwenye utukufu Wake, badala ya kujielekeza kwenye dhambi za wanadamu. Je, utatafakari upya jinsi unavyokabiliana na dhambi ya dhahiri kwenye maisha ya watu wengine?


V.                Juma lijalo: Mkombozi wa Ayubu.